Kipi kati ya hivi kina nafasi kubwa kukutoa kimaisha?

Ni kile ambacho unakiweza kwa nafasi yako, ndio maana wapo ambao wanavifanya vyote hivyo tena kwa ufanisi. Na pia wapo ambao wanafanya kimoja wapo kwa mazoea ndio maana tunaendelea kulalamika kila siku
Tusiige maisha.
Fact
 
Kutoka ni mchakato unaoweza kuanza na kimoja kati ya hivyo vitatu ulivyovitaja.

Si rahisi kuanza na vyote kwa mkupuo, lakini ukibahatika kasi ya kutoka inakupa kubwa.

Ili utoke ni lazima uwe na lengo mahsusi!.. ufahamu kuwa mafanikio yanafungamana sana na muda, hivyo uwe na nidhamu kwenye mipango na matumizi yako ukielekea kwenye lengo.
 
KUAJIRIWA ndio mwanzo wa kukutoa kimaisha maana kipato utachopata kitakupelekea kuweka akiba kidogokidogo.

Akiba itakusaidia kununua ardhi kwa maana ya shamba au mashamba na utapoanza shughuli za kilimo ukiwa kazini utakuwa tayari waandaa kipato cha ziada.

KILIMO kitategemea ni kipi na chenye kuweza kukuongezea uwezo wa akiba baada ya kuuza mazao utayolima.

Hivyo kama walima matikiti maji, au miwa, au machungwa, maparachichi na mazao mengine ya biashara basi utaweza kufikiria kuaqnza biashara yako mwenyewe huku ukiwa bado upo umeajiriwa.

Ukifikia hatua ya kuweza kufanya BIASHARA iwe mazao (yaani walima au kununua mazao) na ikasimama kisawasawa, basi waweza kujiona umetoka kimaisha.

Kumbuka hakuna njia za mkato katika kutafuta kutoka kimaisha ni lazima upitie hatua moja hadi ingine.
 
Namba 1 kama utafanikiwa kupata ajira ya kisiasa kama ubunge!

Namba 2 kama kukiwa na sera nzuri za kilimo na pia assist ya kupata masoko ya uhakika!

Hiki kilimo cha kutegemea uvune upakilie kwenye fuso na kwenda kumkabidhi dalali Sterio,Boma au Mahakama ya ndizi kisha ndio upate chako ni mambo ya kizamani!

Namba 3 ni uhakika endapo sera kandamizi za kodi kwa mfanyabiashara anayeanza kwa kuunga unga zitaondolewa! Mtu aanze kulipa kodi biashara ikishapata wateja wa uhakika!

Japo wenye mitaji mikubwa wanatoboa katika mazingira haya haya magumu. Hela ikiwepo ya kutoa supp
 
Itategemeana na kiwango cha mshahara utakaolipwa pamoja na posho.

Kama mshahara ni kuanzia milioni 5 kwa mwezi hapo unapiga kazi ya kuajiriwa huku ukijikita kuwekeza kwenye majengo ya biashara (kupangisha wafanyabiashara) ila chini ya hapo bora kwenda kulima na kufuga kisha biashara.

Ila pia kama wewe unapenda kuwa kuwa huru katika kazi zako, na unapenda kuwa karibu na familia yako wakati wote kujiajiri ni chaguo sahihi
 
Wewe lima sii chini ya hekari 10 halafu hela unayopata kaiweke kwenye biashara,then huo ndio uwe mizungukoo wa kila mwaka
 
Kwa kuanzia, kuajiriwa ndiyo itasaidia kukujenga. Baadaye ukiwa katika hali ya kati, waweza ongezea income kwa kufanya biashara wakati unaendelea na kazi ya kuajiriwa. Kumbuka kufanya saving ya mshahara wako, kati ya 15-20%. Hii savings baada ya muda itasaidia kununua assets kama kiwanja, au shamba, na kadhalika.
 
Inategemea na nidhamu yako ya fedha kama ukiajiriwa na ukawa na matumizi mazuri ya fedha, ukalima kilimo Cha mazao ya pesa kama maharage ukiweza panua kilimo mpaka heka tano Hadi kumi hapo faida utayopata kwenye kilimo fungua biashara na uisimamie kikamilifu, Anza na mtaji mdogo huku ukiipanua biashara yako, ukikua kibiashara Jenga majengo ya kupangisha kupitia faida ya biashara, nawasilisha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom