Kipato cha milioni moja kwa mwezi life style gani ya kuishi na kipi kifanyike uweze kufika mbele zaidi kiuchumi ushauri

mzeewangese

JF-Expert Member
Feb 11, 2016
639
500
Habari za jioni Wadau, Wakubwa shikamooni.

Natumaini nipo jukwaa sahihi kabisa kama nimekosea naomba iamishwe jukwaa. Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu. Natumaini kuna watu waliopita kwenye stage hiyo wakafika mbali zaidi.

Kwa kipato cha milioni moja kwa mwezi unawezaje kujipanga ukiwa kama famili yenye members wanne baba mama na watoto. Kuanzia bei ya nyumba ya kupanga. Aina za watoto shule kusoma.

Kipi kifanyike au life style gani itakuwa appropriate kwa kipato hiko. Natumaini kupata ushauri positive kwa ajili ya kusonga mbele zaidi.
  • Makazi Dar es Salaam
  • Watoto age:1years Mwengine 4years
  • Note 1:Wife income haipo kwenye consideration.
  • Note 2: Mishindo pembeni ya 1milioni ipo inatokea kwa kutegemea na upepo wa mwezi but fixed ni 1milion per month.
Nawakilisha Asante.
 

FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
5,180
2,000
Binafsi kwa kipato hicho..

Nyumba napanga karibu na kazini kama wahindi

Chakula tunakula cha kawaida kama familia nyingi zinavyokula nyumbani.. wastani ni elfu 10 kwa siku.. kwa mwez laki 3.

Watoto elimu ya msingi wanasoma shule za goverment .. ila walimu wa masomo muhimu hesabu, na english na science nawaekea bajet ya posho ya tution kwa mwezi wastani elfu 10 kila mwalimu.

Laki moja bajet ya dharura..

Na laki mbili ni bajet ya maendeleo ya familia kama ujenzi ama biashara ndogo ndogo.

Ukijichanganya tu ukamsikiliza mwanamke watoto ukapeleka shule za kina junior na caren utateseka sana na ujenz utafeli.. unless mwanamke nae awe anachangia pato la familia kila mwezi kuijazia hiyo milioni yako ya baba
 

Consultant

JF-Expert Member
Jun 15, 2008
10,921
2,000
50%: Essential needs (chakula, nyumba, usafiri), 30%: wants/luxury and 20%: savings for potential investments
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom