Kipaumbele cha elimu serikali ya Magufuli ni kipi?

darcity

JF-Expert Member
Jul 20, 2009
8,589
16,615
Bado sijaelewa mwenendo wa elimu na vipaumbele vyake kwa sasa. Kipindi cha JK msisitizo ulikuwa katika masomo ya sayansi ili kupata wataaluma na wataalamu katika tasnia ya sayansi. Hivi sasa sijajua hawa watendaji wa JPM vipaumbele ni nini, nahisi kama ''wanabutua'' vipaumbele vyote vya nyuma, kama vile kuwapata walimu wa kutosha wa masomo ya sayansi kwani wanafunzi wa UDOM waliokuwa wanasoma stashahada ya ualimu katika masomo ya sayansi wameitwa vilaza na wamerudishwa nyumbani, kisa? form four hawana sifa ya kujiunga na chuo na kusoma diploma kabla ya kusoma cheti.
(hiyo kozi inasomwa miaka mitatu ambayo logically ni sawa na mtu anayesoma cheti mwaka mmoja na kisha akasoma diploma katika miaka miwili) na wengi wao ni vijana waliopata daraja la kwanza hadi la tatu na kupata credit katika michepuo ya sayansi. Bado katika selection ya form six waliomaliza shule mwaka huu wanafunzi waliofaulu vizuri michepuo ya sayansi (CBG,PCM,PCB,EGM nk) wamechaguliwa kwenda kusoma masomo ya sanaa. Mbaya huko mashuleni hasa shule za kata wallimu wa kujitolea/muda (temporary teachers) ambao wengi wao walikuwa ni vijana waliomaliza kidato cha sita hivi sasa hawana nafasi kutokana na sera ya elimu bure.Kundi hili lilikuwa linasaidia sana kuwasaidia wanafunzi katika masomo ya sayansi na biashara kutokana na uhaba wa walimu wa masomo hayo.Walimu wakuu wa shule wengi wanaogopa kuwaajiri kutokana na uhaba wa fedha kwani fedha zinazoletwa zina maelekezo ya matumizi na hakuna fungu la kuwalipa walimu wa kujitolea,unless kama wazazi wakakaa kikao na uongozi wa shule wakakubali kumlipa mwalimu wa muda,kitu ambacho kutokana na nidhamu ya woga iliyopo hivi sasa hakuna hata mkuu wa shule anayetaka kufanya hivyo.Je ni kweli tuanataka kuboresha ubora wa elimu bila msaada wa wananchi ilhali wanafunzi wakiumia? (may be to get political attention) na kama ndio hivyo mkakati wa taifa kutatua tatizo hili ni upi? au bado tupo katika ombwe la kila kiongozi kufanya maamuzi kwa mtazamo wake anayohisi kwamba yanafaa kwa taifa bila kuangalia ubora (faida) na hasara zake kwa taifa (personal judgement). Moja ya maamuzi hayo mabaya kabisa mfano wake ni kama ule wa Mungai aliyeondoa masomo ya biashara na michezo mashuleni. Napita tu...nenda zangu.
 
umesema kweli, ila naogopa kutoa hisia zangu hapa kwa sabab ya ufinyu wa uhur wa kujieleza.
 
umesema kweli, ila naogopa kutoa hisia zangu hapa kwa sabab ya ufinyu wa uhur wa kujieleza.
 
Naskia sasahivi wafanyakaz wa umma hamna kwenda masomoni ukienda mshahara hupew kwa sababu haupo kazini
 
