Kiongozi wa UVCCM atokomea na mamilioni aliyochangisha Nahodha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kiongozi wa UVCCM atokomea na mamilioni aliyochangisha Nahodha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BONGOLALA, Feb 15, 2012.

 1. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #1
  Feb 15, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,785
  Likes Received: 2,395
  Trophy Points: 280
  sasa wanaccm wameamua kuwa wanyang'anyi wa mchana
   
 2. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #2
  Feb 15, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,148
  Likes Received: 2,106
  Trophy Points: 280
  ndo nini sasa hii, kama bado umesinzia si usubiri kuche uandike vizuri? Wacha uzushi
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Feb 15, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mkuu taarifa nusu nusu hatuzitaki humu. Endapo ulionelea kuwa na mapenzi makubwa sana na hizo taarifa KAMILI ulizozipata basi ni mara 100 ungebaki nazo tu usituchokoze nazo hamu hivi.

  Weka kila kitu kilichokamilika humu ili tupate pa kushika tunapoanza mjadala wetu humu.

 4. sumasuma

  sumasuma JF-Expert Member

  #4
  Feb 15, 2012
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 331
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  MWENYEWE ALITOA SH2 MILIONI, SHEKIFU, OLE SENDEKA NAO WALICHANGIA
  Peter Saramba, Arusha
  MMOJA wa wanachama wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Wilaya ya Simanjiro, mkoani Manyara, anadaiwa kutoroka na zaidi ya Sh26 milioni za jumuiya hiyo zilizochangwa kwenye harambee iliyofanyika Mei 9, mwaka juzi na kuongozwa na aliyekuwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha.
Akizungumza kwa simu kutoka Mererani, Simanjiro, Mwenyekiti wa UVCCM wilayani humo, Kiria Laizer alithibitisha kuwa fedha hizo zilizochangwa kwa lengo la kutunisha mfuko wa maendeleo ya vijana Simanjiro ziliyeyuka muda mfupi baada ya harambee hiyo.

  Katika harambee hiyo, Nahodha ambaye sasa ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi alichanga fedha taslimu Sh2 milioni.
  Ilielezwa kwamba wageni wawili waliohudhuria shughuli hiyo kwa mwaliko wa mtuhumiwa huyo ambao walitambulishwa ukumbini kuwa dada wa Rais Kikwete, walichangia 400,000.

  Kwa mujibu wa kumbukumbu rasmi za shughuli hiyo, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Henry Shekifu ambaye sasa ni Mbunge wa Lushoto (CCM), alichangia Sh500,000.

  Viongozi wengine waliohudhuria na kiasi walichochanga kwenye mabano ni Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Khalid Mandya (200,000), Mbunge wa Simanjiro (CCM), Christopher Ole Sendeka (Sh1.5 milioni), na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Manyara, Lucas Ole Mukusi (Sh100,000).

  Laizer alisema tukio la wizi huo limebaki kuwa kama mchezo wa kuigiza huku baadhi ya wanachama na viongozi wenzake wakimtuhumu hata yeye wakidhani alihusika kwa njia moja au nyingine.

  “Baada ya mgeni rasmi (Nahodha) kunikabidhi mfuko wenye fedha usiku ule pale ukumbini, nilimwita (mtuhumiwa jina tunalo) na kumkabidhi mbele na wajumbe wawili wa kamati ya utekelezaji wilaya na tangu siku ile, sijawahi kumwona wala kupata mawasiliano naye,” alisema Laizer.

  Aliwataja Wajumbe wa Kamati ya Utendaji walioshuhudia makabidhiano hayo kuwa ni Bonny Shongo na Paul Sipitet.
  “Siku tatu baadaye tulimtafuta (mtuhumiwa), bila mafanikio na tulipompata kwa njia ya simu alidai yuko Mjini Arusha kwa shughuli binafsi lakini baada ya muda mfupi alitutumia ujumbe mfupi wa simu akitutaka kutafuta mtu mwingine (wa kujaza nafasi yake) kwani yeye ameondoka,” alisema Sipitet.

  Katibu wa UVCCM wilayani humo, Mwanakombo Amiri alisema kwa simu hakuna kumbukumbu yoyote kwenye majalada ya kiofisi inayohusu kikao cha maandalizi wala fedha zilizopatikana kwenye harambee hiyo.

  “Hakuna chochote kwenye faili kuhusu jambo hilo unalouliza. Kikao kilichopita cha kamati ya utekelezaji kilizungumzia suala hilo ingawa haikuwa moja ya ajenda. Ila kikao kijacho ambacho siwezi kukutajia kitafanyika lini hilo ni moja ya ajenda muhimu na tutatoa uamuzi kulingana na kanuni zetu,” alisema Mwanakombo.

  Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, ambaye ni miongoni mwa waliotafuniwa fedha zao walizochangia alithibitisha ofisi yake kupokea taarifa za fedha za kuyeyuka kwake na kusema tayari ameziagiza ngazi husika (UVCCM), kuchukua hatua kulingana na kanuni na taratibu zao na pia kutoa taarifa polisi ili hatua za kisheria zichukuliwe.

  “Sisi kama Serikali, chama kikichukua hatua na kuwasilisha taarifa, nitaagiza polisi wachukue hatua za kisheria kwa kuchunguza na kumtia mbaroni mtuhumiwa. Nakushauri pia uwasiliane na katibu wa CCM wilaya ambaye ndiye mlezi wa jumuiya zote za chama ngazi ya wilaya,” alisema Mandya.

  Mkuu huyo wa wilaya alisema baada ya ofisi yake kutopata taarifa za utekelezaji wa amri yake ya mhusika kuchukuliwa hatua hadi sasa, ameamua kuuandikia barua rasmi uongozi wa UVCCM na chama wilaya kudai utekelezaji wa agizo lake kutokana na wahusika kuonekana wazito katika jambo hilo.

  Hata hivyo, Katibu wa CCM Wilaya ya Simanjiro, Jamila Mjungu alikataa kuzungumzia suala hilo akisema UVCCM ni jumuiya inayojitegemea, yenye viongozi na wasemaji na kanuni za kutatua matatizo yao.

  Uchunguzi wa kina umebaini kuwa mtuhumiwa huyo sasa ni diwani katika moja ya kata za Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma ambako aligombea na kushinda kwenye uchaguzi mkuu uliopita.

  Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigela alisema ingawa jambo hilo halijaripotiwa kwake na uongozi wa wilaya ya Simanjiro, atafuatilia na kuhakikisha mhusika anachukuliwa hatua kulingana na kanuni za jumuiya hiyo na sheria za nchi bila kujali cheo, umaarufu wala nasaba yake na viongozi.

  “Kwanza inawezekana mtuhumiwa ni tapeli mzoefu anayetumia jina la mheshimiwa Rais na familia yake kuwatisha
  :A S 465:
   
 5. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #5
  Feb 15, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Naona huko ndani ya CCM si baba si mwana wala nini; wote ni wakwapwaji hodari kila mahali. Baada ya kutukwapulia vya kutosha huko serikalini naona sasa wameanza kugeuziana kibao wao kwa woa tu.

  ----------------------------------------------------------------------------

  MWENYEWE ALITOA SH2 MILIONI, SHEKIFU, OLE SENDEKA NAO WALICHANGIA

  Peter Saramba, Arusha

  MMOJA wa wanachama wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Wilaya ya Simanjiro, mkoani Manyara, anadaiwa kutoroka na zaidi ya Sh26 milioni za jumuiya hiyo zilizochangwa kwenye harambee iliyofanyika Mei 9, mwaka juzi na kuongozwa na aliyekuwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha.

  Akizungumza kwa simu kutoka Mererani, Simanjiro, Mwenyekiti wa UVCCM wilayani humo, Kiria Laizer alithibitisha kuwa fedha hizo zilizochangwa kwa lengo la kutunisha mfuko wa maendeleo ya vijana Simanjiro ziliyeyuka muda mfupi baada ya harambee hiyo.

  Katika harambee hiyo, Nahodha ambaye sasa ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi alichanga fedha taslimu Sh2 milioni.
  Ilielezwa kwamba wageni wawili waliohudhuria shughuli hiyo kwa mwaliko wa mtuhumiwa huyo ambao walitambulishwa ukumbini kuwa dada wa Rais Kikwete, walichangia 400,000.

  Kwa mujibu wa kumbukumbu rasmi za shughuli hiyo, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Henry Shekifu ambaye sasa ni Mbunge wa Lushoto (CCM), alichangia Sh500,000.

  Viongozi wengine waliohudhuria na kiasi walichochanga kwenye mabano ni Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Khalid Mandya (200,000), Mbunge wa Simanjiro (CCM), Christopher Ole Sendeka (Sh1.5 milioni), na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Manyara, Lucas Ole Mukusi (Sh100,000).

  Laizer alisema tukio la wizi huo limebaki kuwa kama mchezo wa kuigiza huku baadhi ya wanachama na viongozi wenzake wakimtuhumu hata yeye wakidhani alihusika kwa njia moja au nyingine.

  "Baada ya mgeni rasmi (Nahodha) kunikabidhi mfuko wenye fedha usiku ule pale ukumbini, nilimwita (mtuhumiwa jina tunalo) na kumkabidhi mbele na wajumbe wawili wa kamati ya utekelezaji wilaya na tangu siku ile, sijawahi kumwona wala kupata mawasiliano naye," alisema Laizer.

  Aliwataja Wajumbe wa Kamati ya Utendaji walioshuhudia makabidhiano hayo kuwa ni Bonny Shongo na Paul Sipitet.
  "Siku tatu baadaye tulimtafuta (mtuhumiwa), bila mafanikio na tulipompata kwa njia ya simu alidai yuko Mjini Arusha kwa shughuli binafsi lakini baada ya muda mfupi alitutumia ujumbe mfupi wa simu akitutaka kutafuta mtu mwingine (wa kujaza nafasi yake) kwani yeye ameondoka," alisema Sipitet.

  Katibu wa UVCCM wilayani humo, Mwanakombo Amiri alisema kwa simu hakuna kumbukumbu yoyote kwenye majalada ya kiofisi inayohusu kikao cha maandalizi wala fedha zilizopatikana kwenye harambee hiyo.

  "Hakuna chochote kwenye faili kuhusu jambo hilo unalouliza. Kikao kilichopita cha kamati ya utekelezaji kilizungumzia suala hilo ingawa haikuwa moja ya ajenda. Ila kikao kijacho ambacho siwezi kukutajia kitafanyika lini hilo ni moja ya ajenda muhimu na tutatoa uamuzi kulingana na kanuni zetu," alisema Mwanakombo.

  Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, ambaye ni miongoni mwa waliotafuniwa fedha zao walizochangia alithibitisha ofisi yake kupokea taarifa za fedha za kuyeyuka kwake na kusema tayari ameziagiza ngazi husika (UVCCM), kuchukua hatua kulingana na kanuni na taratibu zao na pia kutoa taarifa polisi ili hatua za kisheria zichukuliwe.

  "Sisi kama Serikali, chama kikichukua hatua na kuwasilisha taarifa, nitaagiza polisi wachukue hatua za kisheria kwa kuchunguza na kumtia mbaroni mtuhumiwa. Nakushauri pia uwasiliane na katibu wa CCM wilaya ambaye ndiye mlezi wa jumuiya zote za chama ngazi ya wilaya," alisema Mandya.

  Mkuu huyo wa wilaya alisema baada ya ofisi yake kutopata taarifa za utekelezaji wa amri yake ya mhusika kuchukuliwa hatua hadi sasa, ameamua kuuandikia barua rasmi uongozi wa UVCCM na chama wilaya kudai utekelezaji wa agizo lake kutokana na wahusika kuonekana wazito katika jambo hilo.

  Hata hivyo, Katibu wa CCM Wilaya ya Simanjiro, Jamila Mjungu alikataa kuzungumzia suala hilo akisema UVCCM ni jumuiya inayojitegemea, yenye viongozi na wasemaji na kanuni za kutatua matatizo yao.

  Uchunguzi wa kina umebaini kuwa mtuhumiwa huyo sasa ni diwani katika moja ya kata za Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma ambako aligombea na kushinda kwenye uchaguzi mkuu uliopita.

  Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigela alisema ingawa jambo hilo halijaripotiwa kwake na uongozi wa wilaya ya Simanjiro, atafuatilia na kuhakikisha mhusika anachukuliwa hatua kulingana na kanuni za jumuiya hiyo na sheria za nchi bila kujali cheo, umaarufu wala nasaba yake na viongozi.

