Umomi
JF-Expert Member
- Mar 31, 2020
- 677
- 983
To be honest, hakuna kitu kinaumiza graduates nikiwemo mimi kama kusoma huku nikijua kabisa ajira ni ya kusotea sana. Nikipiga mahesabu pesa niliyotumia kusomea chuo kikuu Ni zaidi ya 9.5m ilikuwa inatosha kujiajiri. Naumia sana ila sina cha kufanya. Najua wengi mtahuji kuwa nilisaini mkataba wa kuajiriwa baada kumaliza kusoma.
Jibu ni kwamba kujiajiri naweza sana lakini tayari nimetumia pesa na kupoteza muda mwingi sana kusoma masomo ya chuo kikuu. Yani bora ningeishia form nikafanya mishe mishe make haya maisha niliyaona kipindi cha Corona ni MAGUMU nilikuwa napiga biashara ndogo ndogo ila hali ni ngumu sana. Niseme ukweli kabisa nilianza biashara kwama tarehe 28/3/2020 ila mpaka tunafungua vyuo sikuwahi kupata Faida 20000 kwenda juu kwa siku. Nakumbuka siku nimepata faida kubwa sana nilipata 14500 but siku zingine nilikuwa naishia 4000 mpaka 10500.
Jamani Mimi Kama mhitimu wa Elimu ya juu siyo kwamba sipendi kujiajiri napenda sana lakini mtaani Ni kugumu sana, niseme ukweli kabisa nawaza sana. Ila kinachoniumiza zaidi n kwenda kuanza upya baada ya kumaliza kusoma na umri umesonga sana hivyo hata kwenda kukaa nyumbani ama kwa ndugu naona aibu sana. Mi nimesoma ualimu wa Elimu ya msingi (Bachelor of Education in Primary Education). Naomba hata mwenye connection na shule anifanyie mpango kweli hata nikaanze maisha jmn. Mtaji nimejichanga ila naona hautoshi kwa plani zangu.
Naomba kuwasilisha