Atclkwanza
JF-Expert Member
- Dec 20, 2015
- 823
- 998
Kibaya gani wewe Kipanya kafanya?Hivi kwanini mnapenda kuwatisha watanzania kuitumia Rwanda kama kivuli chenu ili watu wasitoe maoni yao.Kipawa ukitumia vibaya inakuwa sio kipawa tena bali laana,tafakari,Kipanya anatumia kipawa chake kueneza chuki,kumbuka hata Rwanda walioeneza chuki ni watu waliotumia vipaji vyao kama Kipanya,Kipanya akitaka siasa ajiunge tu na siasa na si kutumia kivuli cha uchoraji wa vikaragosi,nani asiyejua kuwa Kipanya ni kikaragosi cha Chadema?kumbuka pakichimbika hata hivyo vikaragosi vyake hakuna atakyekuwa na muda wa kuvisoma.Je ina maana unapotoa msaada kwa jirani wewe jamaa zako hawana shida?
Njoo nikwaambie kitu mauaji ya kimbari yalisababiswa Na serikali kwa kukandamiza jamii nyingine hasa ya kitusi,
Na kagame alikuwa mpinzani wa serikali(RPA),Ni sawa na ACT ingawa kagame alitumia kuipinga serikali kwa kuvamia Rwanda kutumia jeshi hasa kutokana na mazingira magumu ya kufanya siasa yaliowekwa na serikali ya Habriamana,Na ndicho tunakiona hapa kwetu hii miaka ya karibuni,Nadhani wote ni mashuda jinsi ulivyo mswada wa vyama vya siasa.
Huwa nafurahi sana mnavyotolea mfano Rwanda kwa kujua au kutokujua kwamba tukimchukulia kagame alikuwa mpinzani akitaka udhalimu,ukandamizaji uliokuwa umeshamiri chini ya utawala wa kihutu ukomeshwe,
Kwa hiyo mnavyowatisha watanzania kwa kutumia Rwanda ni upuuzi,Wale intaharamwe kile ni kikundi kilichokuwa kinaratibiwa na serikali kuendesha mauji,
Je mnavyotumia mfano wa Rwanda kwa hiyo mnawambia wapinzani wa serikali wasiikosoe serikali,kwasababu serikali inaweza kusababisha mauji kama ya Rwanda kama walivyofanya intarahamwe chini ya chama tawala(MRND) hapa kwetu sawa na CCM.
Na chombo cha habari ambacho kilikuwa kinatoa hate speech ni cha serikali na chama tawala k
ilikuwa kinaitwa RTLM sawa na Radio UHURU ya CCM.
Kwa muktadha huu serikali inataka watu wakiikosoa iwafyeke wapinzani wake kama ilivyofanya serikali ya Habriamana na interahamwe.
Halafu nadhani we mchangiaji hujui hata Mauji ya kimbari ya Rwanda chanzo nini acha kukariri kwa sababu Rais katolea mfano,nina uhakika hata mhehimiwa Rais hajui chanzo chake.
Tufike kipindi tuache kuwatisha watanzania ukiminya Uhuru wa watu watautafuta kwa nguvu kama alivyofanya kagame usiku mwema.
Vinara wa mauaji ya kimbari
I) Robert kajuga huyu alikuwa Rais wa intarahamwe.
ii)Jean kambanda-waziri mkuu kwenye serikali ya mpito baada ya kifo cha Habriamana
iii)Augustine Bizimungu) huyu alimbadili Gatsinzi kuwa chief of staff kutokana kuwa extrimist.
iv)Justin Mgenzi
V)Mathieu Ngirumpatse-Aliyekuwa Rais wa chama tawala MRND
Vi)Ephrem Nkezabera -kiongozi wa kamati ya kuratibu mauaji wa intaharamwe
Vii)Andre ntegerura mlezi wa MRND
Viii)Theonest Bagosora huyu alikuwa na misimamo mikali kwa wahutu alikuwa waziri wa ulinzi nyakati za mwisho wa utawala wa MRND.
Wote hao walikuwa ni kutoka ndani ya serikali ya MRND siyo upinzani RPF.