Kipato cha haraka kwa watanzania wote. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kipato cha haraka kwa watanzania wote.

Discussion in 'Matangazo madogo' started by Mama, Nov 25, 2010.

 1. M

  Mama JF-Expert Member

  #1
  Nov 25, 2010
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  MLETE MTEJA KATIKA KAMPUNI YETU YA USHAURI NA UENDELEZAJI WA BIASHARA NA UTALIPWA ASILIMIA ISHIRINI (20%) YA KIASI ATAKACHOLIPA MTEJA HUYO KULINGANA NA AINA YA HUDUMA

  ANAGALIA KUHUSU SISI NA AINA YA HUDUMA TUNAZOTOA HAPA CHINI
  Kuhusu sisi:
  EVAG Consulting Firm (T) Ltd ni kampuni inayojihusisha na utoaji wa huduma ya ushauri na msaada wa kuendeleza biashara na huduma mbalimbali za wafanyabiashara,mashirika ya uma,Makampuni Binafsi,yasiyo ya kiserikali n.k.Kampuni hii imesajiliwa chini ya sheria ya makampuni ya umma ya mwaka 2002 Lengo la kampuni hii kwa ujumla ni kusaidia uanzishwaji,uendelezaji na ukuaji wa wafanyabiashara wadogo wa kati na wakubwa kufikia kiwango cha juu cha ufanisi wa malengo yao.

  Huduma zitolewazo:
  • Kuandaa vitabu vya mahesabu ya biashara na masuala yote ya kiuhasibu:Tunaandaa vitabu vya biashara za aina zote yaani kwa watu binafsi,Mashirika yasiyo ya kiserikali(NGO’s),mashirika ya umma na mahesabu ya makampuni binafsi.Vilevile tunatoa ushauri wa aina ya vitabu vya kutunza kumbukumbu na programu nzuri za kompyuta za uhasibu kulingana na mahitaji ya kazi zako.
  • Uchunguzi wa masoko,Uchunguzi wa uwezekano wa masoko na Utafiti wa masoko:Tunazifanya kazi hizi kwa umakini mkubwaili kutambua aina ya wateja,na kile wanachokihitaji sana katika bidhaa na huduma zako,ukubwa wa soko,kiasi cha ukuaji wa soko,faida inayoweza kupatikana,garama za kuingia sokoni,njia za usambazaji wa bidhaa,mwelekeo wa soko na mbinu za kipekee za mafanikio.

  • Semina,mafunzo na makongamano mbalimbali ya kijasiriamali:Hizi zinakuwa juu ya masula mbalimbali ya kijasiriamali kama kujenga uwezo na mitazamo,uongozi wa biashara,jinsi ya kuendesha biashara,vyanzo vya mapato,uvumbuzi wa mawazo mapya n.k.
  • Kuandaa michanganuo ya biashara:Hii ni nyaraka muhimu sana katika biashara yoyote kwani hutoa dira katika kuweka mipango ya biashara,sababu za kwamba inatekelezeka,mbinu za jinsi ya kufanikisha mipango hiyo,na hutumika hata kuombea mikopo katika taasisi za fedha n.k.
  • Kuandaa Mapendekezo ya miradi na tathmini zake:Tunaandaa na kusanifu nyaraka hizi kwa wateja wetu waweze kutoa mipango ya utendaji wa mawazo yao,kutoa sababu kwamba kwanini kuchukua hatua,uwezekano wa mradi na kumshawishi msomaji kukubaliana na wazo na kuidhinisha mipango ilyowekwa na mwenye pendekezo la mradi
  • Kupitia upya mwenendo wa biashara:Hapa tunarejea nakupitia upya mfumo na mwenendo wa biashara na huduma yako na kubuni michakato mipya ya kuirejesha biashara inayolegalega ili kuiletea biashara yako mafanikio tena
  • Kuhesabu mali:Hapa tunafanya uchunguzi,kuhesabu na kukadiria thamani ya bidhaa zilizopo stoo,na kukadiria upya thamani ya bidhaa hizo kulingana na mwenendo wa soko katika maeneo mabalimbali mfano katika maghala,bohari za serikali na binafsi, maduka n.k.
  • Kubuni na Kuandaa maelezo mafupi ya kampuni (Taswira): Tunafanya kazi hii kulingana na mfumo/aina ya biashara, bidhaa na huduma zako ili kuendana na mfumo wa soko.
  • Masuala ya kodi na yote yanayohusiana nayo.

  Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi:
  EVAG Consulting Firm (T) ltd
  Jengo la kitengo cha Ujasiriamali cha chuo kikuu cha Dar es Salaam,
  Kampasi ya Mlimani,
  Mkabala na Mgahawa wa “Hill Park”
  Chumba namba 202B
  Simu: +255 0769852820/+255 0712194828 /+255 0655 570700
  Barua pepe: evagconsultants@ymail.com

   
 2. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #2
  Nov 25, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 0
  Hongera mama. Lakn unaonaje mkitoa Punguzo la 20% kwa mteja atayekuja kwenu, mlivofanya naona imekaa "kiudalali" zaidi!
  Ni wazo tu!
   
 3. M

  Mama JF-Expert Member

  #3
  Nov 25, 2010
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Sio udalali, wazo lako ni zuri ila atakujaje bila kuletwa/Kufahamishwa.Tunahitaji watu wengi zaidi wafahamu ubora wa huduma zetu
   
 4. M

  Maamuma JF-Expert Member

  #4
  Nov 25, 2010
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 856
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Mama, Hongera sana. Je, mna mpango wowote wa kuwa na matawi mikoani? Unaonaje mkiwa na "wakala" ambaye anaweza kuwa kama kiungo kati yenu na watu wa mikoani. Kwa maana ya kwamba anatafuta wateja na wakipatikana wa kutosha mnaenda kupiga darasa. Mnaweza kupata wateja wengi kwa mpigo. Ni mchango wangu wa mawazo.
   
 5. M

  Mama JF-Expert Member

  #5
  Nov 26, 2010
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Asante sana kwa maoni yako mazuri.
  Hiyo ni nzuri sana na tunawatafuta watu kama hao na watakaoweza kuratibu na kutafuta watu katika sehemu mbalimbali za Tanzania.Kama upo tayari kuwa wakala tunaweza kuwasiliana .
   
 6. M

  Mama JF-Expert Member

  #6
  Dec 3, 2010
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Thanks your suggestions
   
 7. c

  cronique Member

  #7
  Dec 3, 2010
  Joined: Jan 25, 2009
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mama,
  Nilikuwa na idea kidogo kama hiyo lakini tofauti, angalia kwenye forum ya business and economics. Kuna thread nimeandika inaitwa Procurement group. Ukiona interesting, please tuwasiliane tuongee vizuri. E-mail yangu ni cronique@msn.com
   
Loading...