Kipaji changu kimepotea

KimpaGhasha

JF-Expert Member
Jun 21, 2020
327
448
Habarini humu ndani

Moja kwa moja kwenye mada

Aisee Watanzania na Waafrika kiujumla hatuna desturi yakuwafuatilia watoto wetu ili kuona Mungu amewabariki na kitu gani cha kipekee ambacho kinafaa kumuendeleza kwa manufaa yake na jamii kwa ujumla.

Leo nasikitika nikikumbuka kipaji changu kilichopotea haki yanani jamani

Wazazi wabaki kung'ang'ana nakasumba ya fanya hivi ili uwe kama mtoto wa fulani mbayaaa saana hii kwakweli

Nakumbuka wakati nikiwa mdogo kama wamiaka 11-15 nilikuwa mtunzi mzuri wa mashairi yaani nilikuwa na uwezo wakuongea na mtu kwa vina na mizani kabisa hata kwa maongezi ya kawaida.

Nakumbuka kwenye mtihani wa mwisho necta si wakaingia mkenge eti tunga shairi lenye beti 4 lenye vina na mizani sijui walisema 16 maana nishasahau saivi

Aaah alafu lina marks nyingi nikasema hili nafanya ziķiwa zimebaki dk 5 tu aisee nilifanya dk chache alafu limesimama vibaya yaani alokuwa anasaisha hilo shairi nahisi aliganda kwa mda akiangalia kipaji cha mtu.

Ila sasa asalaleeee kipaji kimepotea masikini!!

Siwezi chochote kwa kwelii!
 
Uku kwetu kwa na desturi tulizonazo mzazi kuivest kwenye talent ya mwanae badala la elimu ni ngumu. Hawana imani na mambo ya sanaa, wanahisi nikupoteza muda na kufikili kuwa mambo ya sanaa mengi yahusiana na uhuni.
 
Kuna baadhi ya vipaji kwa nchi yetu hua haviwezi kukupa mkate wa kila siku, sarakasi, ngumi, uigizaji, huo utunzi n.k. labda baadaye baadaye hivi
 
Uku kwetu kwa na desturi tulizonazo mzazi kuivest kwenye talent ya mwanae badala la elimu ni ngumu. Hawana imani na mambo ya sanaa, wanahisi nikupoteza muda na kufikili kuwa mambo ya sanaa mengi yahusiana na uhuni.
Wewe unasemaje maoni yako! labda utuambie pia kati ya vijana 10 wanaohangaika na nashairi wangapi wamefanikiwa kimaisha
 
Kama ni kipaji toka kwa Mungu hakipotei, simama kwa imani na anza kujipa mazoezi mdogo mdogo utajikuta mambo yamerudi kua sawa. Labda kama na wewe kwa sasa umekua na mambo mengi.
 
Kipaji huwa hakipotei ndugu
Acha bhana mi mwenyewe nakuambia kimepotea alafu unabisha

Kama hakina muendelezo kinayeyuka kiongozi.

Yaana saivi mpaka nijiumeume ndo ukute naweza ila haliwi konki kama enzi zangu
 
nilitegemea bandiko hili uandike kwa vina na mizani kuthibitisha hilo ila imekuwa tofauti ama ndo kipaji huna tena.

kipaji huwa hakipotea bali kinafifia tu ila chembechembe zake zipo tu
Kweli nakuambia, kimepotea kipaji.

Utotoni nakiwazia, nilikuwa mwimbaji.

Hakiyamungu nilifikia, kilele chautungaji.

Wengi walisifia, leo wamekuwa watetaji.

Umeona kazi hiyooo
 
Basi hakikua kipaji. Kipaji huwa hakipotei kwa asilimia zote.
Kweli nakuambia, kimepotea kipaji
Utotoni nakiwazia, nilikuwa mwimbaji
Hakiyamungu nilifikia, kilele chautungaji
Wengi walisifia, leo wamekuwa watetaji


MUNDENDE,

amini bhanaa
 
Nimekuambia kimepotea siwez kitu kiongoz ila enzi zile ningeshusha madini mpaka ungeniPM mwenyewe
Tatizo umekubali kimepotea, lakini mimi naamini hakijapotea,
Jaribu kufanya alichokwambia mkuu

Binafsi nina kipaji cha uchoraji, miaka ya 1990 nilikua nina uwezo wa kuchora mtu kwa kutumia kalamu ya wino bila kukosea, na vivuli naweka kwa kutumia kalamu ya wino,
Ila sa hv siwezi lakini ukinipa kalamu nichore naweza japo sio kwa asilimia zote kama kipindi hicho
 
Unawafahamu washairi wangapi kwa sasa wanaopata rizki zao za kila siku kupitia ushairi?

Wakati huo ulipokuwa mdogo, wazazi wako walikuwa wakifahamu wangapi waliokuwa wakijipatia rizk kwa ushairi?

Pana marefu, mapana, kina na muda wazazi huzingatia katika kumshauri mtoto achague fani ipi.
 
Back
Top Bottom