Kipenzi Changu Afrika. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kipenzi Changu Afrika.

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Gamba la Nyoka, Oct 29, 2007.

 1. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2007
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,600
  Likes Received: 6,767
  Trophy Points: 280
  Juu ya mataaluma chombo kimeshika mwendo kasi
  Kama Nyoka kwenye majani chateleza kwa kasi
  Ndanimwe kimeshiba watu walioketi kwa nafasi

  Nipo ndani naangaza katika madirisha ya tumbo lake
  Miti na milima yapita ikienda zake
  Nakumbuka nyumbani kwetu nilipotoka
  Natabasamu kwa raha nikikumbuka Afrika

  Mbeleko yako imembeba mwanadamu
  Kwa karne nyingi sana yafaa akuheshimu

  Umepambwa kwa rubi dhahabu na almasi
  Na mito itiririkayo polepole na iendayo kasi
  Ukarimu wa watoto wako ni mfano halisi
  Wa uzuri wako ewe kipenzi Afrika

  Umevumilia ngurumo na misukosuko mingi
  Maumivu, na machungu mengi
  Kwa upendo na huruma tele
  Huku chozi likikutoka ukasema yalopita si ndwele
  Ukatoa tabasamu la uchungu ukasema tuangalie ya mbele

  Afrika usilie watoto wako watarudi
  Watarudi nyumbani wakuletee zawadi
  Wamwagilie maua na miti yenye kunyauka
  Wakupambe uzidi
  kupendeza Afrika
   
Loading...