Kipanya: Katika manunuzi ya ndege

Wakishanunua tunaotwa kuipokea na kukata viuno kutwa nzima kumbe kuna kama kawaida imepitishwa kwao
 
Manunuzi yetu hufanywa kienyeji
Hapo tatizo ni manunuzi ya ndege kwa bei nafuu bila kufuata taratibu za manunuzi ya umma ama ni rushwa katika manunuzi?

Maana hicho kikaragosi kinaonesha nia ovu peke yake katika manunuzi hayo, hakijaonesha tija ya jambo hilo, ina maana kinalaani.

Mkuu, ya ngoswe mwachie mwenyewe.

Hayo yote unayoyaona kama marumbano kwenye ishu ya manunuzi, ni vurugu za fisi kugombania mzoga.

Hivi katika manunuzi ya nyumbani kwako, ninavyoelewa kabla ya maamuzi ya manunuzi, lazima uzunguke kwanza madukani uelewe bei iliyo nafuu mf; unataka suti aina flani mtaa wa kongo inauzwaje, maduka mengine nje ya Kariakoo wanauzaje, je kwenye duka la jirani yako anayekopesha, anaweka cha juu kiasi gani, baadaye unaamua kununua mtaa wa kongo kwa laki3, suti ileile inayouzwa na jirani yako lai5 kwa mkopo.

Itashangaza kama jirani yako atakulaumu kwenda kununua 'keshi' suti ya aina hiyo Kariakoo na kumkwepa yeye anayekopesha na riba zake!

Sasa suti imekwishakununuliwa, ninayo tayari, nitalaumiwaje kwa kuamua kufuata unafuu na kukwepa madeni?

Mifumo ya manunuzi ya kiserikali ukiifanyia 'shotikati' lazima tu kelele hazitokosa kwa sababu wanufaikaji wengi katika upigaji unakuwa umewanyima ulaji.
 
Acha kutuona wajinga,mfumo wa manunuzi umewekwa ili kuepuka usiri,lazima upitie taratibu zote halali unapotaka kununua au kuuza,ndivyo sheria inavyotaka,kufanya jambo lolote bila kufuata sheria jambo hilo linakuwa haramu,na siku zote haramu haileti halali
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom