Kipi bora, Kufundisha chuo vs Kufanya kazi ya taaluma yako?

vurumai

Senior Member
Feb 9, 2014
178
0
Habari Wadau.

Naomba kuwasilisha mada. Kipi bora kati ya kufundisha chuo taaluma uliyosomea au kwenda kufanya kazi ya hio taaluma yako ?

Karibuni kwa michango.
 

qn of sheba

JF-Expert Member
Sep 13, 2011
3,230
1,250
Kwangu bora kufundisha chuo.. Unakuwa free kufanya kazi zako binafsi kama umefungua ofisi yako na pia kama unabiashara yako pia unakuwa na muda wa kuiendesha au miradi kadhaa.
 

island

JF-Expert Member
Nov 26, 2013
908
1,000
ungeweka kwanza taaluma yako nn ? Fanya kazi ya taaluma yako .. chuo mpaka uje uwe senior ni issue af utakuwa una deal na watoto wa chuo na mawazo yako yatakuwa hayo hayo .. mtaani au ofisini unakutana na wadau wakubwa wakubwa ambao ndo channel zenyewe za maisha
 

gx100 Msc

Member
May 14, 2014
90
0
Mfano mdogo tu ni huu...MTU mwenye degree ya uhasibu akienda kufanya Kazi ya uhasibu bila kua na CPA yeye uishia kulipwa 450-700. Ila MTU huyo huyo akiajiliwa kufundizha kama teaching assistant (T.A) utalipwa 1.5 kwa vyuo vya serikali wakati huo huo unamuda wakutosha kufanya mambo yako
 

qn of sheba

JF-Expert Member
Sep 13, 2011
3,230
1,250
Mfano mdogo tu ni huu...MTU mwenye degree ya uhasibu akienda kufanya Kazi ya uhasibu bila kua na CPA yeye uishia kulipwa 450-700. Ila MTU huyo huyo akiajiliwa kufundizha kama teaching assistant (T.A) utalipwa 1.5 kwa vyuo vya serikali wakati huo huo unamuda wakutosha kufanya mambo yako

Umeona eeh uhadhiri unalipa kama Tutorial unatoka na 1.5m je ukifika senior na bado una chance ya kufanya research na consulting zako binafsi.. Kutoa machapisho mbalimbali km uko mambo ya business kuandaa business plan za watu mbalimbali n.k
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom