Kiongozi yupi wa upinzani ni msafi na hakuwahi kunyooshewa kidole?

binjo

JF-Expert Member
Feb 22, 2016
2,115
1,240
Habari za majukumu mlionayo kwenu nyote na poleni.

Naja kwenu kufahamu ama nimjue ni kiongozi yupi wa Upinzani ambaye ni msafi hakuwahi nyooshewa kidole cha uchafu katika chama chake kwa ubadhirifu wa mali, uongo,usaliti ,udikteta, unafiki wala ukanda ama udini.

Nahitaji nianze leo kumpigia kampeni za chinichini mpaka ifikapo 2019 asilimia flani ya jamii naamini itakuwa imemuelewa na kumkubali na kuwa tayari kumpigia kura.

Ni hayo asanteni.
 
Habari za majukumu mlionayo kwenu nyote na poleni.

Naja kwenu kufahamu ama nimjue ni kiongozi yupi wa Upinzani ambaye ni msafi hakuwahi nyooshewa kidole cha uchafu katika chama chake kwa ubadhirifu wa mali,uongo,usaliti,udikteta,unafiki wala ukanda ama udini.

Nahitaji nianze leo kumpigia kampeni za chinichini mpaka ifikapo 2019 asilimia flani ya jamii naamini itakuwa imemuelewa na kumkubali na kuwa tayari kumpigia kura.

Ni hayo asanteni.
Hashjim Rungwe na Fahmi Dovutwa!
 
Labda mh.rungwe na mh.dovutwa mh.mnyika si alinyooshewa kidole katika ishu ya chacha wangwe au walimsakizia tu!
 
Dovutwa na Rungwe sijawah sikia chochote kiwahusucho.

Lakini Mbunge wangu Mh.Mnyika aliwahi nyooshewa kuhusu sakata lile.
Magufuli alipokuwa Waziri wa ujenzi alituhumiwa kuongoza Wizara iliyotumia zaidi ya bilioni 600 kiholela na kuuza kireja reja bila mpangilio wala hoja muwala nyumba za serikali, lakini leo hii ndiyo rais wetu!!
 
Kwa hiyo mkuu unaniambia kuongozwa na mtu ambaye alishanyooshewa kidole chochote kibaya si tatizo?

Hakuna msafi ccm tunajua sasa nani msafi tujiandae kumpigia kampeni za chinichin maana za juu virungu tutafaid.

Hayo unayozungumza ni marudio ya kila siku sasa tuanze na nani msafi ili atuondolee huyu mchafu MKUU.
 
Huyu jamaa atakuwa anamsema mh. Cheyo yaani mzee wa mapesa, huyo ndiyo mpigie debe, ukawa usijaribu kabisa kuwapigia kampeni kwa sababu wanajitambua na wanauwezo wa kuwafikia wananchi
 
Huyu jamaa atakuwa anamsema mh. Cheyo yaani mzee wa mapesa, huyo ndiyo mpigie debe, ukawa usijaribu kabisa kuwapigia kampeni kwa sababu wanajitambua na wanauwezo wa kuwafikia wananchi
Mkuu hoja ni nani msafi kama Ukawa yupo mtaje tu.

Kwani naamini hakuna mtu yeyote ambaye atanikataza kumpigia kura mtu msafi kutoka chama chochote.
 
Mkuu binjo, kunyooshewa kidole kunachafua mtu?! Akitokea hapa jamaa anayeitwa Njobi akakunyoshea kidole na kukutuhumu kwa uongo kuwa wewe ni mchawi, utakuwa wewe ni mchawi kweli kwa sababu umenyoshewa kidole?!
Kunyoshewa kidole haitoshi kumfanya mtu awe mchafu. Kwa mfano baba Je-seeker ananyooshewa vidole kuwa haheshimu katiba wala sheria, na kwa maneno ya kinywa chake(polisi waibe matairi ya magari wanayokamata wakayauze au trafiki kuchukua elfu tano ni kwa ajili ya kubrashi viatu, nk) yanadhihirisha kuwa anacholalamikiwa ni kweli anakifanya.
 
Back
Top Bottom