darcity
JF-Expert Member
- Jul 20, 2009
- 8,718
- 16,932
Bado sijaelewa mwenendo wa elimu na vipaumbele vyake kwa sasa. Kipindi cha JK msisitizo ulikuwa katika masomo ya sayansi ili kupata wataaluma na wataalamu katika tasnia ya sayansi. Hivi sasa sijajua hawa watendaji wa JPM vipaumbele ni nini, nahisi kama ''wanabutua'' vipaumbele vyote vya nyuma, kama vile kuwapata walimu wa kutosha wa masomo ya sayansi kwani wanafunzi wa UDOM waliokuwa wanasoma stashahada ya ualimu katika masomo ya sayansi wameitwa vilaza na wamerudishwa nyumbani, kisa? form four hawana sifa ya kujiunga na chuo na kusoma diploma kabla ya kusoma cheti.
(hiyo kozi inasomwa miaka mitatu ambayo logically ni sawa na mtu anayesoma cheti mwaka mmoja na kisha akasoma diploma katika miaka miwili) na wengi wao ni vijana waliopata daraja la kwanza hadi la tatu na kupata credit katika michepuo ya sayansi. Bado katika selection ya form six waliomaliza shule mwaka huu wanafunzi waliofaulu vizuri michepuo ya sayansi (CBG,PCM,PCB,EGM nk) wamechaguliwa kwenda kusoma masomo ya sanaa. Mbaya huko mashuleni hasa shule za kata wallimu wa kujitolea/muda (temporary teachers) ambao wengi wao walikuwa ni vijana waliomaliza kidato cha sita hivi sasa hawana nafasi kutokana na sera ya elimu bure.Kundi hili lilikuwa linasaidia sana kuwasaidia wanafunzi katika masomo ya sayansi na biashara kutokana na uhaba wa walimu wa masomo hayo.Walimu wakuu wa shule wengi wanaogopa kuwaajiri kutokana na uhaba wa fedha kwani fedha zinazoletwa zina maelekezo ya matumizi na hakuna fungu la kuwalipa walimu wa kujitolea,unless kama wazazi wakakaa kikao na uongozi wa shule wakakubali kumlipa mwalimu wa muda,kitu ambacho kutokana na nidhamu ya woga iliyopo hivi sasa hakuna hata mkuu wa shule anayetaka kufanya hivyo.Je ni kweli tuanataka kuboresha ubora wa elimu bila msaada wa wananchi ilhali wanafunzi wakiumia? (may be to get political attention) na kama ndio hivyo mkakati wa taifa kutatua tatizo hili ni upi? au bado tupo katika ombwe la kila kiongozi kufanya maamuzi kwa mtazamo wake anayohisi kwamba yanafaa kwa taifa bila kuangalia ubora (faida) na hasara zake kwa taifa (personal judgement). Moja ya maamuzi hayo mabaya kabisa mfano wake ni kama ule wa Mungai aliyeondoa masomo ya biashara na michezo mashuleni. Napita tu...nenda zangu.