Kipi bora kununua Hiace mpya kwa 30M ama kuchukua Tata Marcopolo kwa mkopo

mkuu unaweza kupata mkuu au tafuta sehemu huku mjini fungua duka la nafaka ni Bashara inayotembea maana kila siku lazima watu wale.Hardwire risk ni chache sana ukinunua hiyo HiAce ukiona simu ya konda au dereva unaanza kuhisi kuwa gari imegongwa au ajali while kwenye hardwire nondo cement haviozi
Ukiogopa changamoto mafanikio utayasikia kwa wenzio man
 
Vijana tusiogope changamoto .. hakuna biashara nzuri wala mbaya.

Mkuu nakupongeza kwa uamuzi huu japo wenyi watakuja na kusema kuna changamoto , kumbuka kuna matajiri wakubwa wamenzia kwenye daladala.


Mkopo inaweza kukulipa kwa sababu ya makusanyo mazuri kwa siku@keisangora,
 
Hardware inaweza ikanipa 100-150k kwa siku kweli mkuu.
Hardware cement mfuko faida ni 500-1000.
Ninaangalia biashara nitakayotengeneza 150-200 padei. Nimefanya Savei ya biashara nyingi sana na changamoto zake zote.
Asante kwa wazo lako pia
Hata mia 300k kwa siku inapatikana inategemea namtaji namaeneo.
Cement hainapesa kma vitu vya chuma kwenye hardware nondo, flat bar navinginevyo(bati achana nazo).
Tafuta usafir kma canter ya 3.5 tons suply bidhaa 2 au tatu za hardware kwa jumla kwenye maduka ya rejareja kwakutumia usafir wako.
Kwasiku ukiweza kusuply ton 3 au 4 zanondo inatosha kwakuanzia, kwajumla nondo inauzwa kuanzia tani 1 means naongelea wateja 2 au 3 kwasiku ambayo inaweza kukupa 20 tons kwa week ambayo kila ton inafaida ya 70k kwa week inakua ni 1.4m.
Biashara inafaida sababu hata pics moja haiwez kuaribika chance ya hasara nindogo mno plus gari pia inakua haitumik sna
1575460377101.jpeg
 
Bro mimi sina elimu kuhusu magari huo ndo ukweli..ila nimekua angalau nashuhudia Eicher nyingi hudumu kuliko Tata hasa ishu za mashine(injini) pia kibiashara hupendwa zaidi kuliko TATA hasa kwa abiria wenyewe(Muonekano) na hata wamiliki wenzako pia hata ikija ukitaka kuiuza ni rahisi kuliko TATA.

Nimeshea na kushauri asilimia japo 1 ninayoifahamu
Thank you mkuu ubarikiwe. Unaweza ukanipa muda wako kwa kuweka nyama kidogo ni kwa sababu gani na wengine ili tujifunze kwa kuelezea tofauti ya tata na eicher. Nina imani tumezaliwa hata hatuwajui wazazi ila tumekuwa wakubwa tukawajua. Am sure everything is learnable kikubwa uwe tayari kujifunza
 
Kiongozi hakuna daladala yenye hesabu ya kulaza 200k, hizi ndio zile hesabu za kulima matikiti, hesabu ni 100k - 150k only, tena pengine na mshahara ukatoa.
Inategemea na route....kaulize zile gari za Mnazi mmoja to Kivukoni zinapeleka hesabu gani kwa siku.
 
Kuna jamaa yangu ni anazungusha TATA route kkoo-kisewe mbgala wao wanapeleka 150k,ila kuhudumia TATA bora uchukue eicher spare zake ziko affordable kuliko huyo muhindi TATA.Tafuta coaster ipige route za shamba huko pwani to Dar
 
wakubeti,
Mnajua biashara ya kwenye karatasi ni tofauti na ktk uhalisia halisi!!! Naona watu wengi mna base sana kwenye biashara za makaratasi!! Hivi kwenye biashara ya hardware hadi uingize hiyo laki 3 kwa siku sio kazi rahisi hivyo!!! Nondo tani 3-4 kwa siku?!!! Biashara, jamani sio rahisi hivyo!! Hususani kwa uchumi wetu wa sasa huko mtaani!!
 
Lakin mkuu kuna jamaa kakushauri hardware wewe unasema unataka faida kubwa kwa siju, iwe 100k mpaka 150k.
Unaweza ingiza hyo na pesa usiione kutokana na pressure yake. Fanya biashara kwa kiasi cha pesa yako au hatakama unakopa mm sikushauri magari mkuu. Bora hata hyo h/w hatakama utaingiza 50k lakini niyakwako mkuu.
Hii mkuu nitajifanya kuwa kuna tajiri akanipa Gari akaniambia nitafute Dereva mkuu. Namie nitakuwemo kama mfanyakazi. Mana biashara hii changamoto wanasema kuwa ni usimamizi ndo kazi.
So nimeamua niwe naisimamia mwenyewe
 
Mnajua biashara ya kwenye karatasi ni tofauti na ktk uhalisia halisi!!! Naona watu wengi mna base sana kwenye biashara za makaratasi!! Hivi kwenye biashara ya hardware hadi uingize hiyo laki 3 kwa siku sio kazi rahisi hivyo!!! Nondo tani 3-4 kwa siku?!!! Biashara, jamani sio rahisi hivyo!! Hususani kwa uchumi wetu wa sasa huko mtaani!!
Nilipoajiriwa tunazaid ya tani 15 kwasiku
 
Back
Top Bottom