Kipa Ivo Mapunda, Kocha Micho, wang'ara Ligi ya Ethiopia

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,720
21,778
Kipa Ivo Mapunda, Kocha Micho, wang'ara Ligi ya Ethiopia
Na Vicky Kimaro

KIPA wa zamani wa Yanga, Ivo Mapunda na kocha wake Mserbia Sredojevich Milutin 'Micho' wameiongoza St. George kutwaa ubingwa wa ligi ya Ethiopia mapema.

St. George imetangaza ubingwa ikiwa na mechi mbili mkononi chini ya kocha wa zamani wa timu ya Yanga, Micho.

Hadi mwishoni mwa wiki Ivo alikuwa amefungwa mabao saba na hajapaoteza mchezo hata mmoja, hivyo Shirikisho la Soka la Ethiopia huenda likamtangaza kuwa kipa bora.

Micho aliiambia Mwananchi jana kuwa pamoja na nchi hiyo kuingia kwenye matatizo ya kufungiwa na Shirikisho la Soka duniani (Fifa), ligi ya Ethiopia imemalizika vizuri bila matatizo.
 
Hongera sana IVO....jiandae kustaafu soka vizuri maana umri nao.....
 
Hongera kwake ivo anaturusha huko pembe ya afrika, kaza moyo na urudi kusaidia nchi, pengo lako linaonekana, nafkiri bado atacheza kwa muda mrefu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom