Kiongozi wako ana madaraka kukiko yaliyoandikwa

Aventus

JF-Expert Member
Mar 8, 2013
1,914
1,977
"kiongozi wako wa kazi anayo mamlaka na madaraka makubwa kuliko yaliyoandikwa, sio kila jambo lazima iwe kanuni" — Job Ndugai, Spika wa bunge

Hii ni kauli ya Spika la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai wakati akifanya mahojiano na kituo cha cha Azam TV.., Mkutano wa 8 wa bunge la 11 umemalizika mjini Dodoma juma hili, huku moja kati ya mambo yaliyotanda kutoka katika mkutano huo ni "TABIA YA UKALI" kutoka kwa spika huyo anaetokana na CCM dhidi ya wabunge wa upinzani..,

Kabla sijaizungumzia kauli yake akiwa Azam Tv.., hii tabia yake ya ukali ina faida gani kwenye mahusiano ya kibunge na pia heshima ya chombo hicho!? Mhimili mmojawapo kati ya mihimili mitatu ya dola..., huyu Spika wakati wa mfungo wa mwezi mtukufu wa RAMADHAN, aliwahi kulalamika wabunge wa upinzani kususia iftari aliyokuwa ameandaa.., leo amesahau!? Hajui chanzo ni kitu gani hadi watu kususia futari!?

Anyways, tuachane na hilo, labda NDUGAI hajui kwamba wanadamu wanamiliki nyongo na wanamiliki nyoyo zenye nyama.., hivyo kuna nyakati wana wa ADAMU wanachoka na wanaamua kufanya ambayo wanafikiri ni sahihi kutuliza munkari wao.., anapaswa kutambua kwamba "sio wakati wote madaraka yanapaswa kuongozwa na nguvu.., busara na hekima na uvumilivu ni nyenzo kuu ya kuongoza taasisi yoyote ile"

Kauli yake kwamba anayo madaraka na mamlaka makubwa kuliko yaliyoandikwa..,

...., hii ni kauli mbovu sana kutolewa na kiongozi mkubwa ambae anaongoza chombo chenye mamlaka ya kutunga sheria za nchi yetu.., kwamba Ndugai hajui umuhimu wa mipaka ya taasisi ambayo anaiongoza!? Hajui na kutambua uwepo wa kanuni ambazo zinaongoza bunge!? Kwamba Ndugai hatambui kwamba taasisi pasipo na kanuni ni genge la walowezi tu!? Kwamba Ndugai hatambui..., kwamba Ndugai anataka kutuaminisha kwamba kuna kanuni zingine hazijaandikwa lakini yeye anazitumia kwa mamlaka yake!? Zipo kwenye bunch ipi!?

Kwamba una mamlaka kuliko pengine yaliyoandikwa katika kanuni za kudumu za bunge? Kuna maana ipi haswaa bunge kuwa na kanuni za kudumu ikiwa Spika wa bunge ana mamlaka makubwa kuliko yaliyoandikwa kwenye kanuni hizo!? Vipi viongozi wa mihimili mingine (Rais na Jaji mkuu) pia wakisema wanayo mamlaka makubwa kuliko yaliyoandikwa!? Vipi hawa viongozi wa taasisi zingine za umma (IGP, CDF etc) nao wakisema hivyo!? Nani atabaki salama!? Taifa lipi hilo ambalo viongozi wake wanayo mamlaka zaidi ya yaliyoandikwa!?

Spika ajifunze kumiliki hasira na jazba zake, mara zote ajifunze kuwa na subira.., ajipe muda wa kutafakari kabla ya kutoa maamuzi yake., kuna namna za kushughulikia kero na matatizo ya kinidhamu ya wabunge.., Spika atumie kamati za maadili, kamati za nidhamu za bunge kufanya maamuzi, sio vyema kuongoza taasisi kwa kutumia hisani ya mamlaka ya pekee kichwa.., wabunge wote ni wabunge wa bunge la Jamhuri.., wasibaguliwe kwa misingi ya itikadi zao za kisiasa..,

.., misingi ya UDIKTETA ni kufikiri kwamba una mamlaka makubwa zaidi ya yaliyoainishwa kisheria, kikanuni na kikatiba.., hakuna sehemu ambayo inatoa ruhusa kwa Spika wa bunge kumzuia mbunge kuzungumza au kutoa uwakilishi kwa wananchi wake katika kipindi cha ubunge wake wote..., lakini hilo linawezekana katika taasisi au nchi yenye kuongozwa katika misingi ya UDIKTETA.., sitaki kuamini kama tumefika huko, bado naendelea kuamini kwamba nchi yetu ipo salama, isipokuwa kuna watawala ambao wanafikiri wao ni "miungu watu"..., kanuni, taratibu na sheria zipo ili zifuatwe.., hakuna ambae yuko juu ya sheria za nchi..

Ipo siku mtawala wa sasa (wakati wowote) atakuwa mpinzani.., Sasa ni vyema kuishi kwa upendo na amani na tufuate sheria za nchi yetu bila kukomoana.., kwa sababu kuna maisha mengine baada ya madaraka kupita.., tuache kuishi kama wafalme kwenye nyakati za madaraka...
—————————————

MMM
FB_IMG_1505797717994.jpg
 
Naomba nirekebishiwe heading na uzi wangu upelekwe jukwaa husika la siasa.
 
Back
Top Bottom