Kiongozi wa zamani wa Bolivia ajaribu kujiua akiwa Gerezani

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
Rais wa zamani wa mpito wa Bolivia Jeanine Anez amefanya jaribio la kujiua akiwa jela siku moja baada ya kufunguliwa mashtaka ya "mauaji ya halaiki" kutokana na vifo vya waandamanaji vilivyotokea mwaka 2019.

Mmoja ya mawakili wa Anez, Jorge Valda, amesema kiongozi huyo wa zamani ambaye amefadhaishwa na tuhuma zinazomkabili alijaribu kuondoa uhai wake lakini jaribio hilo limeshindwa.

Anez, amekuwa jela tangu mwezi Machi mwaka huu kwa madai ya kufanya mapinduzi dhidi ya mtangulizi wake na rais wa zamani wa Bolivia, Evo Morales.

Mwanasiasa huyo anayeegemea sera za kihafidhina aliingia madarakani kama kiongozi wa mpito mwaka 2019 baada ya Morales kujiuzulu na kuikimbia nchi hiyo lakini wapinzani wanasema hatua yake ya kuchukua madaraka ilikuwa sawa na mapinduzi.
 
Back
Top Bottom