Kipi kianze kura ya muungano au katiba mpya?

Fredrick Sanga

JF-Expert Member
Jan 27, 2011
3,153
697
Katika kufatilia hali halisi ya mchakato wa kupata katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, nimeona nami nitoe maangalizo na maoni yangu binafsi.

Zanzibari imeshatunga katiba yake mpya. Je hii katiba ya muungano itagusa mabo yaliyomo katika katiba ya Zanzibari? Kama jibu ni ndiyo, basi hapa kuna kazi ya ziada, maana katiba ya Zanzibari inaweza kuimeza katiba mpya

Je kama wananchi watapenda zaidi mfumo wa serikali tatu. Nani atatengeneza rasimu ya serikali ya Tanganyika? Maana kuna uwezekano wa kuwa na mapendekezo ya serikali tatu kushamiri sana katika mchakato wa hii katiba mpya. Hii itasababisha haja ya kurasimu katiba mbili, yaana ya Tanganyika na ya Muungano.

Je kama wananchi watataka muungano upumzike, watakubaliwa au watafungwa kama wahaini. Kama watafungwa je huu mchakoto utakuwa huru kweli. Mimi napenda muungano uendelee, lakini labda wasioupenda ni wengi? Sijui? Je tume inajua?

Mwaka 1964 nilikuwa bado mdogo sana, lakini sikumbuki kama wananchi waliulizwa kuhusu, haja ya muungano, muundo, na mambo yake. Na kama kweli kuna mkataba wa Muungano, uko wapi? unasemaje? Je kuna tofauti kati ya mkataba wa muungano na hati ya muungano?

Inasemekana kuna hati zimefichwa, kama ni kweli ni kwanini? Muungano ni haki ya umma au serikali? Kama zipo, huu sio wakati muafaka wa kuzichapisha katika magazeti ya serikali? ili nasi tujue yaliyomo ili kuondoa haya mambo ya uvumi uvumi. Yanawapa watu visingizio vya kuzungumza mengiiii.

Naona kama kuna haja ya kuangalia vizuri sana huu mchakato wa katiba. Bado naamini kabisa ukifanyika vizuri utamjengea Raisi na bunge letu heshima kubwa sana kihistoria, na nchi kutupatia amani na maendeleo ya kudumu.

Nengeshauri, kwa hali ilivyo sasa, bila kutumia vitisho, maoni ya awali yakakusanywe Zanzibar (Pilot study), ili tume iweze kuwa na roadmap nzuri. Sikubaliani na vitendo vya kihuni, na nategemea vyombo vya sheria vinashughulikia. Ila nahisi kuna kitu cha kuangaliwa kwa umakini sana Zanzibar.

Nayasema haya kwa nia nzuri, nikiamini kutoka moyoni kwamba naipenda nchi yangu, na vizazi vyake vijavyo. Na ningependa sana amani ya kweli katika mfumo wa demokrasia ijengeke na kukomaa kadri miaka inavyoendelea. Bila katiba muafa, nahisi matatizo makubwa mbele ya safari. Kuna haja sana ya kujikana nafsi zetu, katika suala la kutengeneza katiba mpya, yaani tunatikiwa kuwa wayakinifu zaidi, kuliko kubebwa na ushabiki wa aina yeyote ile.

Samahani kwa nikaokuwa nimewakwaza.
 
Je kama wananchi watataka muungano upumzike, watakubaliwa au watafungwa kama wahaini. Kama watafungwa je huu mchakoto utakuwa huru kweli. Mimi napenda muungano uendelee, lakini labda wasioupenda ni wengi? Sijui? Je tume inajua?
Samahani kwa nikaokuwa nimewakwaza.

Wewe kwanini unataka uendelee? Mkuu Fredrick Sanga hapa jamvini nakueshimu sana lakini kwenye red naona ngoja niondoke kwenye hii thread kuepusha shari mkuu sitapenda nitumie neno MASABURI kwako. like niliyokupa ni 98%
 
Mkuu naomba sana usikasirike, ndio maana nikasema, ya wengi yaheshimiwe, lakini hapa tulipo hatujui. Mimi nahashimu hata mawazo yako. Naamini una sababu za kutosha. Samahani kwa kukuudhi.
 
Mim naona mchakato wa katiba ungesimamishwa kwa mda lizingumzwe na kutatuliwa swala la muungano kwanza.
Zanzibar washaunda katiba yao ya kwao inaonesha kabisa kuna mengi yapo katika katiba hiyo pamoja na kuukana muungano.

Je kama suala la mchakato wa kuunda katiba mpya ya jamuhuli ya muungano wa tanzania utaendelea na kukamilika halafu mwisho wa siku mambo ya muungano yakatibuka na ikaonekana watu hawautaki muungano je itakuwaje??
Ni upande upi utakuwa umekula hasara zaidi kama siyo tanganyika?
Kwanza itakuwa haina katiba kabisa.
Pili hasara kwani gharama zilizo tumika kwenye mchakato wa katiba ya muungano ni bora zingeelekezwa kwenye mchakato wa kupata katiba ya tanganyika.
 
Sio tu gharama na muda, hata ufanisi wa mchakato uko mashakani. Maana kama mabavu yatatumika, basi wananchi wataogopa kutoa mawzo.
 
Binafsi nashauri tupige kwanza kura ya maoni kuhusu kuendelea na muungano au la. Halafu kwenye mchakato wa katiba tutajua tunatoa maoni kuhusu lipi. Yaani kama hatuendelei nao basi turudishe serikali ya Tanganyika. Kama tunaendelea na muungano, basi tupendekeze uwe wa namna gani. Na maoni yangu ni either serikali moja au shirikisho. Hii ya serikali mbili sijawahi kuelewa hata siku moja. Naona kama watu waliooana halafu mke anaendelea kuwa kama bachela wakati mume anafungwa na sheria za ndoa. Z'bar wana kila kitu kinachoitambulisha kama nchi wakati Tanganyika imemezwa kwenye muungano. Imefika mahali hata viongozi wanaogopa kuitaja Tanganyika. Siku ya mapinduzi ya Zanzibar inaheshimiwa na kutajwa hadharani. Lakini siku ya uhuru wa Tanganyika tunaambiwa ni "uhuru wa Tanzania bara". Kwanini mapinduzi sio ya Tanzania visiwani? Hii inadhihirisha muungano ulivyoleta athari hadi kwenye fikra za viongozi wetu wa Tanganyika! Kumekuwa na unafiki mwingi sana kuhusu muungano. Ndio maana mimi binafsi siutaki muungano. Ila kama wengi watautaka uendelee basi mapendekezo yangu kuhusu aina ya serikali nimeyatoa hapo juu!
 
Kwa mtazamo wangu huu mchakato wa kutafuta
katiba mpya usitishwa na Serikali ifikirie kwanza
kutatua kiukamilifu hili suala la Muungano manake naona
hizi chokochoko zinaweza kutupeleka pabaya.
Kama ni kura za maoni ziiteshwe kwa haraka tutoe maoni yetu kama tunautaka uendelee au usiendelee
au uwe katika muundo gani.
naamini kwa njia hii tutaweza kumaliza hizi chokochoko.
 
Binafsi muungano sihuitaji kwasababu sioni faida yake na wanaojua faida zake hawataki kuzisema jambo linalonipa shaka kama kweli una manufaa kwa wananchi wa kawaida.
 
Binafsi nashauri tupige kwanza kura ya maoni kuhusu kuendelea na muungano au la. Halafu kwenye mchakato wa katiba tutajua tunatoa maoni kuhusu lipi. Yaani kama hatuendelei nao basi turudishe serikali ya Tanganyika. Kama tunaendelea na muungano, basi tupendekeze uwe wa namna gani. Na maoni yangu ni either serikali moja au shirikisho. Hii ya serikali mbili sijawahi kuelewa hata siku moja. Naona kama watu waliooana halafu mke anaendelea kuwa kama bachela wakati mume anafungwa na sheria za ndoa. Z'bar wana kila kitu kinachoitambulisha kama nchi wakati Tanganyika imemezwa kwenye muungano. Imefika mahali hata viongozi wanaogopa kuitaja Tanganyika. Siku ya mapinduzi ya Zanzibar inaheshimiwa na kutajwa hadharani. Lakini siku ya uhuru wa Tanganyika tunaambiwa ni "uhuru wa Tanzania bara". Kwanini mapinduzi sio ya Tanzania visiwani? Hii inadhihirisha muungano ulivyoleta athari hadi kwenye fikra za viongozi wetu wa Tanganyika! Kumekuwa na unafiki mwingi sana kuhusu muungano. Ndio maana mimi binafsi siutaki muungano. Ila kama wengi watautaka uendelee basi mapendekezo yangu kuhusu aina ya serikali nimeyatoa hapo juu!

Hata mimi nimeliona hilo. Tusije twanga maji kwenye kinu. Sidhani kama hadidu za rejea za tume, zinawezesha kuvuka viunzi vizito. Wangepewa hata mamlaka ya kuitisha kura ya maoni, na kuangalia katiba ipi inaandikwa. Huenda hata ile ya Zanzibari inabidi ipitiwe upya, kuwa na muafaka na mpya.
 
Back
Top Bottom