Kipande cha barabara cha mita 200 Tabata Kimanga chatumia miaka 10 kuwekwa lami

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
36,018
40,686
Tangu mwaka 2009 mkandarasi yupo site na anafanya kazi usiku na mchana, anafunga barabara na kupitisha magari kwenye diversion.

Kila siku vijiko na magreda naviona vinafanya kazi pale, vifusi na kokoto vinamwagwa kila kukicha, ila kipande hicho cha mita 200 huko Tabata Kimanga hakijafanikiwa kuwekwa lami.

Na huyu mkandarasi yupo hapo site tangu 2009, na tunamuona akifanya kazi kila siku. Hata leo hii mkienda pale mtamuona yuko site na vifaa vyake, ila barabara haikamiliki.

Nasikia kuna kaburi la bibi mmoja pale lilihamishwa bila kufuata mila, ndio maana lami imegoma kuwekwa.

Kwa wajuzi wa hicho kipande cha barabara hiyo Tabata Kimanga, tunaomba maelezo, ni muujiza gani unafanyika hapo?
================================
Update:29/08/2020
Hatimae jana wameanza kuweka lami, baada ya kusota kwa miaka 10, JF kiboko
 
Wakati ninahamia maeneo hayo mwaka 2011, walifanikiwa kuweka lami ambayo haikudumu miaka 2-3, ikabomoka. Baadae wakadai hili eneo lina maji chini, hivyo ujenzi mpya wakaanza kuweka mawe chini. Leo wanamwaga kifusi, wanarudi baada ya miezi 3 kumwaga kingine. Sasa toka miaka hiyo ya 2013+ hadi leo ni mauzauza tu.
 
Mkuu hawapo site huwa wanakuja na kupotea sasa hivi ni mwezi hawajawahi kurudi shida pale nadhani ni siasa maana viongozi waliokuwepo ni upinzani labda sasa hivi itajengwa baada ya kilichotokea maana haingii akilini kipande kidogo vile kijengwe zaidi ya miaka hiyo wakati barabara ya segerea hata likitokea shimo tayari utakuta wanaziba
 
Wewe ndio umeongea, hapo ni siasa tu, eneo hilo ni la upinzani so hutakaa uone maendeleo mpaka mwisho wa dahari.
Haya masuala tuliyaongea sana kwenye vijiwe vyetu huku. Kata ipo kwa upinzani, sasa tumeonja joto ya jiwe. Kwingine huko lami inawekwa, huku kama tupo periphery.
 
Suala t.kimanga ni upinzani kwa tabata kimanga imejinasibisha zaidi kwa levels za juu kipinzani na chadema ndio wanamiliki kata, ambapo diwani amekataa katakata kufika bei
 
Tangu mwaka 2009 mkandarasi yupo site na anafanya kazi usiku na mchana, anafunga barabara na kupitisha magari kwenye diversion.

Kila siku vijiko na magreda naviona vinafanya kazi pale, vifusi na kokoto vinamwagwa kila kukicha, ila kipande hicho cha mita 200 huko Tabata Kimanga hakijafanikiwa kuwekwa lami.

Na huyu mkandarasi yupo hapo site tangu 2009, na tunamuona akifanya kazi kila siku. Hata leo hii mkienda pale mtamuona yuko site na vifaa vyake, ila barabara haikamiliki.

Nasikia kuna kaburi la bibi mmoja pale lilihamishwa bila kufuata mila, ndio maana lami imegoma kuwekwa.

Kwa wajuzi wa hicho kipande cha barabara hiyo Tabata Kimanga, tunaomba maelezo, ni muujiza gani unafanyika hapo?
================================
Update: Nimeambiwa mkandarasi ni Del Monte, na nasikia baada ya uzi huu kwenda hewani, kuna kikao cha dharura kimeitishwa usiku usiku na kinaendelea hadi asubuhi hii
......kutoka hapa Kona ni pabaya kabisa
 
Back
Top Bottom