Naskia sasahivi wafanyakaz wa umma hamna kwenda masomoni ukienda mshahara hupew kwa sababu haupo kazini
na inasemekana ukitaka kuomba ruhusa ya kwenda kujiendeleza kielimu uandike barua ya kuomba likizo bila malipo na hapo ukumbuke hupewi mkopo
 
na inasemekana ukitaka kuomba ruhusa ya kwenda kujiendeleza kielimu uandike barua ya kuomba likizo bila malipo na hapo ukumbuke hupewi mkopo
Sasa sjui watajiendelezaje maana mkopo hawapewi mshahara hawapewi sasa hawa watumishi watasomaje gharama za kujisomesha watazitoa wapi?naona hapa serikali hii insure haijaichunguza kiumakini lengo ni kuwauwa watumishi wa umma washindwe kujiendeleza .Ila dawa yao watumishi wa umma ukitaka kwenda kusoma chukua mkopo mrefu benk mana hakuna namna.halaf cha kushangaa viongoz wao wenyewe walipitia mfumo wa awali wa kujiendeleza kwaio kwakua wao walishatoka ngoja wawaumize wenzao .
 
Sasa sjui watajiendelezaje maana mkopo hawapewi mshahara hawapewi sasa hawa watumishi watasomaje gharama za kujisomesha watazitoa wapi?naona hapa serikali hii insure haijaichunguza kiumakini lengo ni kuwauwa watumishi wa umma washindwe kujiendeleza .Ila dawa yao watumishi wa umma ukitaka kwenda kusoma chukua mkopo mrefu benk mana hakuna namna.halaf cha kushangaa viongoz wao wenyewe walipitia mfumo wa awali wa kujiendeleza kwaio kwakua wao walishatoka ngoja wawaumize wenzao .
Yaan sijui nia yao kwakwel hawa viongoz nahisi huwa wanakurupuka na haya maamuzi yao,tanzania ya viwanda tutaisikia kwenye bomba
 
Wataalamu Wa Kikoloni Walisema "UKITAKA KUMTAWALA MTI, BASI MNYIME ELIMU"
Hatari Ya Kumtawala Mtu Halafu Ukampa Elimu Ndiyo inayojitokeza Leo Hapa Nchini, Chama Cha Kijani Kina Hofu Ya Kuwaacha Vijana Wapate Elimu Wakaja Wakajitokeza Maelfu Ya Tundu Lissu Hapo Baadae.

Kwani Tundu Lissu Mmoja Tu Huyu Aliyepo Angelinyimwa Elimu Hapo Awali, Basi Asingiliwapa tabu Kama Hizi Anazowapa Sasa.

Je Leo Iwapo Vijana 100,000 Watakamilisha "Masters Digree" Zao unafikiria Chama Kijani cha Elimi ya Mwendo Kasi Kitakuwa Katika Hali gani??

Kutokana Na Hilo, Serikali Ya Mr Self decision Anaangamiza Elimu Kwa Makusudi ili vijana wote wawe na Mawazo ya Kama wale wa Lumumba Kwa Pretex mbali mbali ambazo hata hazitiliki Akilini.

Wewe Angalia tu Vijana 7000 waliotimuliwa UDOM wanajenga Picha gani iwapo Wangegraduate Na Kusambazwa Mashuleni???
Ni Wazi Kuwa Chama Cha Kijani Kinauwa elimu Kwa Kusudi ikiwa ni mmoja ya Mkakati wao Kuandaa Vijana Wajinga iwatawale.

Angalia Mfano huu wa Wajinga Wanavyokuwa:-
Inapotokezea Mkurugenzi wa taasisi Fulani Ya Serikali Kukamatwa Kwa Ufisadi Wa Mabillions huku Akihusishwa Kupokea Mishahara Hewa 17, Basi Wajinga Hufurahi Na Kummwagia Sifa Mr Magu Na Kuanza Kuwabeza Wapinzani!!
Lakini Kutokana na Ujinga Wao Wanashindwa Kujiuliza Je Baada Ya Kukamatwa Kwake Kimeendelea Nini??
Mbona Bado Yupo Kitaa, Anamiliki Private Schools Zake Kama Kawaida, Hana Mashtaka Aliyofunhuliwa, Hakuna Kilichotaifishwa, Hakuna Uchunguzi Halali Unaofanywa Juu Yake! bali ni Sifa Na Promo za Kidikteta tu.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom