Kipengele cha "Zanzibar ni Nchi Ndani ya Katiba ya Zanzibar, 1984," So What? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kipengele cha "Zanzibar ni Nchi Ndani ya Katiba ya Zanzibar, 1984," So What?

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Buchanan, Aug 9, 2010.

 1. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #1
  Aug 9, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) inafanya marekebisho ya katiba ya mwaka 1984, ambayo yanaipa Zanzibar hadhi kamili kama nchi ndani ya Jamhuri ya Muungano.

  Marekebisho hayo ya katiba yanatarajiwa kuwasilishwa katika kikao cha Baraza la Wawakilishi kinachoanza leo Zanzibar, ambapo pia yataruhusu kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa baada ya uchaguzi wa Oktoba mwaka huu.

  Kwa mujibu wa rasimu ya marekebisho ya katiba hiyo, sura ya kwanza ibara ya kwanza iliyokuwa ikisomeka, Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imefutwa chini ya marekebisho hayo.

  Rasimu hiyo ambayo itawasilishwa na Mwanasheria Mkuu, Idd Pandu Hassan, inapendekeza kifungu hicho sasa kisomeke ‘Zanzibar ni nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na visiwa vidogo vilivyoizunguuka na bahari yake, ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar iliitwa Jamhuri ya watu wa Zanzibar’.

  Aidha, marekebisho hayo ya katiba yamegusa kifungu cha pili na kueleza kuwa Zanzibar ni miongoni mwa nchi mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


  Kwa habari zaidi Soma Tanzania Daima.

  WanaJF kwa kuweka kipengele hicho cha Zanzibar ni nchi ndani ya Jamhuri ya Muungano inaongeza nini hasa, maana naona Hati za Muungano zipo pale pale na ndio hasa zinazounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Au hii ni move inaelekea wapi hasa, maana CUF ambao ni anti-Muungano ndio hao wanaingia kwenye Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar!
   
 2. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #2
  Aug 11, 2010
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  it means...it is not long before we have a total separation!
   
 3. M

  Mchili JF-Expert Member

  #3
  Aug 11, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Itabidi tu kuwe na serikali tatu, maanake itakavyo kuwa wabara hawana serikali hasa kama Raisi wa Jamhuri atatokea Zanziber.
   
 4. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #4
  Aug 11, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Mabadiliko Katiba Z`bar yazua jambo

  Mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 yameelezewa kuwa yatatikisa Muungano wa Tanzania kwa kuwa yanagusa Katiba ya Jamhuri ya Muungano.
  Mabadiliko hayo ambayo yalipitishwa na Baraza la Wawakilishi juzi kwa wajumbe wote 75 waliokuwako wa CUF na CCM kuyakubali kwa kauli moja, yanaelezwa kuwa yataathiri Katiba ya Tanzania kwa kuwa inaitambua Zanzibar kama sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  Katika kikao hicho maalum katiba hiyo sasa inaongeza kifungu kinachoitambua Zanzibar kama nchi, ambayo eneo lake litakuwa ni eneo lote la visiwa vya Pemba na Unguja ambavyo kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar vilikuwa vikiitwa Jamhuri ya watu wa Zanzibar.
  Mabadiliko hayo yanasisitiza kwamba Zanzibar ni nchi mbili zilizounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  Kabla ya marekebishio hayo, Katiba ya Zanzibar ilikuwa ikiitambua kama sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, bila kutaja kuwa ni nchi ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  Mbali na marekebisho ya kuitambua Zanzibar kama nchi, pia yalilenga kuweka kipengele kitakachoruhusu uundwaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, mwaka huu.
  Mbadililiko hayo pia yamemuongezea mamlaka Rais wa Zanzibar ikiwamo kuteua wakuu wa mikoa bila kushauriana na Rais wa Jamhuri ya Muungano kama ilivyokuwa awali, kugawa mikoa na wilaya. Kutokana na mantiki ya mabadiliko hayo, baadhi ya wanasiasa wamesema marekebisho yanayoipa Zanzibar hadhi ya nchi kamili yanaweza kuuathiri Muungano.
  Wa kwanza kueleza hisia zake ni Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo, aliyesema yanaondoa misingi ya Muungano na kwamba yataleta mkanganyiko na kuwagawa zaidi Wanzanzibari na Watanganyika.
  Alisema mabadiliko hayo hasa msingi wa kuweka mipaka ya Zanzibar itaondoa ile dhana iliyopo kwenye Katiba ya Jamhuri kwamba Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  "Sielewi asili ya jambo hili na linakoelekea, mimi niseme tu kwamba sioni dhamira yoyote ya kuimarisha muungano ni confusion (mkanganyiko), nadhani tungetafuta vitu vinavyotuweka karibu zaidi badala ya kututenga kama inavyoonekana," alisema.
  Alisema utekelezaji wa maazimio hayo utaongeza ufa mwingine wa Muungano na kuongeza: "Mimi nilidhani kwa miaka yote hii ambayo tumekuwa kwenye Muungano tungekuwa na mawazo ya kuuimarisha zaidi badala ya kuchomeka vitu ambavyo vina nia ya kuubomoa."
  Cheyo alisema: "Nadhani ingekuwa vyema hawa watu wakaweka wazi mabadiliko haya na mjadala ukawahusu Watanzania wote kwa nia ya kubadilisha Katiba ya Jamhuri badala ya ilivyofanyika kujadili Katiba ya Zanzibar ambayo ni sehemu ya Jamhuri."
  "I am really confused (kwa kweli nimechanganywa) katika hii issue (suala) kwa sababu napenda zaidi tuungane kuliko kutengana," aliongeza Cheyo.
  Alionyesha wasiwasi wake wa namna Zanzibar itakavyotambulika kwa kueleza kwamba nje ya nchi itaonekana kwamba sio nchi, lakini ndani ya Jamhuri itakuwa nchi inayojitegemea.
  Mmoja wa viongozi wa juu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), aliliambia gazeti hili kwamba mabadiliko hayo yanatishia uhai wa Muungano wa Tanzania.
  "Kitu kinachonitisha ni pale Katiba ya Zanzibar inafanyiwa marekebisho bila kuhusisha Katiba ya Jamhuri," alisema.
  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Tanzania Labour (TLP), Augustine Marema, alisema kuwa alitarajia kuwa Baraza la Wawakilishi lingeshughulikia mambo ambayo yanataka kuzitenganisha Zanzibar na Tanzania Bara, lakini ameshangaa kuona yanafanyika maamuzi ambayo yana dalili za kutaka kuuvunja Muungano.
  "Zanzibar kusema ina mipaka ni kutaka iwe nchi inayojitegemea, hiyo ni mbaya na tutaishia pabaya," alisema Mrema kwa njia ya simu akiwa mkoani Kilimanjaro.
  Alisema maamuzi hayo yanakwenda kinyume cha malengo ya waasisi wa Muungano, Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere na Hayati Abeid Amani Karume. "Sijui ajenda ni nini hasa kwa sababu tulichokitarajia ni kuimarisha utaifa, mshikamano na mambo ya Muungano," alisema Mrema.
  Mrema alisema Zanzibar ikijitenga itapata hasara kuliko manufaa kwa sababu haina ardhi ya kutosha na kwamba Wazanzibari wengi hasa kutoka Pemba wanaishi na kufanya shughuli zao Tanzania Bara.
  Mwenyekiti huyo alisema anahisi kuwa ajenda hiyo ni ya watu wachache wanaotaka Zanzibar ijiondoe katika Muungano kwa maslahi yao binafsi.
  Suala la Zanzibar ni nchi au la liliibuka mwaka jana, baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kulieleza Bunge kuwa Zanzibar si nchi, kauli ambayo ilipingwa vikali na wanasiasa wa Zanzibar na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.
  Hata hivyo, Rais Jakaya Kikwete alitoa ufafanuzi alipolihutubia Bunge na kueleza kuwa Zanzibar ni nchi ndani ya Jamhuri ya Muungano kama ilivyo kwa Tanganyika isipokuwa sio nchi nje ya Tanzania.
  Katika hatua nyingine, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Katiba na Utawala), Ramadhani Abdallah Shaaban alisema neno Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) litaendelea kutumika licha ya kupitishwa muundo mpya wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
  Waziri huyo ambaye aliwasilisha muswada wa mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar, alisema hakuna haja ya jina la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kubadilishwa ili iitwe Serikali ya Mapinduzi ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar kama ilivyokuwa imependekezwa na baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.
  Waziri Shaban alisema hakuna ulazima wa jina hilo kubadilika kwa sababu hata Marekani haitumii neno Jamhuri na neno Mapinduzi litaendelea kutumika kwa misingi ya kulinda Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.
  Awali, wakichangia marekebisho hayo, Wawakilishi wa Gando Said Ali Mbarouk (CUF), wa Amani, Ali Denge Makame (CCM) na wa Kwahani (CCM), Ali Suleiman Ali, walipongeza hatua ya SMZ kwa kupendekeza marekebisho ya katiba yanayoipa hadhi Zanzibar kama nchi katika sura ya Muungano.
  Denge alisema Zanzibar ni nchi kwa kuwa ina mipaka na rais na hatua hiyo itasaidia kumaliza utata wa kisheria ambao umekuwa ukijitokeza na kuzua mijadala ya kisiasa nchini.
  Hata hivyo, Mbarouk alisema Zanzibar inapaswa kuitwa Jamhuri na kupendekeza jina la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar libadilishwe na badala yake liitwe Serikali ya Mapinduzi ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.
  Ali Suleiman Ali alisema anaunga mkono ibara ya kwanza ya katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kufuta maneno yaliyokuwa yakisomeka kuwa Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati Zanzibar ni nchi ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.


