Kipi kinaanza, Maisha bora kwa kila mtanzania, tumaini lililorejea au safari yenye matumaini?

Njaare

JF-Expert Member
Sep 26, 2010
1,081
275
Wana Jamvi,

Mimi ninaamini kuwa ilitakiwa kuanza safari ya matumaini. Safari ikikolea au ikifika mwisho tunapata tumaini lililorejea. Tumaini likisharejea, kila mtanzania anaishi maisha bora.

Mimi hapa nimechanganyikiwa kutokana hizi slogans zinazosemwa na kundi hili la wanamtandao lililotuwekea rais mwaka 2005. Mwaka 2005 likijiita wanamtandao, kabla ya uchaguzi likitumia baadhi ya watu walikuwa maarufu na kuheshimika sana katika jamii (sasa hivi hawasikiki na ninadhani hawaheshimiki tena) walituambia mgombea toka wanamtandao hao ni tumaini lililorejea. Wakazidi kutuambia kuwa sasa wanaleta maisha bora kwa kila mtanzania.

Tukaamini tukijua kuwa sasa hawa jamaa watazitumia rasilimali zetu tulizonazo kuboresha afya, elimu na huduma nyingine za kijamii. Tuliamini kuwa hawa jamaa watawasimamia na kufufua sekta ya viwanda na usafirishaji ili wakulima tuweze kuongeza thamani ya mazao yetu.

Tuliamini sana kuwa asasa watakuja na mpango wa kukusanya mapato na kupunguza utegemezi wa bajeti na kupunguza mzigo wa kodi kwa wafanyakazi. Kumbe loh! Jamaa miaka kumi inapita bado bajeti inategemea bia na sigara kama vyanzo vikuu vya mapato ya ndani!

Leo 2015, kundi lile lile linatuambia kuwa lilipoteza lile tumaini walilotuambia mwaka 2005 sasa tunaanza safari ya kusaka tumaini? My God! Kwa maana nyingine kundi hili lililojibadili jina na kujiita Friends of Lowasa linataka kutuambia kuwa badala ya kuleta mabadiliko chanya ya kutumia lile tumaini lililorejea 2005 kuleta maisha bora kwa kila mtanzania, walipoteza tumaini hilo.

Kwangu mimi ninauona huu ni zaidi ya usanii na ni uhuni uliokubuhu na dharau kwa watanzania na ninamuunga mbunge mmoja aliyesema watanzania wakiirudisha CCM madarakani atatafuta consultancy wa kuwapima akili. Na mimi nasema, CCM wakimrudisha mwanamtandao mwingine kugombea itabidi nijiulize kama CCM kuna watu wako timamu.
 
wanatapatapa hawana jipya. wametudanganya vya kutosha, uongo umeisha, mbinu zimekwisha, vijana hawataki tena pilau, kofia, kanga wala tisheti.
 
CCM wako makini , tusubiri mtu safi. Hakuna zaidi ya CCM kuliongoza hili taifa kwa sasa.
 
wanatapatapa hawana jipya. wametudanganya vya kutosha, uongo umeisha, mbinu zimekwisha, vijana hawataki tena pilau, kofia, kanga wala tisheti.

Kanga , Kofia na tisheti ni lazima na siyo kwa CCM tu, hata CHADEMA huwa wanawavalisha makamanda wao kofia, skafu n.k. huwezi kufanya uchaguzi pasipo utambulisho wa chama chako.
 
Mwisho Wa Ccm Umekalibia MUNGU Kaamua Kuwahalibia Lugha

Kweli Mungu kaamua kuwaharibia Lugha, wakati Marry Nagu akiongea kwa mbwembwe kuwa umaskini wa watanzania unapungua kwa kasi, Team EL inasema tunaanza safari ya matumaini. Wanaongea Lugha gongana kama wale wajenzi wa mnara wa babeli!
 
Wana Jamvi,

Mimi ninaamini kuwa ilitakiwa kuanza safari ya matumaini. Safari ikikolea au ikifika mwisho tunapata tumaini lililorejea. Tumaini likisharejea, kila mtanzania anaishi maisha bora.

Mimi hapa nimechanganyikiwa kutokana hizi slogans zinazosemwa na kundi hili la wanamtandao lililotuwekea rais mwaka 2005. Mwaka 2005 likijiita wanamtandao, kabla ya uchaguzi likitumia baadhi ya watu walikuwa maarufu na kuheshimika sana katika jamii (sasa hivi hawasikiki na ninadhani hawaheshimiki tena) walituambia mgombea toka wanamtandao hao ni tumaini lililorejea. Wakazidi kutuambia kuwa sasa wanaleta maisha bora kwa kila mtanzania.

Tukaamini tukijua kuwa sasa hawa jamaa watazitumia rasilimali zetu tulizonazo kuboresha afya, elimu na huduma nyingine za kijamii. Tuliamini kuwa hawa jamaa watawasimamia na kufufua sekta ya viwanda na usafirishaji ili wakulima tuweze kuongeza thamani ya mazao yetu.

Tuliamini sana kuwa asasa watakuja na mpango wa kukusanya mapato na kupunguza utegemezi wa bajeti na kupunguza mzigo wa kodi kwa wafanyakazi. Kumbe loh! Jamaa miaka kumi inapita bado bajeti inategemea bia na sigara kama vyanzo vikuu vya mapato ya ndani!

Leo 2015, kundi lile lile linatuambia kuwa lilipoteza lile tumaini walilotuambia mwaka 2005 sasa tunaanza safari ya kusaka tumaini? My God! Kwa maana nyingine kundi hili lililojibadili jina na kujiita Friends of Lowasa linataka kutuambia kuwa badala ya kuleta mabadiliko chanya ya kutumia lile tumaini lililorejea 2005 kuleta maisha bora kwa kila mtanzania, walipoteza tumaini hilo.

Kwangu mimi ninauona huu ni zaidi ya usanii na ni uhuni uliokubuhu na dharau kwa watanzania na ninamuunga mbunge mmoja aliyesema watanzania wakiirudisha CCM madarakani atatafuta consultancy wa kuwapima akili. Na mimi nasema, CCM wakimrudisha mwanamtandao mwingine kugombea itabidi nijiulize kama CCM kuna watu wako timamu.
#Tanzaniampya
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom