Kiongozi wangu, simba wangu ndugu Hussein Juma Ruhava

Oct 1, 2016
6
20
Jina kamili la Simba huyu anaitwa Ndug. HUSSEIN JUMA RUHAVA.
Cheo cha Simba huyu ni Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Kigoma-Ujiji, aliyepatikana baada ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015 na kuwa diwani wa kata ya BANGWE kupitia chama cha ACT WAZALENDO. Meya huyu ni wa kwanza katika historia ya chama cha ACT-Wazalendo na halmashauri anayoongoza ndiyo ya kwanza na pekee kuongozwa na chama hiki.

Malengo makubwa ya Simba huyu ni kuifanya Halmashauri ya Kigoma Ujiji kuwa mfano wa kuigwa na halmashauri nyingine zote hapa nchini. Na katika miaka mitano ijayo Kigoma iweze kuonekana kuwa inahama kutoka kwenye Manispaa na kuwa Jiji.

Umahili wake wa kufanya kazi kwa weredi ndani ya halmashauli ya Kigoma ujiji kunapelekea halmashauli hiyo kupiga hatua kwa kasi sana ukilinganisha na halimashauli zingine hapa nchini.

9/12/2016 (Ijumaa) Simba huyu anayeiongoza manispaa ya Kigoma-Ujiji alikutana na Meya na Governor wa Miji 15 Pasis Ufaransa ukumbi wa City Hall kusaini azimio la utekelizwaji wa ahadi zao. Kwa upande wa ACT wazalendo, Simba huyu alisaini ahadi 5 ambazo ni :-
1. AFYA
2. ELIMU
3. MAJI
4. ARDHI
5. BAJETI
Ambazo utekelezwaji wake ni kwa kipindi cha 2016/2017 – 2017/2018.
Ikumbukwe manispaa ya Kigoma – Ujiji ni moja ya Miji 15 duniani iliochaguliwa kujiunga na mpango wa utekelezaji wa serikali kwa uwazi (OPEN GOVERNMENT PARTNERSHIP) OGP.

Kwa sasa manispaa inayoongozwa na Simba huyu inasomesha wanafunzi wa kidato cha 5 na 6 BUREEE. Na hivyo hupelekea wanafunzi kusoma bure kwaanzia la darasa la kwanza hadi kidato cha sita

Simba huyu alishawahi kuwa Naibu Spika wa Bunge la Wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala (KIU), alijizolea umaarufu mkubwa sana pale chuoni mpaka wanafunzi wa chuo hicho wakampachika jina la Zitto Kabwe kutokana na aina ya siasa za masuala, Siasa za hoja na Siasa za aridhiano alizokuwa anazifanya pale chuoni. Hiyo ilikuwa kwenye mwaka 2012.

Kwa muda mrefu Simba huyu amesha wahi kufanya kazi na chama cha msalaba mwekundu Tanzania ilikuwa ni mradi wa (TOGETHER WE CAN) ukilenga kupunguza maambukizi kwa vijana HIV/AIDS Prevention2005-2010 na Mradi wa Damu Salama 2012-2015.

FAHAMU MAMBO MENGINE YANAYO MUHUSU SIMBA HUYU
Simba huyu ndie alikataa kutumia gari alilotakiwa kupewa kwa hadhi yako ya umeya lenye thamani ya shilingi milioni 150. Kwani Mara baada ya kuchaguliwa kwake kuwa Meya wa Halmashauri ya Kigoma-Ujiji, wenzake katika Baraza la Madiwani walipitisha bajeti ya gari la Meya wao. Gari lenyewe ni aina ya Prado lenye thamani ya dola 70,000 (takribani shilingi milioni 150).

Simba huyu alisema hivi nanukuu “Naheshimu wote mliopendekeza kwamba ninafaa kununuliwa gari. Hata hivyo, halmashauri yetu ina changamoto nyingi sana. Kigoma ni mojawapo ya mikoa masikini zaidi hapa nchini. Tazama, Tanzania ni mojawapo ya nchi masikini zaidi duniani. Halafu Kigoma ni mkoa masikini katika nchi masikini zaidi. Kununua gari la shilingi milioni 150 katika hali yetu ya sasa si suala jema sana. Kwahiyo niwaombe hizo milioni 150 tuzipeleke katika mambo yanayoumiza watu wetu. Kwenye maeneo ya afya, elimu na miundombinu.” Mwisho wa kunukuu. (HUYU NDIO SIMBA WANGU).
Asanteni

SEMA CHOCHOTE JUU YA HUSSEIN JUMA RUHAVA (SIMBAA) ALAFU SHARE POST HII
ACT WAZALENDO (SIMBA)
TAIFA KWANZA LEO NA KESHO
#CHAMA_LA_WANAAA.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom