Kipi bora kuwa kiongozi wa kisiasa kama Waziri au Rais au kuwa mfanyabiashara mkubwa kama Mengi au Mo?

konda msafi

JF-Expert Member
Sep 5, 2018
806
1,000
Hivi hapa duniani kipi ni kitu cha fahari zaidi kati ya kuwa mwanasiasa na kufikia mafanikio ya kuwa waziri au rais kabisa, na kuwa mfanyabiashara bilionea kama alivyokuwa Mengi au Mohamed Dewji (Mo)?

Kuwa kiongozi wa kiasa kuna raha yake, kusafishiwa njia na ving'ora kwa pembeni ukiwa unapita, ulinzi wa kutosha wa TISS, polisi na jeshi, nchi nzima inakujua na full heshima, ukitoa amri kila mtu anatekeleza.

Ukiwa bilionea level ya akina Mo au Bill Gates nako kuna raha yake, full kula bata na kuenjoy life unavyotaka maana pesa sio tatizo kwako. Sasa huwa najiuliza hapa duniani kati ya hivi vitu viwili, kipi kinachokupa ufahari wa hali ya juu.

Kumbuka Mo na mihela yake alitekwa ila mwanasiasa kama waziri au rais sio rahisi kumteka. Pia kumbuka mwanasiasa kuna kustaafu baada ya muda na kuuacha huo utukufu wote wa madaraka, lakini mfanyabiashara haina kustaafu ni kuponda raha hadi kufa labda ufirisike. (Bill Gates hawezi kufirisika).
 

Roadmap

JF-Expert Member
Aug 19, 2013
2,126
2,000
Utakuwa na hela sana mwisho utataka power tu, leo Trump anaweza kumuita Bill gate au Elon Musk muda wowote na jamaa akaenda ila ni ngumu kwa Bill Gate kumuona Trump muda wowote anaotaka.
 

konda msafi

JF-Expert Member
Sep 5, 2018
806
1,000
Utakuwa na hela sana mwisho utataka power tu, Leo Trump anaweza kumuita Bill gate au Elon musk muda wowote na jamaa akaenda ila ni ngumu kwa bill gate kumuona Trump muda wowote anaotaka
Dah! Kwa hiyo mwanasiasa ndio nayetesa hapa duniani kuliko billionea?
 

Dr. Zaganza

JF-Expert Member
Jul 15, 2014
760
1,000
You need money and power by any means, only if you want revenge. Unless, Love is enough to give you everything.
 

T14 Armata

JF-Expert Member
Mar 7, 2017
3,205
2,000
Putin hili swali aliwahi jibu pale wapinzani wake walipokadiria ana dola bilioni 200 zimefichwa kwa assets kadhaa.

Waliomtetea waliwauliza kama anaendeshwa kwenye ndege ambayo hakuna tajiri yeyote duniani anaweza miliki tena ziko Ilyushin tatu, anaishi Kremlin au nyumbani kwake Nova Ogaryovo ambako hakuna mtu anaamua kuishi mwenyewe, ana fleet ya magari maalumu zaidi ya 12 ambayo hayauziki popote, ana heshimika na kulindwa. Haya yote anapata kutoka serikalini.

Then huo utajiri wanaosema utampa nini ambacho hawezi pata kwa sasa. Au kuna tajiri gani duniani ana maisha mazuri kumzidi. So far wanasiasa wezi wanaishi vizuri ila sitamani maisha yao.
 

ighaghe

JF-Expert Member
Mar 25, 2013
2,171
2,000
Siasa katika level ya uraisi huwezi ilinganisha na bilionea yoyote, uraisi ni kiwango cha juu kabisa cha mafanikio. Huku chini uwaziri na mengineyo hamna ishu sana. Cc bilionea wa Alibaba
 

Lob

JF-Expert Member
Jul 24, 2017
409
500
Mfanyabiashara bilionea ni maisha ya kweli hakuna kuigiza kazi kazi tu mpaka unatoboa.
 

alphonce.NET

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
810
500
Utakuwa na hela sana mwisho utataka power tu, Leo Trump anaweza kumuita Bill gate au Elon musk muda wowote na jamaa akaenda ila ni ngumu kwa bill gate kumuona Trump muda wowote anaotaka
Trump hawezi kumwita Gates wakati wowote anaotaka na akaenda. Nguvu ya mamlaka ilivyo Afrika ni tofauti kabisa na magharibi. Kwao Facebook na twitter wanamfungua Rais wa nchi account zake na Rais hawezi kutumia mamlaka yake kuwafanya chochote.
 

Abuu abdurahman

JF-Expert Member
May 9, 2017
986
1,000
Trump hawezi kumwita Gates wakati wowote anaotaka na akaenda. Nguvu ya mamlaka ilivyo Africa ni tofauti kabisa na magharibi. Kwao Facebook na twitter wanamfungua Rais wa nchi account zake na Rais hawezi kutumia mamlaka yake kuwafanya chochote
Mfano mzuri huu uchaguzi wa juzi tu Marekani . Trump alifutiwa tweets zake hadi akakaribia ukichaa na hakuwa nachakufanya zaidi ya kutulia tuu!
 

lyalya

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
329
250
Unajua haya yote yanatokea baada ya Wanadamu kutafuta furaha ndini ya dunia wakati hakuna furaha hana dunia ukipata.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom