Kipi bora kununua Hiace mpya kwa 30M ama kuchukua Tata Marcopolo kwa mkopo

Kiongozi hakuna daladala yenye hesabu ya kulaza 200k, hizi ndio zile hesabu za kulima matikiti, hesabu ni 100k - 150k only, tena pengine na mshahara ukatoa.
Mkuu uda hesabu yake ni kwa siku.pia kumbuka mfanyakazi ndiye bosi mwenyewe
 
Chukua hiyo ya kulaza 200k kwa siku ukipiga mwezi una milioni 6,
Ndani ya miezi sita ukitoa service ndogo ndogo unamaliza deni na kuanza kula faida,

Nb.
Kuwekeza kwenye biashara ya Usafiri kunahitaji Uvumilivu na kujitoa maana muda wowote kitu kikibuma/mnemba unapata lose.
Mm nafanya biashara ya hizo gari mkuu, daladala zinachangamoto.
Kiujumla body ya eicher haiitaji barabara mbovu za shurba tofauti na Tata. Lakin pamoja na hayo unapoweka hesabu kubwa unaongeza muda wa kulaza. Hizo hesabu za 200k ni kulaza gari saa 6 na kuamshwa saa 8 hivyo engine haipoi na unaweza shusha gear box ndan ya miezi mitatu ukapata wazimu kama sio kichaa.
Bishara hii ya daladala kwa ujumla
inachangamoto zifuatazo:-

1. Usimamizi( kujaza mafuta - kituo kimoja na sehem ya kulaza)

2. Service( fundi wako sio wa dereva)

3. Breakdown (how to handle it)

4. Hesabu( 160-180) kulaza saa 3- 4 usiku) na kuamsha kuanzia sa 10 alfajir

5. Vyeti ( clean driving licence)

6. Madereva (age, certified, confidence, defensive driving, uthibitisho wa makazi)
 
Mkuu uda hesabu yake ni kwa siku.pia kumbuka mfanyakazi ndiye bosi mwenyewe
Mkuu nadhani utakuwa umefanya kosa kubwa kuangalia upande mmoja tu wa shilingi. Kumbuka gari huharibika au kupata ajali hata mpya. Ndiyo, unaweza kununua gari mpya ndani ya miezi sita ikapata hitilafu kubwa kwenye injini au gea box. Kumbuka mhindi yeye anategemea kila mwezi utampelekea fungu lake. Ungeniambia unaanza na mtaji wako angalau ningekuelewa kwani ikifeli madhara yake siyo makubwa kama mkopo. Kuliko kukopa ni bora kununua gari la uwezo wako uangalie maendeleo yake. Mara nyingi mkopo kwenye biashara ni mzuri pale unapokuwa tayari unaijua na unataka kuongeza operation zako. Kwa mfano una gari moja tayari na ukaona linafanya vizuri, umepata uzoefu na kujua changamoto zake na kiasi halisi unachoweza kuingiza kwa mwaka mmoja. Hapo ndiyo unaweza kuongeza jingine kwa nia ya mkopo au ukauza lile la zamani na kununua jipya.
 
Mkuu hao wa hindi wanahitaji ulipe angalau 50% ya bei ambayo ni kama 60m kwa hire purchase tena hizo Tata zinalaza 120,000 hadi 150,000 kwa route za Dar manaake utaendesha miaka miwili kumaliza deni Tata hiyo intakua imedepreciate sana, lakini kikubwa zaidi vipuri vya hizo gari nivipya na bei iko juu sana hamna used, utaendesha kwa pressure yeye muhidi hana hasara atakuambia ukate Bima kubwa incase yeye gari lake linarudi......tena mtu mwenye mali ya 120m hawezi kukaa kwenye mlango au usukani stress ninyingi utagonga na pia ma konda na madereva watakupiga vita paka uwachie gari.....unaweza ukafa kabla hujamaliza mkopo huo, jua kila sehemu/kazi inawenyewe acha wazarama waendesha dala dala zao utaumia zaidi tafuta biashara nyingine salama zaidi
Kila biashara ina changamoto, kikubwa ni ku "take risk" unayoweza imudu / kuivumilia endapo mambo yakienda Mrama!
 
Hesabu ya 200k kwa Tata, kuna makubaliano ya mshahara kiongozi na muda wa kulaza gari ni saa 5 au 6, na gari kuamshwa saa 8 au 9, injini haipoi
Inategemea na route....kaulize zile gari za Mnazi mmoja to Kivukoni zinapeleka hesabu gani kwa siku.
 
[
Hesabu ya 200k kwa Tata, kuna makubaliano ya mshahara kiongozi na muda wa kulaza gari ni saa 5 au 6, na gari kuamshwa saa 8 au 9, injini haipoi
Kuna wakati ktk shughuli zangu niliwahi kuwafahamu madereva wawili waliokuwa wakiendesha hiyo ruti ya Mnazimmoja to Kivukoni....

jamaa walinieleza kuna wakati walikuwa wakipeleka 300,000/= TZS kwa bosi kila siku. Na hapo mafuta wameshajaza, na posho wameshajilipa. Ile ruti ina hela nyingi kwa sababu distance ni fupi wakati nauli ni ile ile, 400. Kutokana na ufupi wa route hivyo wanaweza kufanya safari nyingi kwa siku ukilinganisha na yule anayeenda route ya mbali sana.
 
[

Kuna wakati ktk shughuli zangu niliwahi kuwafahamu madereva wawili waliokuwa wakiendesha hiyo ruti ya Mnazimmoja to Kivukoni....

jamaa walinieleza kuna wakati walikuwa wakipeleka 300,000/= TZS kwa bosi kila siku. Na hapo mafuta wameshajaza, na posho wameshajilipa. Ile ruti ina hela nyingi kwa sababu distance ni fupi wakati nauli ni ile ile, 400. Kutokana na ufupi wa route hivyo wanaweza kufanya safari nyingi kwa siku ukilinganisha na yule anayeenda route ya mbali sana.
Haiwezekani walikuongopea (kama wewe ni demu) ili uwawone wako juu, hapo kuna foreni ya kufa mtu pia na magari nimengi na abiria wengi wanapatembea kakuogopa foreni
 
Nakushauri kwa uzoefu, nimetoka Kahama kumpelekea MTU Coaster 24 namba DE ambayo tumnunulia kwa 36m. Nakushauri nunua Coaster iliyo kwenye hili nzuri, itakulipa.

Wakati narudi nikakosa usafiri wa Trinity ya Rwanda, nikapata Coaster ya kampuni ya Travel Partner jamaa ametujaza utadhani machungwa. Nikawaza kuwa kumbe MTU unaweza kuanzisha route ya mchana na ikakulipa sana! Maana Kahama To Dar mafuta hayazidi laki tano na wasafiri wapo!

Wakati tunaondoka juzi tulipata abiria wengi tu njiani na tuliondoka Dar SAA Tisa mchana jumapili!


So kuna fursa kwa kweli. All the best
Miezi hii hamna shida ikifika march na kuendelea 2020 je hali bado itakuwa hivyo?
 
Sijawahi ifanya mkuu. Ndo my first time. Am sure hakuna aliyezaliwa anajua wote tunajifunza
Naam jambo au shughuli yo yote ifanye mwenyewe ujionee, kwani wao waweze wana nini hata sisi tushindwe tuna nini?
 
Wanasajili mkuu.Ishu ni kuongea na sumatra vzuri, Mwanza bado sana kuziondoa hiace ujue. Mji bado ni mdogo sana kulinganisha na dar
Mkuu una uhakika wanasajili au unakisia?....coz mimi kuna mtu wamemkazia route ya kishiri buhongwa..mji umepanuka ndugu...route zimekuwa nyingi...
 
Mkuu una uhakika wanasajili au unakisia?....coz mimi kuna mtu wamemkazia route ya kishiri buhongwa..mji umepanuka ndugu...route zimekuwa nyingi...
Ndo hapo kuongea nao vizuri mkuu ama hunielewi bado. Ama sio ni mkenya nayeongea naye
 
Back
Top Bottom