Jeshi la Polisi wilayani Uvinza mkoani Kigoma limemkamata Kiongozi wa UKAWA na Katibu Mkuu wa NCCR Mosena Nyambabe kwa kile wanachodai ni uchochezi.
Kiongozi huyo amelala Rumande jana na leo anahamishiwa makao makuu ya Jeshi hilo Mkoani Kigoma.
Mosena Nyambabe ni mkuu wa Msafara wa viongozi wa UKAWA ambao wako Kigoma kuzungumza na wananchi.
Mkoa wa Kigoma ni moja ya Ngome Kuu za UKAWA huku chama cha NCCR kikiwa na jumla ya wabunge wanne mkoani humo.
Kukamatwa kwa Kiongozi huyo wa UKAWA ni baada ya mbinu mbalimbali na vitisho vya serikali dhidi ya UKAWA kushindwa kufua dafu.
CCM ilibuni mbinu nyingine ya kuwatumia mamluki kutoa taarifa za kupinga UKAWA kwenye vyombo vya habari lakini nayo mbinu hiyo imeshindwa.
Wakati akihutubia Zanzibar Mmoja wa viongozi wakuu wa UKAWA Maalim Seif Sharrif Hamad aliwataka viongozi wa UKAWA kujizatiti kwani zitatumika mbinu mbalimbali kuwatisha zikiwemo kuwakamata na kuwafungulia mashtaka.Lakini aliwaambia wasife moyo kwani ushindi utakuwa unakaribia.
Source:Mwananchi Breaking News