Kipi bora, kufurahia chakula haramu au kuendelea kuvumilia njaa?

2019

JF-Expert Member
Dec 31, 2018
2,982
4,457
Natuamai mko powa.

Toka Rais Samia aapishwe kuna watu wanahisi ni tumaini jipya Tanzania, hotuba hata 5 bado lakini watu wanahisi shida zao zimeisha.

Ni kweli watu wapepata tumaini jipya? Magufuli alianzaje? Tumbua tumbua yake, fukuza fukuza yake, wafanyakazi hewa, vyeti feki, matamko matamu matamu n.k.

Matukio yote hayakufurahisha watu? Bila shaka hata mimi nilifurahi, kabla hajabadili gia wenye maono wakashauri kwanini haya matamko yasitengenezewe sheria ila akitoka yabaki? Watu wakadai hakuna haja wakidhani kesho uhakika.

Sasa mama Samia kaingia, nae mwendo ni ule ule japo yeye katoa uhuru zaidi lakini tuna uhakika na kesho? Leo yupo kesho asipokuepo?

Watanzania tunapaswa kujiuliza tunahitaji matamko,watu au katiba ambayo kila kiongozi atakaekuja ataifuata?

Kama US wangekuwa na katiba na uoga kama wa Tanzania Trump angeibadili na kutawala maisha. Kwa hiyo nyie mnaoshangilia msije lia badae, Samia yuko vizuri lakini bila katiba hakuna jipya kabisa ni swala la muda tu.
 
Mimi naungana na wewe

Kuna vitu vinafanyika tunakuwa na watu wazuri lakini hatuna system nzuri kama tungekuwa na system nzuri basi hata kama tukiwaweka mtu mbaya bado system itafanya kazi vizuri na mtu hata onekana mbaya
 
Mi nadili na kichwa Cha habari tu ni hivi we Bata hakuna chakula haramu! Hata wewe unaweza kuliwa na aliekukula akaishi vizuri tu nimemaliza.
 
Yaan nife njaa na vya haramu vipo?si ntakua msemgerema,acha tule vya haramu kufa njaa na familia yako
 
Back
Top Bottom