Kipi kinaendelea ujenzi wa soko kuu la kisasa la jiji la Mwanza?

Dr Akili

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
4,952
4,324
Ni zaidi ya mwaka mmoja sasa tangia eneo la soko kuu la jiji la Mwanza lizungushiwe uzio kupisha ujenzi wa soko kuu la kisasa.

Tuliambiwa fedha za ujenzi huo zipo na kwamba ujenzi utachukua miezi 6 tu na kwamba tuwavumilie kulifunga soko hilo pamoja na barabara ya Rwegasore na stand kubwa ya taxes na daladala.

Hadi sasa hakuna dalili ya cho chote kinachofanyika humo. Nini kimetokea?
 
Mi niliona ni siasa make mwaka jana mwishoni mwa mwezi wa 10 nilipita nikaona uzio afu narudi mwaka huu mwezi wa 4 nakuta hakuna kitu chochote afu sisikii ata msumali ukidondoka mle ndani ya uzio nikajua hapo sasa huwa tunajinadi kuwa tu fweza za kutosha kumbe hakuna kityuuu.

Bongo kuna mambo sana! Kuna sehemu moja inaitwa kahama inapakana na Busweru hilo eneo walianza kusimamisha nguzo za umeme mnamo mwaka 2017 ila mpaka kesho umeme utakuwa haujawasha.

Bongo n maneno na siasa kuliko kutatua matatizo ya wananchi ila hii ilikuwa ni nyongeza
 
Kama vipi watoe mibati yao mambo yaendelee maana watu washaanza kulifanya eneo choo mbadala..,wanakojoa kwenye makopo wanatupa mule...kuna siku nilipita nikakuta wamefungua nikayaona mengi kinyama😬😬😬.
 
Yaani inakera sana. Wamachinga waliokuwa wakifanya biashara zao humo wakasambazwa kwenye barabara nzuri ya lami iliyojengwa na TARURA ya kutokea Hospitali ya Agha Khan hadi kanisa la Bugando na kuungana na Pamba road.

Barabara hiyo nzuri imekuwa haipitiki ikisubiri kukamilika kwa soko kuu hilo la kisasa ambalo lita accomodate pia biashara za machinga hawa. Yaani inakera.

Mkurugenzi wa jiji na Meya wa jiji wanatakiwa wawajibishwe kwa kufunga soko hilo kabla ya maandalizi ya ujenzi kuwa tayari. Kipi kiliwafanya wafunge soko hilo faster faster kabla hawajajipanga kuanza kulijenga?
 
Ni zaidi ya mwaka mmoja sasa tangia eneo la soko kuu la jiji la Mwanza lizungushiwe uzio kupisha ujenzi wa soko kuu la kisasa.

Tuliambiwa fedha za ujenzi huo zipo na kwamba ujenzi utachukua miezi 6 tu na kwamba tuwavumilie kulifunga soko hilo pamoja na barabara ya Rwegasore na stand kubwa ya taxes na daladala.

Hadi sasa hakuna dalili ya cho chote kinachofanyika humo. Nini kimetokea?
Tunamalizia uwanja wa ndege kwanza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom