Kipi kifanyike ili kutibu ama kuondoa tatizo la chumvi majumbani?

King Rabbit

JF-Expert Member
Mar 29, 2015
590
1,000
Ushauri, maoni yote yanakaribishwa kwa yeyote mwenye mawazo chanya katika kuondoa au kumaliza tatizo la chumvi majumbani kwetu.

1. Mimi ni mkazi wa Dodoma(Ilazo) na kwa bahati mbaya sana nyumba nyingi wanahangaika na hii kitu na ina tabia ya kula sana maeneo ambako kwa kawaida kuna matumizi makubwa ya maji mfano chooni,bafuni.

2.Kwa bahati mbaya chumvi imetafuna nyumba yangu ambayo ilikuwa imeshapigwa skimming tayari kiasi kwamba naogopa hata kupiga rangi nahisi nitakuja kutia huruma baada ya muda mfupi.

3. Picha zifuatazo hapo chini ni picha halisi za matokeo ya chumvi.

#Karibuni kwa maoni na ushauri.

IMG20210331121013.jpg
IMG20210331082558.jpg
IMG20210331121138.jpg
IMG20210331121211.jpg

IMG20210331082542.jpg
 
Malchiah

JF-Expert Member
Feb 10, 2021
976
1,000
Pole sana kiongozi.
Angalia ni kwa namna gani msingi wako unaingiza maji,maana tulikuja gundua kuwa maji yakizidi katika eneo,huanza kupanda juu ya nyumba na kusababisha hali hiyo.
Hatua tulizo chukua ni kuweke hata,pia kuzungusha peeving kuzunguka nyumba au kumwaga zege kuzunguka nyumba,lengo likiwa ni kuzuia maji kutokupanda juu.
Baada ya kuona hali hiyo ilibidi tupige cigar kuzuia ukuta kuoza zaidi.
 
Asante mkuu,na baada ya kufanya hivyo tatizo lilisha kabisa???
 
Pablo

JF-Expert Member
Apr 2, 2017
2,449
2,000
Waona hawa jamaa..wanatibu hilo tatizo na hutoona tena likijirudia

NORPAD GS CO.
+255 753 318 131
 
Bemendazole

JF-Expert Member
Nov 14, 2020
666
1,000
Umejenga kwenye ardhi yenye chumvi. Chimba mtaro urefu wa mita moja na nusu kuzunguka nyumba. Jenga mtaro wa upana wa nusu mita kuzunguka nyumba huku upande wa ndani ukiacha matobo ili yanyonye maji yasipande kwenye nyumba. Maji yanayokuwa drained yaelekeze kwenye karo maalum kwa maji ya chumvi.
 
GEMBESON

JF-Expert Member
Apr 15, 2012
1,170
2,000
Hali hii ya Chumvi kula ukuta, hujitokeza sana kwenye kuta za Bafu au vyoo vya ndani.

Suluhisho: Weka tiles kwenye kuta zote za Bafu na choo cha ndani.
 
Hapa kwenye karo siwezi kuelekeza kwenye karo la maji taka??
 
King Rabbit

JF-Expert Member
Mar 29, 2015
590
1,000
Hali hii ya Chumvi kula ukuta, hujitokeza sana kwenye kuta za Bafu au vyoo vya ndani.

Suluhisho: Weka tiles kwenye kuta zote za Bafu na choo cha ndani.
Ndani bafuni pamoja na chooni nmepiga tiles pako safi kabisa shida hapo nje,pako kama jinsi panavyoonekana.
 
King Rabbit

JF-Expert Member
Mar 29, 2015
590
1,000
Pole sana kiongozi.
Angalia ni kwa namna gani msingi wako unaingiza maji,maana tulikuja gundua kuwa maji yakizidi katika eneo,huanza kupanda juu ya nyumba na kusababisha hali hiyo.
Hatua tulizo chukua ni kuweke hata,pia kuzungusha peeving kuzunguka nyumba au kumwaga zege kuzunguka nyumba,lengo likiwa ni kuzuia maji kutokupanda juu.
Baada ya kuona hali hiyo ilibidi tupige cigar kuzuia ukuta kuoza zaidi.
Problem ilikuwa solved mkuu???!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom