Kipi bora kati ya kuwa na maendeleo ya nchi bila demokrasia au kuwa na demokrasia bila maendeleo ya nchi?

Quinn

JF-Expert Member
Oct 17, 2017
473
1,180
Nchi nyingi uonekana kukosa balance ya maendeleo na demokrasia kwenda pamoja na badala yake kimoja uzidi kingine yaan maendeleo yawe juu na demokrasia kuwa chini au demokrasia kuwa juu na maendeleo kuwa chini......nini wazo lako kuhusu hili?
 
Hayo maendeleo yaonekane basi. Unaona wanasiasa tu ndio wanajineemesha na kuneemesha kwao, sharti udai Demokrasi ili sauti yako uitoe
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Nchi nyingi uonekana kukosa balance ya maendeleo na demokrasia kwenda pamoja na badala yake kimoja uzidi kingine yaan maendeleo yawe juu na demokrasia kuwa chini au demokrasia kuwa juu na maendeleo kuwa chini......nini wazo lako kuhusu hili?
Maendeleo ni muhimu zaidi.
 
Nchi nyingi uonekana kukosa balance ya maendeleo na demokrasia kwenda pamoja na badala yake kimoja uzidi kingine yaan maendeleo yawe juu na demokrasia kuwa chini au demokrasia kuwa juu na maendeleo kuwa chini......nini wazo lako kuhusu hili?

Boss Quinn "Anayelazimishwa, hafurahii". Bora Demokrasia juu ya Maendeleo.
 
mmmh kweli baadhi ya watazania wana zero IQ ,sasa mkuu ndio umeandia nini,kwanza unatakiwa ujue nini maana ya demkrasia,demokrasia sio kwenye siasa tu,hata mwanao kuamua nini anataka kula nyumbani ni demokrasia,Maamuzi ya mkeo nini anataka avae wakati anatoka ni moja katika demkrasia...

Bila ya kuwa na uwazi wa kufanya mambo,bila ya kuwa na fikra na mawazo tafauti katika kuiendeleza nchi,nchi haiwezi kuendelea....

Demkrasia ni mfumo wa maisha unaotumiwa na nchi ili nchi iendelee na ipate maendeleo kutoka kwa wananchi wake,kila mwananchi ana haki ya kuchangia katika kuleta maendeleo ya nchi...

Uhuru wa kujiamulia,uhuru wa kupata habari,uhuru wa kuchangia,utawala unaoheshimu sheria...na mengi mengineo...hiyo ndio demokrasia...mkuu
 
Mfano DRC, yaani Democratic Republic of Congo-utawala wa kidemorasia ndo unawafanya waendelee kuteseka maana hakuna nchi nyingine duniani inayoweza kuwaamulia wajitawale vipi. Hadi atokee mwanamapinduzi wa ndani wa kuubadili upepo ndo mambo yatabadilika. Uganda hali kadhalika, kisa eti demokrasia. Shit..ole
 
Vyote vinatakiwa kwenda sambamba maendeleo pasipo demokrasia ni hatari kubwa chukulia mfano libya gadafi aliangamiza wanaharakati wengi waliokua wanapigania demokrasia kwa kisingizio wanarudisha maendeleo nyuma matokeo yake adui zake wakatumia mwanya huo kumuondoa na maendeleo ambayo gadafi aliyaleta yakaharibiwa yote saizi libya si chochote mbele ya dunia
Tuje kwa jirani yetu hapo ruanda je unadhani kagame ataongoza milele je unajua mrithi wake atakua na sera kama za kagame? Mara nyingi nchi ambazo hazina demokrasia zipo kwenye hatari ya kuingia kwenye machafuko wakati wowote kwa sababu maadui wengi wanatumia kigezo cha kuminywa kwa demokrasia kuchafua nchi na wanapewa suport na nchi za magaribi ambao ndio viranja wa demokrasia
 
Nchi nyingi uonekana kukosa balance ya maendeleo na demokrasia kwenda pamoja na badala yake kimoja uzidi kingine yaan maendeleo yawe juu na demokrasia kuwa chini au demokrasia kuwa juu na maendeleo kuwa chini......nini wazo lako kuhusu hili?
Huwezi tofautisha POLICCM na FISIEM
 
maendeleo mazuri ni yale yaliyotanguliwa na demokrasia, 90% ya waliotumbuliwa na JPM walikuwa wanamaendeleo yasiyo na demokrasia (namaanisha maendeleo yao yaliitangulia demokrasia) sasa piga picha kama nchi itakuwa na maendeleo alafu demokrasia ikawa nyuma mambo yatakuwaje!! tutashikana uchawi tu. maendeleo thabiti ni yale yanayotanguliwa na demokrasia na sio maendeleo kuitangulia demokrasia. Ahsante
 
Sababu ya binadamu kukubali kuanzisha dola ni ili aweze kumiliki mali bila kuhofia kunyang'anywa kwakua kabla ya dola kuwepo maisha yalikua yanaenda kwa mtindo wa mwenye nguvu mpishe.

Ikiwa tumeshaunda dola halafu demokrasia hakuna ni wangapi wanaweza kumiliki mali?

Ni wangapi wanaweza kumiliki mali na hawajipendekezi kwa watawala na hawahofii kunyang'anywa mali zao?

Naamini majibu yako yapo humo
 
Vyote vinatakiwa kwenda sambamba maendeleo pasipo demokrasia ni hatari kubwa chukulia mfano libya gadafi aliangamiza wanaharakati wengi waliokua wanapigania demokrasia kwa kisingizio wanarudisha maendeleo nyuma matokeo yake adui zake wakatumia mwanya huo kumuondoa na maendeleo ambayo gadafi aliyaleta yakaharibiwa yote saizi libya si chochote mbele ya dunia
Tuje kwa jirani yetu hapo ruanda je unadhani kagame ataongoza milele je unajua mrithi wake atakua na sera kama za kagame? Mara nyingi nchi ambazo hazina demokrasia zipo kwenye hatari ya kuingia kwenye machafuko wakati wowote kwa sababu maadui wengi wanatumia kigezo cha kuminywa kwa demokrasia kuchafua nchi na wanapewa suport na nchi za magaribi ambao ndio viranja wa demokrasia
Watu wa magharibi hawatoi silaha ila nchi zenye migogoro hupenda kununua silaha huko (business)
 
Nchi nyingi uonekana kukosa balance ya maendeleo na demokrasia kwenda pamoja na badala yake kimoja uzidi kingine yaan maendeleo yawe juu na demokrasia kuwa chini au demokrasia kuwa juu na maendeleo kuwa chini......nini wazo lako kuhusu hili?

Demokrasia inapunguza kasi ya maendeleo...
Demokrasia baadae.....
 
Back
Top Bottom