Kipi kinafanya wasomali wagombane?

getrusa

JF-Expert Member
Aug 16, 2013
2,150
1,812
Niko hapa Ndola Zambia, ninapata kifungua kinywa kwenye moja ya mgahawa wa mwanamke wa kisomali eneo hili ni kama kituo cha wasomali, kuna wasomali wengi sana hapa chakula kinachopikwa ni cha kisomali lugha inayotumika ni kisomali.

Wanaonekana kuwa na umoja na Upendo baina yao, kuna vicheko na bashasha.

Swali langu je, kama upendo huu ndio walio nao kipi kinawafanya wakimbie Nchi yao?

Ninaowaona hapa ni wasomali wa rangi tofauti japo utawatambua kwa sura zao na muonekano wao, Je ni kipi kinachowakimbiza Somalia..?

Mwenye ufahamu wa kutosha naomba msaada.

Nimependa kuja kula hapa sabbu wanaweza pia kuwasiliana kwa kiswahili na baadhi yao wanapenda sana Tanzania.
Nawasilisha
 
kulazimisha mechi za play off kuonyeshwa live na Azam Tv wakati Pamba na GGM hawana mkataba na Azam sio usomali huo,,
 
  • Thanks
Reactions: Drs
Tatizo kule kwao wanabaguana KIKOO/KIKABILA. Machafuko yao ni kutokubaliana ukoo gani ushike hatamu za uongozi. Kilaa ukoo unataka kuwa juu.
 
Jamaa wanapenda vita hao....muulize mmarekani( Black hawk down).....waulize vijana wa Uhuru Kenyatta yanayowakuta

**baada ya breakfast mchana piga beche la mandi hapo
 
Japo wanapozungumza naona wote kama Lugha yao ni moja huenda labda wanajuana zaidi wakiwa kwao lakini kwa mtu wa Nje nadhani ni ngumu sana kuzitambua hizo koo.
Tatizo kule kwao wanabaguana KIKOO/KIKABILA. Machafuko yao ni kutokubaliana ukoo gani ushike hatamu za uongozi. Kilaa ukoo unataka kuwa juu.
 
Wasomali wana
1. Lugha moja
2. Dini moja
3. Koo tofauti....hapo ndio kuna maneno
Kama wanyarwanda vile.
Dini moja
Lugha moja
Pua tofauti
 
binadamu pamoja na kua na akili nyingi lakini ni wanyama kama wanyama wengine tu. chunguza vizuri kwanini wanyama hususani 'social animals' wanaoishi kwa familia/koo kama vile simba, sokwe, siafu na mchwa wanapigana tena vita za kufa mtu na familia/koo nyingine.
 
Niko hapa Ndola Zambia, ninapata kifungua kinywa kwenye moja ya mgahawa wa mwanamke wa kisomali eneo hili ni kama kituo cha wasomali, kuna wasomali wengi sana hapa chakula kinachopikwa ni cha kisomali lugha inayotumika ni kisomali.

Wanaonekana kuwa na umoja na Upendo baina yao, kuna vicheko na bashasha.

Swali langu je, kama upendo huu ndio walio nao kipi kinawafanya wakimbie Nchi yao?

Ninaowaona hapa ni wasomali wa rangi tofauti japo utawatambua kwa sura zao na muonekano wao, Je ni kipi kinachowakimbiza Somalia..?

Mwenye ufahamu wa kutosha naomba msaada.

Nimependa kuja kula hapa sabbu wanaweza pia kuwasiliana kwa kiswahili na baadhi yao wanapenda sana Tanzania.
Nawasilisha

wamerikani ndio waliowafanya wapigane wao kwa wao sababu somalia ina mafuta na gas nyingi sana kuliko nchi za kiarabu pili wanasamaki wengi wakila aina kwenye mwambao wa bahahari yao bahari yao kwa chini kuna shimo kama vile ngorongoro creater ardhi iliteremka chini samaki wapo wengi sana somalia ina uchumi mkubwa sana tatu wasomali 100% uwezi kumkuta mkristo never and ever wote ni waislamu
 
Kwa maana ya kwamba hakuna makanisa Somalia.? Je ipi ni historia ya Taifa la Somalia
 
wamerikani ndio waliowafanya wapigane wao kwa wao sababu somalia ina mafuta na gas nyingi sana kuliko nchi za kiarabu pili wanasamaki wengi wakila aina kwenye mwambao wa bahahari yao bahari yao kwa chini kuna shimo kama vile ngorongoro creater ardhi iliteremka chini samaki wapo wengi sana somalia ina uchumi mkubwa sana tatu wasomali 100% uwezi kumkuta mkristo never and ever wote ni waislamu
Kwa hili la wamarekani na Siasa za Africa nakubaliana nawe kwa kiasi kikubwa sana!
Leo Sudan kama Taifa kubwa Kaskazini mwa Africa imesambaratika mafuta ya Sudan yanavunwa na mabeberu wakati sie wenyewe tukipigana wenyewe kwa kelele za Democrasia Angalia Sudan iliyobaki nayo pia inaelekea kupotea ..
 
Back
Top Bottom