  Source: IPPMEDIA.
   
 5. K

  Kipimautu Member

  #5
  Aug 24, 2010
  Joined: Nov 23, 2007
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katiba ya Zanzibar ilifanyiwa mabadiliko baada ya kupigwa kura ya maoni na wananchi kura yenye maelekezo potofu kwa sababu zisizokuwa wazi kwa umma wa watanzania.
  Karatasi ya kura ya maoni ilikuwa na swali hili :
  "Je, Unakubali kuwepo kwa muundo mpya wa Serikali baada ya Uchaguzi Mkuu, 2010?"
  Swali hili ndilo lililopigiwa kura. ni swali ambalo ni kitendawili.
  UKWELI - ilikuwa ni kura ya maoni kuhusu serikali ya umoja wa kitaifa + mambo mengine.
  Wazanzibari waliingizwa chaka kama hawakufahamu walichokifanya au ikiwa walikuwa wanajua wanachokifanya basi waliwaingiza mkenge watanganyika na wengine wote nje ya ulingo wa unguja na pemba.
   
 6. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #6
  Aug 24, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Maalim Seif in action! This man is dangerous, believe it or not! Let's wait 'n see!
   
 7. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #7
  Aug 25, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  kwani hana blood connection na sultan aliyepinduliwa 1964?
   
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #8
  Aug 25, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,575
  Likes Received: 18,491
  Trophy Points: 280
  Wajemeni, kuelekea uchaguzi mkuu, mambo mengine tuyawachage tuu pembeni, JF tusije onekana tunataka kumfanyia Seif kile alichofanyiwa Salim na Mtanzania mwaka 2005.
  Ya chini chini yaliwahi sikika, wajuzi wa nasaba wanajua kila kitu, ila sio haki kumfananisha na Sulnani Jamsid eti tuu kwa vile wanafafana sharubu!.

  Nenda Seif nenda!, ikulu ya Zanzibar ni yako na njia nyeupee!.
   
 9. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #9
  Aug 25, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Huyu bwana Seif amekaa kigaidi gaidi!
   
 10. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #10
  Aug 25, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Kuna haja ya Tanganyika nayo kurudishwa na kutambuliwa kama nchi kamili ambayo ipo ndani ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.
   
 11. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #11
  Aug 25, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Nimeanzisha thread inayodai kwamba "Dkt Mvungi: Muungano Ulishavunjika!"
   
 12. KOKUTONA

  KOKUTONA JF-Expert Member

  #12
  Feb 1, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 8,344
  Likes Received: 391
  Trophy Points: 180
  Mimi nadhani kuna haja ya TANGANYIKA kuwa nchi pia, alafu kuwe na serikali tatu. ya Tanganyia, ya Zanzibar na ya muungano. Lakini swali langu ni kwamba, endapo huku bara ikashinda CHADEMA let say, then Zanzibar ikashida CCM then itakuwaje, serikali tatu itawezekana? Nisaidiane jamani
   
 13. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #13
  Feb 2, 2011
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Ni kweli kuwa Zanzibar ni nchi kwa kuwa hata katika historia, Zanzibar haikuacha sovereignty yake ilipoungana na Tanganyika, ndio maana serikali yake iliendelea kuwepo. Tanganyika ndiyo iliyoachia sovereignty yake na kuikabidhi kwa jamhuri mpya ya Tanzania. Kwa maana hiyo, ni makosa kusema kuwa Zanzibar ni miongoni mwa nchi mbili zinazounda muungano wa Tanzania, maana nchi ya pili haipo! Ili kipengele hiki kiwe kweli, inabidi ile nchi ya pili irejeshwe, jambo ambalo wengine wataona ni kuzidi kuvunja muungano. Lakini ni muungano wa ajabu sana huu unaomaanisha kuwa Tanzania ni yetu sote, lakini Zanzibar ni yao! Sioni faida ya huu muungano. Uvunjike tu, tutaendelea kushirikiana kama tunavyoshirikiana na jirani zetu wengine. Hauna maana.
   
