Kipengele cha 'kadhi' chapigwa 'x' ilani ya CCM! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kipengele cha 'kadhi' chapigwa 'x' ilani ya CCM!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MziziMkavu, Aug 17, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 17, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Serikali imetoa kauli ya kusitisha kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi nchini na sasa mfumo mpya wa sheria wa kukidhi haja ya jamii ya Waislamu, utaingizwa katika sheria za nchi katika mwaka huu wa fedha. Sambamba na hilo, imetangaza nia ya kubadilisha mfumo wa kujiunga na Taasisi ya Mafunzo ya Sheria kwa Vitendo (Law School), ambapo si wanafunzi wote waliomaliza shahada ya kwanza ya Sheria watakaoruhusiwa kujiunga nayo, huku ikiweka wazi idadi ya talaka zilizotolewa mwaka jana na mzigo wa kesi ‘unavyoiumiza’ Mahakama nchini.

  Kauli hiyo ya serikali ilitolewa bungeni jana na Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe, wakati alipowasilisha hotuba ya makadirio ya matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka huu wa fedha, yanayofikia Sh bilioni 107.6.


  Kwa mujibu wa Chikawe, badala ya kuanzisha Mahakama ya Kadhi katika mfumo wa mahakama nchini, sasa serikali itaingiza misingi ya dini ya Kiislamu katika mfumo wa sheria za nchi. Uamuzi huo umefikiwa baada ya kumalizika kwa utafiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria kuhusu uanzishwaji wa mahakama hiyo nchini au la.


  “Mapendekezo ya Tume ya Kurekebisha Sheria yamepokewa na kufanyiwa kazi na kamati ya wataalamu wa sheria iliyoundwa ambayo pia imetoa mapendekezo yake kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali,” alisema Chikawe.


  Alifafanua kuwa baada ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kupata mapendekezo ya kamati ya wataalamu, imeanzisha mchakato wa kukusanya maoni kutoka kwa viongozi wa madhehebu yote ya dini ya Kiislamu.


  “Nia ya mchakato wa kukusanya maoni hayo ni kupata orodha ya misingi ya dini ya Kiislamu hususan inayohusu sheria binafsi, kwa madhumuni ya kuihuisha misingi hiyo katika sheria za nchi yetu,” alisema Chikawe.


  Kwa mujibu wa utaratibu uliotolewa na Chikawe bungeni wa kuihuisha misingi hiyo ya dini ya Kiislamu katika sheria za nchi, viongozi wa dini wakishakubaliana kuhusu misingi hiyo, Waziri wa Sheria atatoa tamko litakalotokana na makubaliano ya viongozi hao. “Baada ya hatua hiyo, tamko hilo la Waziri litakuwa sheria itakayotambuliwa na mahakama zote nchini,” alisema Chikawe.


  Kwa uamuzi huo, Chikawe alisema haki zote binafsi za Waislamu zitalindwa na kusimamiwa na serikali na kutekelezwa na mahakama. Kuhusu uamuzi huo na misingi ya Katiba, Chikawe alisema utaratibu huo hautaathiri misingi ya Katiba ya nchi na kutoa mfano kwa Afrika Kusini ambayo ina waumini wengi wa Kiislamu na inatumia utaratibu huo.


  Kuhusu Taasisi ya Mafunzo ya Sheria kwa Vitendo, iliyo chini ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chikawe alisema mwaka huu wa fedha, wizara inakusudia kufanya mabadiliko katika sheria iliyoanzisha taasisi hiyo.


  Baada ya mabadiliko hayo, watakaolazimika kudahiliwa nayo watakuwa wahitimu wa Shahada ya Sheria wanaokusudia kuwa mawakili wa kujitegemea tu na si wahitimu wote wa Shahada ya Sheria.


  Aidha, Serikali imejipanga kuwajengea uwezo mawakili wa serikali, wahasibu, wachumi, wahandisi na watu wa kada mbalimbali katika majadiliano, uandaaji, uandishi na usimamizi wa mikataba.


