Kipi kilichowakumba TDL watengenezaji wa pombe maarufu ya konyagi?

Ngadu01

JF-Expert Member
May 4, 2016
503
792
Habari wakuu,

Mimi ni mfanyabiashara wa pombe kali, wines na bia aina tofauti tofauti kwa jumla na rejareja maeneo flani hapa jijini Dar. Swali langu kwamba ni kipi kilichowakumba Tanzania Distilleries Limited watengenezaji wa konyagi na valuer karibu wiki ya pili sasa mzigo wa konyagi na valuer zilizopo kwenye ujazo wa chupa ndogo za 200 ml upatikanaji wake umekuwa adimu na wenye changamoto nyingi mno tukiwauliza watu wa viwandani kila mmoja anakupa jibu analojua yeye.

Wengine wanasema kuna kifaa muhimu kimeharibika kiwandani wengine wanasema sijui chupa mpya zinatoka Ulaya sasa kama chupa mpya za konyagi zenye filter zinatoka Ughaibuni mbona hata valuer ndogo hakuna? Yani ni full mkanganyiko kwa kweli naomba wahusika wapatapo ujumbe huu watupe ufafanuzi kamili.
 
Matokeo ya kupiga marufuku viroba
 
....Halafu nyinyi wafanyabiashara wa pombe za jumla, hasa bia, majuzi jamaa yangu mwenye bar yake nilimsikia akilalamika kwamba akienda kununua kreti 4 za ilie bia ya Balimi analazimishwa anunue na bia brand nyingine angalau kreti moja, why mnafanya hivi lakini?
 
Mkuu pia sisi kwenye kuchukua mzigo tunalazishwa mfano ili upewe kreti 3000 za balimi lazima kreti 200 ziwe za castle lager au Kilimanjaro ndogo suala la kuforce linakuja ambapo katika hizi via ndogo inayokubalika in safari tu pekee almaruufu kama kirikuu au mwendokasi
 
tangu wapige marufuku viroba wanywaji tumeamia kwenye banana karibuni huku banana moja buku ukipiga 3 chali.
 
Konyagi chupa ndogo faida yake ni ndogo sana, kwa kiasi kikubwa zilikuwa zinapewa backup sana na viroba, na viroba ni product iliyokuwa inabeba almost kampuni nzima kwa sababu ya low cost of production hasa packaging.

Baada ya serikali kupiga marufuku viroba, jamaa wanashindwa ku-cover costs ambazo zilikuwa zinabebwa na viroba, kwa hiyo hata uzalishaji umepungua, hata wafanya kazi wengi sana wamepunguzwa.
 
Mkuu, nikisema kuna wapuuzi pale serkalini utachukia? Wameua ajira za watu na kuondoa mapato ya serkali.
 
huku maeneo ya mbezi, tegeta, wazo hadi bunju kuna konyagi ya kupima inauzwa kwenye chupa lita moja ikijaa ni 5000, juzi nimenunua yani ni konyagi pure na sasa inanyweka sio mchezo!
 
Back
Top Bottom