 14. K

  Kisu changariba Member

  #14
  Feb 11, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nionavyo mimi Mchakato wa mabadiliko ya katiba ya Znz una sura ya uhaini ukiutazama kwa muktadha wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Unawezaje kukuiita kitendo cha kupora baadhi ya Madaraka ya Rais??
   
 15. p

  pat john JF-Expert Member

  #15
  Feb 25, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 245
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sababu za kuwa na muungano zimepitwa na wakati. Let the Zanzbaris go, we remain with our Tanganyika. Tunaweza kuwa na ushirikiano kama uliopo kati yetu na Burundi au Rwanda. Tumechoka kusikia habari zao za mimi Mzanzibari, sisi Wazanzibari. Let them have their country, we remain with our own. Wote Wapemba na Waunguja walio Bara warudi kwao au wawe treated as foreigners. Wabunge wote kutoka huko wakose ajira za bungeni wakagombee kwao.
   
 16. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #16
  Mar 6, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135

  Na wanyamwezi wote walioko visiwani warudi kwao wanawabana Wazanzibari.
   
 17. N

  Nonda JF-Expert Member

  #17
  Mar 6, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Wakuu.
  Tusipoacha kufanya usanii ambao Mwalimu na CCM wameufanya kwa muda mrefu basi tutaendelea kujifanya "vipofu".

  Tanganyika na Zanzibar hawakuungana kuwa nchi moja...Waliunganisha mambo 11 yaliyoitwa mambo ya Muungano.
  Kwa hiyo Tanganyika ilibakisha mambo mengi ambayo hayakuwa ya Muungano na Zanzibar vile vile walibakisha mambo mengi ambayo hayakuwa ya Muungano. Hii maana yake nini?

  Ni kuwa Serikali ya Tanganyika ilibaki na Taasisi zake kwa mambo ambayo si ya Muungano...Zanzibar ilibaki na Taasisi zake kwa mambo ambayo si ya Muungano na ikaja mamlaka mpya pia ya mambo ya Muungano.

  Ujanja wa Mwalimu na ubabe wake kama rais wa Tanganyika akaingiza Serikali ya Tanganyika ndani ya serikali ya Muungano.. akabadilisha jina la Muungano..kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kuwa Tanzania..baada ya hapo ikawa ni sera rasmi kuipoteza Tanganyika..lakini hadi hii leo tunapoandika haya kuna wizara ambazo si za mambo ya Muungano. Jee hizi sio wizara za Tanganyika?...au tunapendelea tuiite Tanzania bara, tumeliokota wapi jina hili? Limetoka wapi jina hili Tanzania bara? Nani aliifuta Tanganyika? Mbona upo mfumo wa sheria wa Tanganyika na wizara za mambo ya Tanganyika? Leo imekuwa fashion kusema Tanzania bara.. ni upotoshaji wa makusudi tunaoufanya.

  Buchanan wewe ni mtu wa sheria..Tanzania ina mamlaka ngapi kisheria? Moja? Mbili? au Tatu?

  EAC haijafuta nchi wanachama wake....au kuna muungano duniani uliozifuta ..ulioziua nchi ziliuunda Muungano huo? Ni kiini macho tu..mazingaombwe ya Mwalimu na CCM.
   
 18. N

  Nonda JF-Expert Member

  #18
  Mar 6, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu.
  Marekebisho/ mabadiliko ya Katiba ya Muungano ya kumuondoa Rais wa Zanzibar kuwa makamo wa Rais wa Muungano yalikuwa na sura gani?..Hawa wenzetu walilalamika sana na walisema kiungo cha Muungano kimeondolewa. Ukipitia hapa pengine unaweza kukubaliana na hoja yao.
  https://www.jamiiforums.com/katiba-mpya-tanzania/115516-zanzibaris-want-more-powers-for-vice-president.html

  Kama ni uhaini tulitangulia kuufanya. Ni sisi tuliouvunja Muungano kwa kujifanya wajanja.
   
Loading...