Kiongozi wa waismailia Aga Khan katika Tanganyika ya kikoloni

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,908
30,249
Nimeingia maktaba ili nai nichangie kitu katika mambo ambayo Waismailia, yaani Aga Khan walifanya katika kusaidia Waislam wa Tanganyika.

Al Jamiatul Islamiyya Muslim School

Katika miaka ya 1930s Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika walikuwa wanajenga shule ambayo sote tunaijua lakini hela zilikuwa tatizo jengo likawa limechukua muda mrefu kukamilika.

Sababu ya kujenga shule hii ni kuwa wazee wetu na wao walitaka wawe na mahali pa kuwasomesha watoto wao kuepuka vijana wao kubatizwa katika shule ambazo serikali ya kikoloni iliziweka mikononi kwa kanisa.

Kleist akiwa kiongozi wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika alitambua mapema sana kuwa tatizo kubwa lililokuwa likiwakabili Waislam ilikuwa ni kukosa elimu ambayo serikali ya kikoloni iliwaachia wamishionari waisimamie.

Si kama Waislam hawakuwa wanatambua faida ya elimu kwa watoto wao. Wazazi wengi walichelea kuwapeleka watoto wao shule kwa sababu wamishionari walichukua fursa hiyo kuwabatiza. Kuliko kwa watoto wao kutolewa katika Uislam na kuwa murtad, wazazi wengi waliamua kuisamehe elimu yenyewe kabisa.

Kleist aliona kuwa ufunguo wa tatizo hilo kwa Waislam ilikuwa ni kuanzisha shule zao wenyewe ambazo zitasomesha Qur’an pamoja na masomo mengine.

Wakati ule, na hata hivi sasa, Qur’an ilikuwa ikisomeshwa kwa mtindo wa asili ambapo mwanafunzi anakaa chini sakafuni mbele ya maalim akiwa na ubao wake na juzuu.

Katika madras kuchapa viboko, kwa jina maarufu mkambaa, ndiyo ulikuwa mtindo wa kusomeshea. Kleist hakuona sababu kwa nini Qur’an nayo isisomeshwe kama elimu nyingine, wanafunzi wakiwa madarasani wakikaa katika madawati.

Alilitoa wazo hili kwa rafiki zake akashauri madras ipanuliwe ili masomo mengine yasomeshwe pamoja na Uislam.

Ushauri huu ulijadiliwa kati ya Kleist, Ali Kiro, Maalim Popa Saleh na Shariff Salim. Wakitambua kazi kubwa iliyokuwa ikiwakabili, waliamua waanze hiyo shule kwa kidogo kidogo kwa awamu. Nyumba itakayokuwa shule ya muda ilitafutwa na wanafunzi wakaanza kusoma.

Kati ya walimu wa mwanzo wa shule hiyo walikuwa Mzee Ali Comorian na Sheikh Abdallah Idd Chaurembo ambao walikuwa kati ya wasomi wa Kiislam waliokuwa wakiheshimika.

Wazazi wa Kiislam waliombwa wachange fedha ili jengo la kudumu lijengwe.

Al Jamiatul Islamiyya ikawa inapita nyumba hadi nyumba ikusanya michango kutoka kwa Waislam.

Bahati nzuri mwaka wa 1936 Aga Khan alitembelea Tanganyika na akafahamishwa kuhusu ujenzi wa shule ile.

Katika hafla ile mtoto aliysoma risala kwa Aga Khan alikuwa Abdul Sykes akiwa na umri wa miaka 12.

Marehemu Kanyama Chiume amenihadithia kuwa wakati huu alipofika Aga Khan Tanganyika yeye alikuwa anasoma Shule ya Kitchwele na alikuwa katika bendi ya shule iliyompokea yeye akipiga, ‘’triangle,’’ na alinieleza kuwa picha yake yeye akipiga, ‘’triangle,’’ ilitokea katika gazeti.

Aga Khan alitoa fedha na shule ikajengwa New Street si mbali sana na ilipokuwa ofisi ya African Association.