  "Kwanza inawezekana mtuhumiwa ni tapeli mzoefu anayetumia jina la mheshimiwa Rais na familia yake kuwatisha
   
 6. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #6
  Feb 15, 2012
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Kwa CCM sio ajabu..anatekeleza ilani yao!
   
 7. NGUVUMOJA

  NGUVUMOJA JF-Expert Member

  #7
  Feb 15, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,353
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Marehemu "uaminifu"alishazikwa kitamambo.
   
 8. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #8
  Feb 15, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  huu ni uzushi.hii habari ni ya mwaka juzi na ilishajadiliwa sana hapa na pia ilikuja kugundulika kuwa haikuwa ya kweli.labda wewe una chuki zako umeamua kuzimalizia hapa,ndio siasa yenyewe.
   
 9. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #9
  Feb 15, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Kwa style hiyo hata mimi ningeingia nazo mitini
   
 10. MTENGETI

  MTENGETI JF-Expert Member

  #10
  Feb 15, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,330
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Hilo dogo kama mliwahi kusikia habari ya Riziwani nkunyangayana kipaza sauti Moshi mwaka 2009. Magamba hayo hayo madogo UVCCM walifanya Harambee ya mkoa mGENI rASMI akiwa ni mwana wa mkulima. tukachanga 30,000,000/= baada ya muda nazo zikayeyuka hivyo hivyo. Mwenyekiti wa Magamba madogo Mkoa wa KILIMANJARO GOODLIVING MOSHI AKAOTA SHAVU GHAFLA, KATIBU WAKE BW. YASINI LEMA ALIKUWA akagongwa na gari akiendesha pikipiki kisa alikuwa anafuatilia fedha hizo. baada ya kufikishwa Hospital KCMC akahamishiwa VIP. then pesa zikatafunwa weeee. mpaka leo milioni thirty kwishney. HAO NDIO MAGAMBA BANA
   
 11. p

  panadol JF-Expert Member

  #11
  Feb 15, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 352
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huu ni uzushi unasababu zako binafsi haya mambo yalishajadiliwa na kuisha ni fitina za kisiasa kuchafuana ili kupoteazana mvuto kwa jamii haya mambo yalishakwisha na ikagundulika ni fitina!
   
 12. Adrian Stepp

  Adrian Stepp Verified User

  #12
  Feb 15, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 2,222
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  Kwani Nahodha alipo kukabidhi lile fuko la hela usiku ule ulikimbilia wapi??? saburi bar??

 13. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #13
  Feb 15, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Like Father, like Son. This is CCM bana! Chukua Chako Mapema.
   
 14. J

  J.K.Rayhope JF-Expert Member

  #14
  Feb 15, 2012
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 316
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Acha ziliwe,kwani kama zingesimamiwa na kuelekezwa ktk mambo ya kijamii,nadhani zilikuwa na lengo hilo tu,sasa kungekuwa na picha nyingine.Kazi haikuwa kuzichangisha.Mtu akishakaa kwenye kiti cha kuzunguka,full ac,tai kubwa kama tambara la deki,kimini suti mapaja nje full muonekano,nyuma ya laptop au desktop basi anaona anaongoza.Toka na uangalie kazi yako kwa vitendo
   
 15. d

  davidie JF-Expert Member

  #15
  Feb 15, 2012
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 329
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  rais wa migomo nimeamini wewe ni migomo full maana hata jambo la ukweli utagoma kulikubali lakini kumbuka kuwa UVCCM NI UMOJA WA VIJANA CHAMA CHA MAJAMBAZI
   
 16. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #16
  Feb 15, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,792
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  Anatekeleza ilani ya Chama.
   
 17. Alfred Daud Pigangoma

  Alfred Daud Pigangoma Verified User

  #17
  Feb 15, 2012
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,778
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Ni moja yha mafunzo wanayopata! Wakikosa kuiba kura wanaiba hata fedha zilizopo mbele yao!..........
   
 18. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #18
  Feb 15, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,641
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Huyu kaiva sana ki chama huyu. Na hiki ndo chama kinachong'ang'ania dhamana ya kuongoza nchi.
  Halafu nahisi kunamtu karushwa kwenye mgao ndo maana katoa habari hii.
   
 19. K

  Kizotaka JF-Expert Member

  #19
  Feb 15, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 568
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hawa maandazi washakuwa kama mateja!sasa maandazi kama huyo ndo wamekabidhiwa nchi?
   
Loading...