  Akizungumzia uendeshaji wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Chikawe alisema wakala huyo ameendelea kuboresha huduma zake na kwa mwaka wa fedha uliopita, alisajili talaka 73, ndoa 15,345, vizazi 938,775, vifo 105,482 na watoto wa kuasili 39.


  Chikawe hakusita kuonesha mzigo wa kesi uliopo mahakamani ambapo katika Mahakama ya Rufaa, kati ya kesi 2,659 zilizokuwapo, ni kesi 560 tu zilizosikilizwa na kumalizika. Katika Mahakama Kuu, kati ya kesi 18,805 zilizokuwapo kesi 9,590 zilisikilizwa na kumalizwa.


  Katika mahakama za mikoa 23 na za wilaya 100, kulikuwa na kesi 61,237 na kati ya hizo kesi 42,725 tu ndizo zilizosikilizwa na kumalizika. Katika mahakama za mwanzo, kati ya kesi 213,239, ni 151,200 ndizo zilizosikilizwa na kutolewa uamuzi.


  Baada ya hotuba hiyo, Msemaji wa Kambi ya Upinzani, Mbunge wa Chakechake, Fatma Maghimbi (CUF), aliitaka Serikali itoe ufafanuzi wa kwa nini mahakama haijatengewa fungu la fedha kama ilivyo mihimili mingine ya Dola, ili kuongeza uhuru wa mhimili huo.


  Maghimbi alisema hata Rais Jakaya Kikwete katika mkutano wake na watendaji wa mahakama uliofanyika Bagamoyo, aliridhia kuwapo fungu hilo baada ya watendaji hao kumwasilishia ombi hilo rasmi.


  Hata hivyo, Spika Samuel Sitta, kabla ya kusomwa kwa hotuba za Chikawe na Maghimbi, alipokuwa akimkaribisha Jaji Mkuu Augustino Ramadhani bungeni, alisema bajeti ijayo, mahakama itatengewa fedha zake.


  Kuhusu Taasisi ya Mafunzo ya Sheria kwa Vitendo, Maghimbi alisema taasisi hiyo ina matatizo makubwa mawili, likiwemo la kukosa wafanyakazi wa kudumu. Lingine kwa mujibu wa Maghimbi ni wanafunzi kukosa mikopo ambapo kumekuwa na hali ya kutupiana mzigo kati ya Wizara ya Katiba na Sheria na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu.


  Chanzo: Gazeti la HabariLeo
   
 2. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #2
  Aug 17, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Serikali si taasisi ya deen moja, this is what Muhammadans failed to understand at the very first place, na kufikiria kuwa walikuwa na uwezo wa kuweka veto clause ili kuishinikiza Serikali kuweka chochote hao Muhammadans wanachotaka. La hasha, it is not so.

  The picture is now clear that, Muhammdans are not at par with GOV.
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Jun 25, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Katika hali ya kuonyesha mahangaiko, CCM wameamua kuondoa kipengele cha KADHI katika ilani yao ya uchaguzi 2010 baada ya kuona kinawazingua....

  Akitangaza hatua hiyo jana, Makamu mwenyekiti wa CCM Pius Msekwa alisema kwamba wamefikia hatua hiyo baada ya kupata ufafanuzi kutoka serikalini, kwenye Tume ya Kurekebisha Sheria (Law Reform Commission), ambapo walielekezwa kwamba serikali haiwezi kuunda chombo hicho cha KIDINI, na kwamba hilo ni jukumu la Waislamu!....

  Aidha alisema kwamba uamuzi huo tayari umeshafikishwa kwenye uongozi wa Waislamu, na kwamba wameshauriwa kufanya jambo hilo kwa misingi ya dini yao....Huku akionyesha kugwaya wakati akiongea na Waandishi wa habari jana, Makamu huyo Mwenyekiti wa CCM alisema kuwa Tume hiyo ya Kurekebisha Sheria (LRC) ina Mwenyekiti ambaye ni Mwislamu, na anaitwa Ibrahim, kwahiyo huo ni uamuzi sahihi tu!....

  Ndugu mwanajamvi, unaelezea vipi kugwaya huku?....Je tutegemee kiasi gani cha ahadi zitakazokuwa 'FEKI' katika uchaguzi wa mwaka huu?...Je kwanini DINI zitiwe vidole kwa manufaa ya kisiasa ya kundi la watu?...mawazo yenu!
   
 4. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #4
  Jun 25, 2010
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Walipokuwa wanaingiza mahakama ya kadhi kwenye ilani ya uchaguzi ya 2005 hawakuomba ushauri toka kwenye hiyo tume? Inaelekea hawa watu ni wakurupukaji tu. Jee ilani ya 2010 tuiamini vipi? kwa hiyo ccm iliwatapeli wapiga kura waliokipa kura kwa sababu ya mahakama ya kadhi uchaguzi wa 2005?
   
 5. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #5
  Jun 25, 2010
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Walipata walichokuwa wanakitaka kutoka kwa waislamu 2005. Sijui mwaka huu watawadanganya kwa kitu gani, maybe sharia banking! Wajinga ndio waliwao !
   
 6. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #6
  Jun 25, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,954
  Likes Received: 2,094
  Trophy Points: 280
  Kirefu cha CCM na kiwe Chama Cha Matapeli!
   
 7. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #7
  Jun 25, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Ishu ya Sharia Banking ni personal efforts za individual banks, and CCM dudes will be PIRATES if they snitch this!..huh!
   
 8. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #8
  Jun 25, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Hivi hata kama kama wasingepewa ushauri wa kundoa mambo ya mahakama ya kadhi ina maana kuna waislam ambao kigezo muhimu cha kutoa kura kwa CCM ni uwepo mahakama ya kadhi. Na je kuna wakristu kigezo muhimu cha kutoichagua CCM ni kuwepo kwa kipengele cha Mahakama hii ?

  Sidhani kama kuna jibu la ndio kwenye maswali haya mawili.

  Sasa kwenye hiyo ilani ya mwaka 2010 kuna critical national issue gani? Trekta kila kijiji?
   
 9. J

  Jafar JF-Expert Member

  #9
  Jun 25, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  CCM ni sawa na "Ze Komedi" - wametumia kipengee cha mahakama ya kadhi kupata kura za waislam na ndio maana jamaa akapata 80%. Walichotaka wamekipata hawana haja tena na kura zao. Kama kweli walikuwa-serious kwa nini wanakifuta sasa, je kweli inachukua mtu kutumia miaka 5 kujua kuwa serikali haiwezi kuunda mahakama ya kadhi. Hii wazungu wanasema "..good political timing strategy.." (wakati muafaka).

  Tusubiri albamu nyingine ya CCM maana hii ya "KK - Kilimo Kwanza inachuja kabla ya uchaguzi wenyewe.

  Tutasikia mengi.
   
 10. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #10
  Jun 25, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Wakuu naona hakuna kilichoharibika hapa! Mahakama ya Kadhi ni IBADA YA WAISLAMU, kwa hiyo IANZISHWE NA KUGHARAMIWA NA WAISLAMU WENYEWE! Sasa ugomvi uko wapi wajameni? Mnataka kuchafua ILANI YA UCHAGUZI YA CCM, 2010 kama ilivyochafuliwa ILANI YA UCHAGUZI YA CCM, 2005 kwa kuweka ISLAMIC AGENDA? Hongereni CCM kwa kutorudia makosa! Hata saa mbovu huwa inasema ukweli mara mbili ndani ya masaa 24!
   
 11. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #11
  Jun 25, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  ...Woow, this is too good to go uncommented for!..Nimeipenda mkuu!
   
 12. Aza

  Aza JF-Expert Member

  #12
  Jun 25, 2010
  Joined: Feb 23, 2010
  Messages: 1,672
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  na bungeni sasa uyo sijui naibu waziri ndio amelizungumzia hili la kadhi
  kwamaba waislamu tulishughulikie kama dini yetu tu serikali haiwezi kuliweka (serikali haina dini).
  ma-sheikh wanazuoni wetu wanachambua sasa ili likae vizuri kwa imani ya islam.
  good
   
 13. Aza

  Aza JF-Expert Member

  #13
  Jun 25, 2010
  Joined: Feb 23, 2010
  Messages: 1,672
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  malaria sugu ungejua hasa vatican ni nini hasa!!
  ni "nchi" ya wakatoliki so ina wawakilishi ktk nchi zingine
   
 14. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #14
  Jun 25, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Anzisha thread ya mada hiyo, japokuwa thread nyingi sana zimejaribu kuongelea na kuelezea kuhusu Vatican!...Dont polute this thread broda!
   
 15. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #15
  Jun 25, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Ulikuwa hujui kuwa ni wakurupukaji? the sad thing is bado utawapa kura yako.
   
 16. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #16
  Jun 25, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Hiyo ndiyo ccm, too Rhetorical in its dealings. Haifai kuongoza nchi.
   
 17. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #17
  Jun 25, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Malaria SUGU ulewa vatican ni nchi kama ilivyo nchi yo yote ile hapa duniani. Inaraisi wake, sarafu yake, na kila kitu kama tz. Ni bahati mbaya tu kuwa waislamu wengi mnaiona kivingine. Treats zote za kimataifa zinaitambua. wewe hata upige kelele unapoteza wakati. Ukitaka kujua kwa nini ubalozi wake upo nenda wizara ya mambo ya nje watakujulisha.
   
 18. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #18
  Jun 25, 2010
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Jibu lako liko wazi...NDIYO JAMAA AMETUINGIZA MJINI..kwa vile yeye kama yeye kipindi hiki ndicho chake cha mwisho hana wasiwasi na masuala ya kadhi wala kura zetu vilevile kama alivyopasha wafanyakazi wa KCC kwaa maana nyingine kama ni kura zetu basi amezikosa na hana shida nazo, lakini naamini matokeo ya baada ya uchaguzi suala la kadhi watalirudisha 2015 la sivyo patachimbika
   
 19. Mike-Austin

  Mike-Austin Member

  #19
  Jun 25, 2010
  Joined: Nov 20, 2008
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waislamu wanatakiwa kulishughulikia hilo katika imani yao na si ndani ya Serikali. Mbona madhehebu mengine ya Kikristo yana utaratibu wa kuwaandaa viongozi wao wa dini kupitia vyuo mbalimbali? Wameanzisha masomo ya dini katika vyuo hivyo na ndiko wanakopata maelekezo ya kusimamia taratibu zao za dini.

  Waislamu wana Chuo Kikuu cha Morogoro; kwa nini wasikitumie hicho kuwafundisha makadhi hiyo sheria ya Kiislamu (Islamic Law) ili wakifuzu warudi kusimamia taratibu hizo za mirathi, wakfu, talaka na matatizo ya migogoro misikitini. Kuna nini katika mawazo ya hawa waislamu kuhusu mahakama hii?

  Waafrika tumekuwa na mazoea ya kuishi pamoja na kushirikiana kwa mambo mengi. Shuleni watoto wetu wanasoma pamoja; kazini tunafanya kazi kwa pamoja; kwenye vyombo vya usafiri tunapanda bila kuchagua wa kukaa naye; kwenye mitaa yetu hatuchagui jirani wa kuishi naye. Katika mazingira yote hayo utatambua kuwa wanadamu wote ni sawa na mambo mengine yanatengenezwa tu na binadamu na kwa sehemu kubwa yanaundwa tu mambo ya nje ya ulimwengu huu. Imefikia wakati binadamu amekuwa akimbagua mwenzie kwa misingi ya udini, ukabila na rangi.

  Hizi dini zimewafanya baba na mwanae wawe maadui eti kwa vile baba anaamini tofauti na mwanawe; ndugu katika ukoo wanakasirikiana na kuvunja undugu kwa sababu ya dini hizi za Wazungu. Waafrika tulikuwa ndugu kabla ya ujio wa hizi dini lakini sasa tunaekea kubaya.
   
 20. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #20
  Jun 25, 2010
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Narejea nakunukuu hekima zake......

  4th August 2006

   
Loading...