Kipa mzungu aipukutisha zaidi klabu ya Yanga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kipa mzungu aipukutisha zaidi klabu ya Yanga

Discussion in 'Sports' started by MziziMkavu, Mar 25, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 25, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  [​IMG] Kipa namba moja wa timu ya Yanga Obren Curkovic ambaye ameondoka Jangwani kuelekea Afrika kusini tayari kwa majaribio
  Clara Alphonce
  WIKI mbili kabla ya mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baina ya watani wa jadi, Simba na Yanga, klabu hiyo ya Mtaa wa Twiga na Jangwani imeondokewa na kipa wake namba moja, Obren Curkovic aliyekwenda kwa majaribio nchini Afrika Kusini.

  Timu hizo zinachuana Aprili 11 katika mechi ya marudiano ya Ligi Kuu huku Simba wakiwa wameshajitangazia ubingwa mapema.

  Kipa huyo Mzungu ameondoka siku chache baada ya mshambuliaji Jerry Tegete aliyekwenda Sweden kwa majaribio ya wiki mbili.

  Obren ambaye amemaliza mkataba wake na klabu hiyo ameondoka jana kwenda Afrika Kusini huku viongozi wa klabu hiyo wakiwa hawajui timu gani aliyokwenda kufanya majaribio.

  Ofisa habari wa Yanga, Louis Sendeu alisema jana kuwa mchezaji huyo ameondoka , lakini hawajui ni timu gani aliyoenda kufanya majaribio hayo na siku za majaribio.

  ''Ni kweli kaondoka tangu juzi, lakini hatujui ni timu anayoenda kuchezea kwa kuwa safari ilikuwa ya ghafla, ila alisema akifika huko atutumia jina la timu na siku ambazo atakuwa katika majaribio hayo,'' alisema Sendeu.

  Hii ni mara ya pili kwa kipa huyo kuondoka kwenda kwenye majaribio huku uongozi wake ukiwa haujui ni timu gani anayoenda kusaka tiketi ya kuchezea.

  Mara ya kwanza ilitokea msimu uliopita wakati alipoondoka nchini kurudi nchini baada ya kutofanikiwa.

  Wakati ule kama sasa, hakukuwa na taarifa zozote kama kafuzu majaribio au la.

  Wachezaji wengine wa klabu hiyo waliokwenda nje ya makaribio ni chipukizi Ally Msigwa na Razak Khalfan ambao inasemekana wamekwenda Marekani.

  Kipa huyo aliichezea Yanga kwa misimu miwili na kudaka mechi za watani wa jadi. Mzungu huyo amekuwa kipenzi cha mashabiki wa klabu zote mbili, Yanga na Simba kutokana na umahiri wake.

  Kutokana na kuondoka kwa Mzungu huyo, Yanga imebakiwa na makipa Nelson Kimath na Steven Malashi, ambao si wazoefu baada ya Yaw Berko, raia wa Ghana kumaliza mkataba wake wa miezi mitatu tangu mwezi jana na hivyo kutokuwa na kibali cha kucheza soka nchini.
  http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=18720
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Mar 25, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,334
  Likes Received: 22,185
  Trophy Points: 280
  Muda wa kumsajili juma shamte umewadia
   
Loading...