Kiongozi wa UKAWA na Katibu Mkuu NCCR akamatwa na Polisi!

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,492
2,000
Jeshi la Polisi wilayani Uvinza mkoani Kigoma limemkamata Kiongozi wa UKAWA na Katibu Mkuu wa NCCR Mosena Nyambabe kwa kile wanachodai ni uchochezi.

Kiongozi huyo amelala Rumande jana na leo anahamishiwa makao makuu ya Jeshi hilo Mkoani Kigoma.

Mosena Nyambabe ni mkuu wa Msafara wa viongozi wa UKAWA ambao wako Kigoma kuzungumza na wananchi.

Mkoa wa Kigoma ni moja ya Ngome Kuu za UKAWA huku chama cha NCCR kikiwa na jumla ya wabunge wanne mkoani humo.

Kukamatwa kwa Kiongozi huyo wa UKAWA ni baada ya mbinu mbalimbali na vitisho vya serikali dhidi ya UKAWA kushindwa kufua dafu.

CCM ilibuni mbinu nyingine ya kuwatumia mamluki kutoa taarifa za kupinga UKAWA kwenye vyombo vya habari lakini nayo mbinu hiyo imeshindwa.

Wakati akihutubia Zanzibar Mmoja wa viongozi wakuu wa UKAWA Maalim Seif Sharrif Hamad aliwataka viongozi wa UKAWA kujizatiti kwani zitatumika mbinu mbalimbali kuwatisha zikiwemo kuwakamata na kuwafungulia mashtaka.Lakini aliwaambia wasife moyo kwani ushindi utakuwa unakaribia.

Source:Mwananchi Breaking News
 
the ultimatum

JF-Expert Member
Dec 16, 2012
401
250
Ukombozi wa kweli unapitia katika shida, tusikate tamaa tuungane kwa pamoja tuikomboe nchi hii dhidi ya wakoloni CCM
 
hugochavez

JF-Expert Member
Mar 1, 2013
1,909
2,000
nalipongeza jeshi la polisi mkoani kigoma na wilaya husika kwa kazi nzuri ya kulinda amani ya nchi
 
hugochavez

JF-Expert Member
Mar 1, 2013
1,909
2,000
Jeshi la Polisi wilayani Uvinza mkoani Kigoma limemkamata Kiongozi wa UKAWA na Katibu Mkuu wa NCCR Mosena Nyambabe kwa kile wanachodai ni uchochezi.

Kiongozi huyo amelala Rumande jana na leo anahamishiwa makao makuu ya Jeshi hilo Mkoani Kigoma.

Mosena Nyambabe ni mkuu wa Msafara wa viongozi wa UKAWA ambao wako Kigoma kuzungumza na wananchi.

Mkoa wa Kigoma ni moja ya Ngome Kuu za UKAWA huku chama cha NCCR kikiwa na jumla ya wabunge wanne mkoani humo.

Kukamatwa kwa Kiongozi huyo wa UKAWA ni baada ya mbinu mbalimbali na vitisho vya serikali dhidi ya UKAWA kushindwa kufua dafu.

CCM ilibuni mbinu nyingine ya kuwatumia mamluki kutoa taarifa za kupinga UKAWA kwenye vyombo vya habari lakini nayo mbinu hiyo imeshindwa.

Wakati akihutubia Zanzibar Mmoja wa viongozi wa UKAWA Maalim Seif aliwataka viongozi wa UKAWA kujizatiti kwani zitatumika mbinu mbalimbali kuwatisha zikiwemo kuwakamata na kuwafungulia mashtaka.Lakini aliwaambia wasife moyo kwani ushindi utakuwa unakaribia.

Source:Mwananchi Breaking News

umeandika kishabiki mno....
 
hugochavez

JF-Expert Member
Mar 1, 2013
1,909
2,000
kwa kuwa ukawa/ukaua ni boko haram ya tz, na boko haram ni wauwaji...haipaswi kuhurumiwa hata kidogo
 
Mandla Jr.

JF-Expert Member
Dec 15, 2013
3,101
1,195
Molemo,
Hujaeleza sababu au kosa lililosababishwa na huyo kiongozi. Hebu tulia utueleze vizuri kafanya kosa gani?

Mandla.
 
Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,492
2,000
Molemo,
Hujaeleza sababu au kosa lililosababishwa na huyo kiongozi. Hebu tulia utueleze vizuri kafanya kosa gani?

Mandla.

Polisi wanadai ni uchochezi.

Kujua ni uchochezi gani mpaka asomewe mashtaka mahakamani.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom