Katuni za Masoud Kipanya (Special thread)

1570512756209.jpeg
 
Kuna siri kali ktk zao la Korosho. Kwa sisi watu wa kusini ndo tunajua hali inaviendelea. Kwa wasiojua ni hivi.

1. Mpaka leo maghala hayajafunguliwa ili kukusanya korosho mpya. Hii ni kwa sababu korosho za mwaka jana bado zipo maghalani

2. Korosho zinaenda Vietnam. Bei iliyoafikiwa kati ya serikali na wanunuzi haijulijani.

3. Kuna idadi kubwa ya korosho zimekataliwa (rejected) kwa maana ni mbovu. Swali ni je zitaenda wapi?

4. Wakulima mpaka leo hawajalipwa pesa zao

5. Kutokana na mkutaniko wa korosho za mwaka jana na mwaka huu maana yake ni kuna supply kubwa ya korosho which means demand itakuwa ndogo jambo ambalo litapelekea kushuka kwa bei ya korosho msimu huu

6. Msimu uliopita serikali iliwakaba koo wanunuzi wa korosho kwa mfumo usio rasmi yaani kangomba. Lkn sasa kangomba inaendelea na Serikali ipo kimya maana kangomba leo ndo anaonekana mkombozi wa mkulima.

7. Mpaka leo serikali haijaweka wazi bei elekezi ya korosho.
Kwa kifupi serikali imefyata kwanza korosho yenyewe, wafanyabiashara na wakulima ndo mana inakimbizwa kila leo. Karibuni Mtwara
 
Shukrani.

Na je kile kiwanda cha kubangua korosho kimeshajengwa kama ilivyoagizwa?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom