Kipi kianze Kuharakisha viwanda!! Uwekezaje katika Kilimo au Miundombinu ya Usafirishaji?

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,722
Baada ya kuwasikia Wataalamu wa UCHUMI jana ktk kipindi cha ITV kipimajoto, nikashindwa kupata hitimisho lao la pamoja. Inapokuja kutetea Serikali na mipango yake wanakubaliana na uwekejazi mkubwa katika Miundombinu kama kichocheo cha Maendeleo. Ilipokuja suala la VIWANDA pia wanatetea bila kuwekeza kwenye kilimo cha kibiashara Viwanda itakuwa safari ndefu.

Nikagundua wenda BUDGET Yetu ni Ndogo sana kiasi kwamba inakuwa ngumu kuwekeza vyote simultaneously kufikia ndoto ya VIWANDA.

Wataalamu kipi bora kuanza maana hao wataam (PHDs in Economics) niliona kama wanajichanganya...
 
miundombinu na viwanda simultaneously. kwanza.

kisha kilimo kifuate.

hatimae utakuwa na malighafi zitokanazo na kilimo zinazosafirishwa kiurahisi kabisa katika miundombinu bora kuelekea katika mitambo ya viwanda tayari kwa kuchakatwa na kupata finished goods. biashara. maisha bora.
 
Kwangu vyote hivyo haviwezi kusababisha kuharakisha viwanda. Viwanda vinaweza kuharakishwa kwa kutengeneza uhaba wa vitu kutoka nje au kuvifanya viwe ghali. Create scarcity if imported good au make imported goods expensive.
Kama mango picle ya india itazagaa madukanai na ikawa bei sawa na inayotengenezwa hapa usitazamie mnunuzi atanunua ya hapa. Ubunifu wa watengenezaji uruhusiwe kuchukua mkondo wake. Mtengenezaji wa mango picle wa tz akiandika bidhaa yake imezalishwa kwa teknolojia ya india, ni rahisi kinunulika kuliko kuandika imezalishwa tz. Ni ubunifu tu.
 
Kilimo kwanza wandugu, maisha jamani ni malazi mavazi na chakula , muhimu chakula hakuna maendeleo yoyote atakayo pata mtu kama bado kula kuna msumbua
 
wakati unafanya miundombinu na viwanda, malighafi utakuwa unaimport au.
Tunasema awamu iliyopita JPM kama waziri amewezesha ujenzi kwa kilm nyingi zana za barabara. Huoni kama zinatosha kwa kuanzia ili uwekezaji wa kisasa kwenye kilimo uwe umetapakaa, maana hata kama viwanda havitoshi tutaexport na kupata pesa ya kujengea miundombinu ya kisasa zaidi.
 
Kwangu vyote hivyo haviwezi kusababisha kuharakisha viwanda. Viwanda vinaweza kuharakishwa kwa kutengeneza uhaba wa vitu kutoka nje au kuvifanya viwe ghali. Create scarcity if imported good au make imported goods expensive.
Kama mango picle ya india itazagaa madukanai na ikawa bei sawa na inayotengenezwa hapa usitazamie mnunuzi atanunua ya hapa. Ubunifu wa watengenezaji uruhusiwe kuchukua mkondo wake. Mtengenezaji wa mango picle wa tz akiandika bidhaa yake imezalishwa kwa teknolojia ya india, ni rahisi kinunulika kuliko kuandika imezalishwa tz. Ni ubunifu tu.
Unashauri watu wetu wajengewe Uwezo wa kufanya unayoshauri, Katika pitapita kwenye maonyesho watu wetu wanaotengeneza hivyo vitu wanatengeneza katika scale ya chini sana.
Kuhusu uhaba wa vitu hicho kitu kimeshafanyika ndio maana kodi ilipandishwa ya vitu kutoka nje...
 
Kilimo kwanza wandugu, maisha jamani ni malazi mavazi na chakula , muhimu chakula hakuna maendeleo yoyote atakayo pata mtu kama bado kula kuna msumbua
mimi mwenyewe ni Muumini wa Kilimo kwanza na Technology, Viwanda vitakuja automatically kwa kutengeneza mazingira bora ya Uwekezaji bila kuwa na usumbufu usio wa lazima kwao.
Mfano DR mmoja alisema, Sakata la nyanya kushuka bei, Ilikuwa ni Jukumu la serikali kupitia taasisi zake kuangalia wapi afrika duniani (kama nyanya zinakidhi vigezo) wanauhaba wa nyaya kipindi ambapo hapa bongo creti ni 2000 au bure, kisha wanaorganize wazalishaji vijijni na kuwaunganisha kama emergency plan.
 
Napenda muundo wa viwanda uwe kati na mdogo na kuwe sera,kanuni na sheria kulinda uanzishwaji wa hivyo viwanda.
Na iwe bank maalum kwa ajili ya kuwasaidia.
 
mkuu.

upo kwenye mchakato wa kunajenga kiwanda, malighafi za kazi gani tena? nilidhani mpaka kiwanda kiwe timamu ndo uhitaji malighafi ama?
naomba msawazo wa muda wa yote mawili(Viwanda tunategemea wawekezaji, na Ili waseje EASY DOING BUSINESS Indicator lazima ziwe attractive kuliko washindani wetu EA hivyo ni uncertainty).
Hiyo miundombinu mfano standard gauge reli hadi iishe ni miaka kama minne. LAkini kilimo Makini ni Miezi sita,mitatu kuna watu duniani huko wanashida na vyakula na mazao ya kilimo serikali inakuwa link na kulainisha mazingira, Inajipatia mabillion ya fedha za kigeni, Kisha Wanajenga Hiyo Miundombinu. Kama kuna reliable raw materials na mazingira mazuri kwa kutegemea miundombinu hii iliyopo viwanda vitakuja vyenyewe automatically.

Wazo langu ni Investment in Agriculture and Information Technology as the foundation of Industrialization. Miundombinu ni Matokeo ya Mafanikio ktika hayo, maana iliyopo angalau inatosha kwa kuanzia
 
miundombinu na viwanda simultaneously. kwanza.

kisha kilimo kifuate.

hatimae utakuwa na malighafi zitokanazo na kilimo zinazosafirishwa kiurahisi kabisa katika miundombinu bora kuelekea katika mitambo ya viwanda tayari kwa kuchakatwa na kupata finished goods. biashara. maisha bora.

Hauwezi kuanza viwanda ukafata kilimo. Miundombinu na kilimo vinatakiwa vianze halafu baade vifate viwanda.
 
kwanza miundombinu ndo muhimu kuhakikiasha kila mahala pana pitika vizur umeme wa kutosha unapatikana n.k....i halafu kilimo na viwanda viende kwa pamoja
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom