Kipaumbele katika maisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kipaumbele katika maisha

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kisusi Mohammed, Oct 23, 2009.

 1. Kisusi Mohammed

  Kisusi Mohammed JF-Expert Member

  #1
  Oct 23, 2009
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 442
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Imekuwa ni kama kasumba kwa watu wengi waliofikia rika la kujitegemea kukosa uchaguzi sahihi wa kuyaendea maisha yao kwa usahihi endelevu utakao mjenga na kumuendeleza katika kuyakabili maisha yake ya kila siku.

  Wengi wamekuwa wanashindwa kuamua ni kipi haswaa ni cha kipaumbele katika mambo mengi ya msingi ya kufanya ili maisha yawe bora na yenye furaha.

  Kwa Mfano: Kuoa au kuolewa, kuwa na usafiri (gari, pikipiki, baiskeli), kujenga nyumba, kununua shamba, kununua kiwanja, kuwekeza katika hisa, kusafiri nje ya nchi katika kutafuta kipato cha ziada au kufanya lolote lenye muelekeo wa kimaendeleo.

  Hivyo basi kwa mtazamo wa haraka haraka nikiwa kama mmoja wa waliopata tabu sana katika kuamua kipaumbele, nikaonelea haitakuwa vibaya faida hii nikaifikisha mikononi mwa wanaJF ili kila mwenye wazo lake na atupe alichonacho ili kesho na keshokutwa kwa watakaopata mawazo haya mazuri wayatumie na wasiishie kuapata tabu kama mimi.

  Swali la msingi: NI KIPI CHA KUKIPA KIPAUMBELE KATIKA HAYO MENGI NILIYOYATAJA HAPO JUU?

  Natumai nimeeleweka.
   
 2. F

  Franki Member

  #2
  Oct 23, 2009
  Joined: Oct 16, 2009
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umeme
   
 3. Kisusi Mohammed

  Kisusi Mohammed JF-Expert Member

  #3
  Oct 23, 2009
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 442
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Hahahahaaaa kaka Franki umeme ni nyongeza tu, na hauleti maendeleo bali unarudisha maendeleo nyuma "MGAO"!
   
 4. m

  mgiriki Member

  #4
  Oct 23, 2009
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  mimi nadhani bila nyumba nzuri ya kukaa mwanadam hujawa na maisha mazuri. gari badae na vingine vingi ila nyumba ni muhim iwe kijini au mjini
   
 5. K

  Kifimbocheza JF-Expert Member

  #5
  Oct 23, 2009
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 496
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Hi inategema na mtu na mtu.

  Kuna watu kipaumbele chao ni Kuoa kwanza wengine kununua gari na wengine mpka wanunue Shamba. Kwa hiyo kujibu swali lako ni kwamba Kilamtu ana kitu ambacho anakipa kipaumbela zaidi ya kingine.

  Wewe unaweza ukawa unapenda sana ujenge nyumba yako kabla ya kuoa na mtu wengine mambo ya kujenga nyumba wala hayapo sana kwenye akili yake
   
 6. Triplets

  Triplets JF-Expert Member

  #6
  Oct 23, 2009
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 1,103
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Nionavyo mimi:
  1 kuwa na hisa au shughuli yoyote ya kuongeza kipato
  2 kiwanja
  3 kujenga nyumba
  4 usafiri
  kuoa/kuolewa kunaingia popote baada ya namba moja
   
 7. Nyuki

  Nyuki JF-Expert Member

  #7
  Oct 23, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  NAMUUNGA MKONO Triplets
   
 8. Joste

  Joste Senior Member

  #8
  Oct 23, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  The best is what will make you as effective and efficient as possible....Ukianza na gari nadhani utakuwa faster zaidi kufikia malengo yako. After all...ukiwa na 8,000,000 unaweza kupata gari litakalokusaidia mambo yako, the same haiwezi kujenga nyumba. Next ni Mke mwenye kipato na serious.....ukimpata mke serious na akiwa na income mtajenga nyumba nzuri na kubwa kihalali kabisa. Mimi nilifanya hivyo; TOYOTA COROLLA, WIFE and finally HOUSE. I have two houses na sijawahi kupitisha vocha ya mtu wala kutoa na kupokea rushwa kama kina nanihii
   
 9. Kisusi Mohammed

  Kisusi Mohammed JF-Expert Member

  #9
  Oct 24, 2009
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 442
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Kwa kweli nazidi kuelimika na kufaidika kila baada ya mchango wa mdau. Hii itawasaidia wale wote ambao bado wana maswali juu ya kipi kitangulie kabla ya kingine. Ahsanteni sana na bado nataraji mawazo zaidi ili iwe faida kwetu na wengineo wote.
   
 10. Safina

  Safina JF-Expert Member

  #10
  Oct 24, 2009
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 498
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Frank umepinda
   
 11. G

  Greyson Nyamoga Member

  #11
  Oct 24, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kisusi, hongera kwa kuibua haka kamada kazuri na muhimu kwa wengi mimi nikiwemo. Naomba kumuunga mkono Joste kwa asilimia 70.

  Kwa mtazamo wangu Kipaumbele katika Maisha kitategemea na mipangilio ya mtu mwenyewe.Wakati mwingine angependa atangulie kuoa mwingine anafikiria gari kwanza na mwingine angedhani nyumba kwanza. Familia zetu ni extra extended, mara unapopata kakibarua unafuatwa na msululu wa wategemezi nyuma yako, wapo watakao hitaji ada ya shule, mtaji, matibabu na mengine yanayofanana na hayo.Hivyo wakati unaweka Vipaumbele vyako huwezi kuyaweka hayo niliyoyataja kando hata kidogo. Ili Upeo au elimu uliyoipata iweze kutricle down into your family/community lazima uwasaidie hao ili nao angalau wapate macho ya kuona maili kadhaa mbele yao, vinginevyo utakuwa na gari halafu wakwenu hata asprin hawawezi kununua itakuwa haina maana sana.

  Biblia inasema asiyejali wa kwao ni sawa mtenda maovu mwingine yeyote yule.

  Best regards.
   
 12. Kisusi Mohammed

  Kisusi Mohammed JF-Expert Member

  #12
  Oct 25, 2009
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 442
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Ahsante sana kaka Grey, pamoja na utashi wa mtu binafsi nilitegemea nawe utoe orodha yako kulingana na kipaumbele kwa maisha yako ya extra extended family na hali halisi ya familia zetu. Kwa sababu wengi wetu tupo kwenye status kama hiyo, ukitusaidia kuorodhesha priorities waweza tusaidia kufunguka kimawazo.
   
Loading...