kipi bora Kuwa na 80% ya wakulima ambao hawajitoshelezi au 20% ya wakulima wanaolisha wote na kuuza nje...

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,701
hadi 2008 asilimia mbili ya wamarekani walikuwa ni wakulima lakni wanalima na kulisha sio tu marekani bali wanalisha hadi kutoa msaada nchi masikini.

ni kweli hatuwezi kujilinganisha na mabeberu maana tulipishana itikadi lkn wenda tukawa tunajifunza vitu kutoka mahala pengine.

kipi bora kwa mawazo yako.
kuwe na 20% ya wakulima wanaohudumua 80% ya wananchi waliobaki
au tuendelee na mfumo uliopo sasa tangu enzi za oldvai gorge.

nini maoni yako.
 
Mimi nafikiri tuanze kutoa tafisiri sahihi ya kilimo,kisha tuangalie muelekeo wa uchumi wa kikanda,kisha tuwekeze katika miundombinu ya kilimo,kisha tuweke mawakala wanunuzi wa ndani ili wauze nje.

Hapo kilimo kitakua sawa na kisasa.

Tanzania na uchina ziko sawa kwenye mifumo ya kilimo,ila sisi akili ndogo kama nukta
 
Back
Top Bottom