Kleist akawa katika kamati ya ujenzi akikagua kazi hadi ujenzi ulipokamilika. Hii ni moja kati ya shule za mwanzo kujengwa na Waislam wa Tanganyika. Jengo la Al Jamiatul Islamiyya lipo limesimama hadi leo kama ushahidi na kumbukumbu za juhudi za Waislam katika kujiletea maendeleo yao.

Serikali katika kuthamini mchango wa Kleist katika kupeleka mbele elimu kwa ajili ya watoto wa Kiislam ikamchagua kuwa katika Provincial Education Committee of Tanganyika Education.
Mwanae Abdulwahid na yeye vilevile akaja kuwa katika Aga Khan Education Committee.

Halikadhalika walimu wawili wa Al Jamiatul Islamiyya walipewa nafasi muhimu katika siasa na uongozi wa nchi na Sheikh Juma Mwindadi alifanywa mjumbe katika Baraza la Mji wa Dar es Salaam.

Mwaka 1956 Aga Khan alipotembelea Tanganyika Waismailia walimnunulia Mercedes Benz 280S yenye usajili DSQ 666 na hii ndiyo alikuwa akitembeanayo mjini Dar es Salaam.

Mwaka wa 1959 Waismailia waliamua kuiuza gari hii lakini hawakutaka inunuliwe na Muismailia ila inunuliwe na mtu yoyote mwenye hadhi katika jamii ya Watanganyika nje yao.

Gari hii aliuziwa Abdul Sykes na alikaanayo hadi alipofariki 1968.
 
''...zitasomesha Qur’an pamoja na masomo mengine.''

Kipaumbele cha waislam ilikuwa Ilm akhera halafu kwa mbali elimu dunia. Vijana wengi wa kiislam walikosa elimu dunia tokea zamani na ndio maana hili jambo limewatesa kwa muda mrefu na kuanza kushambulia wakristo kuwa wanawanyonya huku wakisahau wakristu wao waliwekeza katika elimu yenye manufaa zaidi.
 
Kuna shida iko mahali, na hata mtoa Maada hataki kuieleza, Waarabu walikuwa kwenye pwani ya Tanganyika na ndani ya Tanganyika kwa Zaidi ya Miaka 500, iweje shule ya kwanza ije kujengwa 30s?, Maana Wareno kwenye miaka ya 1400 walionyeshwa njia ya kwenda India na Waarabu waliowakuta hapa Pwani ya East Africa,
 
Sio kweli,shule ya kwanza ya secondary,Tanganyika ilijengwa Tanga,na mpaka le ipo katikati ya jiji la Tanga,inaitwa Old Tanga Secondary School,ni shule ambayo ina maendeleo mazuri kabisa,na ni shule ambayo mpaka leo iko katika hali yake ya ujenzi wa kihistoria.Na vile vile shule ya kwanza ya secondary kujengwa baada ya Uhuru,ni Tanga School,shule hii ipo mpaka leo.Shule hizi ndio za kwanza,na ziko katika mji uliokuwa na waislamu wengi.
Hizi shule ,kuna mchango mkubwa wa wazee wa kiislamu,wakiwemo waarabu na waafrika.
 
Kuna shida iko mahali, na hata mtoa Maada hataki kuieleza, Waarabu walikuwa kwenye pwani ya Tanganyika na ndani ya Tanganyika kwa Zaidi ya Miaka 500, iweje shule ya kwanza ije kujengwa 30s?, Maana Wareno kwenye miaka ya 1400 walionyeshwa njia ya kwenda India na Waarabu waliowakuta hapa Pwani ya East Africa,
Waismailiya sio waarabu,ni wahindi,ikiwa, hata mataifa hamyajui,mtajua historia.Historia inavyoonyesha kulikuwako na waalimu waarabu,kwa mfano Korogwe,miongoni Kwa waalimu maarufu alikuwako Mohammed Salim Alhousni,huyu alikuwa mwalimu maarufu kwenye miaka ya 1920,na wapo madaktari,ambao wazazi wao walisoma kwa mwalimu huyu,na kuzaa watoto kwa kuwapa jina lake,la Mohammed,lakini kutokana na mwenye jina ni mwalimu walibakia watoto hawa kuitwa,Mwalimu.
 
''...zitasomesha Qur’an pamoja na masomo mengine.''

Kipaumbele cha waislam ilikuwa Ilm akhera halafu kwa mbali elimu dunia. Vijana wengi wa kiislam walikosa elimu dunia tokea zamani na ndio maana hili jambo limewatesa kwa muda mrefu na kuanza kushambulia wakristo kuwa wanawanyonya huku wakisahau wakristu wao waliwekeza katika elimu yenye manufaa zaidi.
Elimu ipi ya manufaa zaidi ya kupotoshana kuwa yesu ni mungu, kumjua m'mungu wa kweli ni elimu yenye manufaa kuliko chengine chochote kile
 
Chachu Ombara,
Naam Qur'an kwetu sisi ndicho bora zaidi lakini wazee wetu hawakupuuza
elimu ya sekula na ndiyo maana umeona wakajenga shule.

Baada ya uhuru 1961, mwaka wa 1962 Waislam walifanya mkutano wa
kwanza, Muslim Congress na wakaweka azimio la kujenga shule na chuo
kikuu.

Hii ni historia ya pekee katika historia ya Waislam wa Tanganyika na kwa
urefu kabisa nimeeleza yaliyotokea kati ya serikali na uongozi wa Waislam
chini ya East African Muslim Welfare Society (EAMWS) ilipodhihirika kuwa
kwa mipango hiyo Waislam watajinasua katika mtego wa elimu uliokuwa
umetegwa na wakoloni wakishirikiana na wamishionari.

Hiki ni kisa maalum kipo katika kitabu cha Abdul Sykes.
 
Waismailiya sio waarabu,ni wahindi,ikiwa, hata mataifa hamyajui,mtajua historia.Historia inavyoonyesha kulikuwako na waalimu waarabu,kwa mfano Korogwe,miongoni Kwa waalimu maarufu alikuwako Mohammed Salim Alhousni,huyu alikuwa mwalimu maarufu kwenye miaka ya 1920,na wapo madaktari,ambao wazazi wao walisoma kwa mwalimu huyu,na kuzaa watoto kwa kuwapa jina lake,la Mohammed,lakini kutokana na mwenye jina ni mwalimu walibakia watoto hawa kuitwa,Mwalimu.

Nani aliyesema WaIsmailia ni Waarabu, ebu nionyeshe hiyo sehemu, acha ukurupukaji wewe, yaani wewe ukisikia mdundiko tu unatoka ndani na mtandio huku kidole juu,
 
Soma hapo,'WAARABU walikuwa kwenye Pwani ya Tanganyika'.Unakimbia kivuli chako,baada ya kukupa ushahidi kama waarabu na waafrika waislamu,walianzisha shule,na wengine kuwa waalimu.Kulikuwako na waalimu Waafrika waislamu maarufu,kama Mwalimu Pera,Mwalimu wa Mwalimu,na wengine wengi.
Kuna shida iko mahali, na hata mtoa Maada hataki kuieleza, Waarabu walikuwa kwenye pwani ya Tanganyika na ndani ya Tanganyika kwa Zaidi ya Miaka 500, iweje shule ya kwanza ije kujengwa 30s?, Maana Wareno kwenye miaka ya 1400 walionyeshwa njia ya kwenda India na Waarabu waliowakuta hapa Pwani ya East Africa,
 
Kuna shida iko mahali, na hata mtoa Maada hataki kuieleza, Waarabu walikuwa kwenye pwani ya Tanganyika na ndani ya Tanganyika kwa Zaidi ya Miaka 500, iweje shule ya kwanza ije kujengwa 30s?, Maana Wareno kwenye miaka ya 1400 walionyeshwa njia ya kwenda India na Waarabu waliowakuta hapa Pwani ya East Africa,
Kituko,
Soma historia utaona kuwa shule za kwanza Pwani ya Afrika ya Mashariki
ni madras za Waislam.

Katika madras hizo ndipo wanafunzi walipojifunza zile 3Rs yaani Reading,
Writing and Arithmetic.

Msome Ishumi yeye katafiti sana katika masuala haya ya elimu.
Hebu soma niliyoandika katika kitabu cha Abdul Sykes:

''Wajerumani walipofika Tanganyika waliwakuta Waislam wanafahamu kuandika, kusoma na walikuwa wameelimika katika hesabu. Mmishionari Ludwig Krapf alipofika kwa Chifu Kimweri wa Usambaa mwaka 1848 alimkuta yeye na wanae wote wanajua kusoma. Herufi walizokuwa wakitumia zilikuwa za Kiarabu. Wajerumani kwa ajili hii basi waliwaajiri Waislam kama walimu, wakalimani na makarani serikalini. Wamisionari na wakoloni waliona wivu kwa maendeleo haya waliyoyakuta kwa Waislam. Kubwa zaidi ni kuwa walikuwa wamekuja kustaarabisha watu ëwashenzi' badala yake wamewakuta watu walistaaarabika na wanye utamaduni wa kupendeza. Elimu hii yote na utamaduni huu wa hali ya juu ulikuwa unatokana na Uislam na shule zake ñ madras. Hapo ndipo zilipoaanza mbinu ya kuvunja maendeleo haya yote.

Herufi za Kiarabu zikapigwa marufuku kutumika na badala yake watu wakalazimishwa kujifunza herufi za Kirumi. Muislam ambae jana alipoingia kulala alikuwa anaitwa ameelimika akaamka asubuhi yake mjinga, hana elimu, hajui kusoma wala kuandika. Njama hizi zote dhidi ya Uislam ilikuwa sehemu ya makubaliano kama ilivyoandikwa katika kifungu IV cha Mkutano wa Berlin wa mwaka 1884. Kifungu hicho kilikuwa kinasema kuwa Ukristo ni lazima ulindwe dhidi ya Uislam.

Kati ya mwaka 1888-1892 katika kutekeleza kifungu hicho kama ilivyokubalika katia Mkutano wa Berlin, Imperial British East Africa Company ilitumia nguvu za kisiasa na kijeshi kuulinda Ukristo katika Afrika ya Mashariki. Ombwe lililoachwa na elimu ya Kiislam ikajazwa na elimu ya Kanisa chini ya usimamizi wa Waingereza. Kanisa hivi sasa linaeneza uongo na propaganda kuwa lenyewe ndilo lililoweka msingi wa kwanza wa elimu Tanganyika. Ukweli ni kuwa Wamisionari walifuata nyayo za madras na walimu wa kwanza katika shule za misheni walikuwa Waislam ambao hawakusoma katika shule za kanisa bali katika madras.''

Kituko,
Kabala ya kutaka kuja kujibizana na Mohamed Said angalau ungefanya
utafiti kidogo.
 
Soma hapo,'WAARABU walikuwa kwenye Pwani ya Tanganyika'.Unakimbia kivuli chako,baada ya kukupa ushahidi kama waarabu na waafrika waislamu,walianzisha shule,na wengine kuwa waalimu.Kulikuwako na waalimu Waafrika waislamu maarufu,kama Mwalimu Pera,Mwalimu wa Mwalimu,na wengine wengi.

Hivi wewe jamaa una shida gani?, hivi kweli unajua ulichoandika? Wapi niliposema WaIsmailia ni Waarabu?,

Kweli ukweli lazima ukubali kaka, Anachokiongelea Mtoa maada ni kingine na wewe unachoandika ni kingine, hakuna Mwarabu aliyejenga shule ya kufundisha Elmu Dunia kabla ya Mzungu, swali ni vipi kwa Mwarabu waliokaa miaka yote hapa Tanganyika/Tanzania lakini hawakujenga shule nje ya hizo za kidini?
 
Kaka Mohamed Said , mi wala sipingi hilo la shule za Madrasa, lakini wewe hoja yako haizungujzii hizo shule, shule unayoizungumza wewe ni shule ya kawaida japo ilikuwa na masomo ya Kidini, Swali nililouliza ilikuwaje Waarabu waliokuwa hapa zaidimya Miaka 400 walishindwa kujenga shule za kawaida?
 
Mwalimu Pera,huyu nadhani ndiye ndie aliyekuwa mwalimu mkuu wa shule ya msambweni Tanga.
 
Hivi wewe jamaa una shida gani?, hivi kweli unajua ulichoandika? Wapi niliposema WaIsmailia ni Waarabu?,

Kweli ukweli lazima ukubali kaka, Anachokiongelea Mtoa maada ni kingine na wewe unachoandika ni kingine, hakuna Mwarabu aliyejenga shule ya kufundisha Elmu Dunia kabla ya Mzungu, swali ni vipi kwa Mwarabu waliokaa miaka yote hapa Tanganyika/Tanzania lakini hawakujenga shule nje ya hizo za kidini?
Soma post # 13,umeshajibiwa.Na vile vile kumbuka mtoa mada,alianza na historia ya Dar.Bado hajakupa ya ,Zanzibar,Tanga,Bagamoyo,Mombasa,Lamu na Pwani mpaka ya Msumbiji.
 
Nimeingia maktaba ili nai nichangie kitu katika mambo ambayo Waismailia, yaani Aga Khan walifanya katika kusaidia Waislam wa Tanganyika.

Al Jamiatul Islamiyya Muslim School

Katika miaka ya 1930s Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika walikuwa wanajenga shule ambayo sote tunaijua lakini hela zilikuwa tatizo jengo likawa limechukua muda mrefu kukamilika.

Sababu ya kujenga shule hii ni kuwa wazee wetu na wao walitaka wawe na mahali pa kuwasomesha watoto wao kuepuka vijana wao kubatizwa katika shule ambazo serikali ya kikoloni iliziweka mikononi kwa kanisa.

Kleist akiwa kiongozi wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika alitambua mapema sana kuwa tatizo kubwa lililokuwa likiwakabili Waislam ilikuwa ni kukosa elimu ambayo serikali ya kikoloni iliwaachia wamishionari waisimamie.

Si kama Waislam hawakuwa wanatambua faida ya elimu kwa watoto wao. Wazazi wengi walichelea kuwapeleka watoto wao shule kwa sababu wamishionari walichukua fursa hiyo kuwabatiza. Kuliko kwa watoto wao kutolewa katika Uislam na kuwa murtad, wazazi wengi waliamua kuisamehe elimu yenyewe kabisa.

Kleist aliona kuwa ufunguo wa tatizo hilo kwa Waislam ilikuwa ni kuanzisha shule zao wenyewe ambazo zitasomesha Qur’an pamoja na masomo mengine.

Wakati ule, na hata hivi sasa, Qur’an ilikuwa ikisomeshwa kwa mtindo wa asili ambapo mwanafunzi anakaa chini sakafuni mbele ya maalim akiwa na ubao wake na juzuu.

Katika madras kuchapa viboko, kwa jina maarufu mkambaa, ndiyo ulikuwa mtindo wa kusomeshea. Kleist hakuona sababu kwa nini Qur’an nayo isisomeshwe kama elimu nyingine, wanafunzi wakiwa madarasani wakikaa katika madawati.

Alilitoa wazo hili kwa rafiki zake akashauri madras ipanuliwe ili masomo mengine yasomeshwe pamoja na Uislam.

Ushauri huu ulijadiliwa kati ya Kleist, Ali Kiro, Maalim Popa Saleh na Shariff Salim. Wakitambua kazi kubwa iliyokuwa ikiwakabili, waliamua waanze hiyo shule kwa kidogo kidogo kwa awamu. Nyumba itakayokuwa shule ya muda ilitafutwa na wanafunzi wakaanza kusoma.

Kati ya walimu wa mwanzo wa shule hiyo walikuwa Mzee Ali Comorian na Sheikh Abdallah Idd Chaurembo ambao walikuwa kati ya wasomi wa Kiislam waliokuwa wakiheshimika.

Wazazi wa Kiislam waliombwa wachange fedha ili jengo la kudumu lijengwe.

Al Jamiatul Islamiyya ikawa inapita nyumba hadi nyumba ikusanya michango kutoka kwa Waislam.

Bahati nzuri mwaka wa 1936 Aga Khan alitembelea Tanganyika na akafahamishwa kuhusu ujenzi wa shule ile.

Katika hafla ile mtoto aliysoma risala kwa Aga Khan alikuwa Abdul Sykes akiwa na umri wa miaka 12.

Marehemu Kanyama Chiume amenihadithia kuwa wakati huu alipofika Aga Khan Tanganyika yeye alikuwa anasoma Shule ya Kitchwele na alikuwa katika bendi ya shule iliyompokea yeye akipiga, ‘’triangle,’’ na alinieleza kuwa picha yake yeye akipiga, ‘’triangle,’’ ilitokea katika gazeti.

Aga Khan alitoa fedha na shule ikajengwa New Street si mbali sana na ilipokuwa ofisi ya African Association.

Kleist akawa katika kamati ya ujenzi akikagua kazi hadi ujenzi ulipokamilika. Hii ni moja kati ya shule za mwanzo kujengwa na Waislam wa Tanganyika. Jengo la Al Jamiatul Islamiyya lipo limesimama hadi leo kama ushahidi na kumbukumbu za juhudi za Waislam katika kujiletea maendeleo yao.

Serikali katika kuthamini mchango wa Kleist katika kupeleka mbele elimu kwa ajili ya watoto wa Kiislam ikamchagua kuwa katika Provincial Education Committee of Tanganyika Education.
Mwanae Abdulwahid na yeye vilevile akaja kuwa katika Aga Khan Education Committee.

Halikadhalika walimu wawili wa Al Jamiatul Islamiyya walipewa nafasi muhimu katika siasa na uongozi wa nchi na Sheikh Juma Mwindadi alifanywa mjumbe katika Baraza la Mji wa Dar es Salaam.

Mwaka 1956 Aga Khan alipotembelea Tanganyika Waismailia walimnunulia Mercedes Benz 280S yenye usajili DSQ 666 na hii ndiyo alikuwa akitembeanayo mjini Dar es Salaam.

Mwaka wa 1959 Waismailia waliamua kuiuza gari hii lakini hawakutaka inunuliwe na Muismailia ila inunuliwe na mtu yoyote mwenye hadhi katika jamii ya Watanganyika nje yao.

Gari hii aliuziwa Abdul Sykes na alikaanayo hadi alipofariki 1968.
Historia iliyotukuka.
 
Kaka Mohamed Said , mi wala sipingi hilo la shule za Madrasa, lakini wewe hoja yako haizungujzii hizo shule, shule unayoizungumza wewe ni shule ya kawaida japo ilikuwa na masomo ya Kidini, Swali nililouliza ilikuwaje Waarabu waliokuwa hapa zaidimya Miaka 400 walishindwa kujenga shule za kawaida?
Kituko,
Madrasa ni shule.
Darsa ni darasa na darasa ni shule.

Hivi wewe shule hadi pawe na kuta, milango na madirisha?

Sisi kwetu maalim anaweza kusomesha bila ya jengo na
ilm yote hii iliyopo Afrika ya Mashariki imesomeshwa kwa
mtindo huo.
 
Elimu ipi ya manufaa zaidi ya kupotoshana kuwa yesu ni mungu, kumjua m'mungu wa kweli ni elimu yenye manufaa kuliko chengine chochote kile
Yeah kujua kama muhamad alikao katoto ka miaka Tisa na kuahidiwa bikra 70 na mito ya pombe peponi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom