Tatizo siyo kunywa katika Msiba,yeye alikunywa na kuwanunulia watu baada ya kusikia habari za msiba.sijasema kama ni kosa ila niimeuliza swali tu..
Wakati mwingine tusipokuwa makini tunaweza kujikuta tunatumiwa bila ya kujijua! Na hii itakuwa ni furaha kwa wale wanaotutumia.
Tujadili hili:
Kuhusu taarifa za kifo cha Wangwe; Kambi ya Upinzani ilianza kuzipata taarifa hizo majira ya saa 6 usiku. Je Mbowe alipewa taarifa hiyo usiku huo huo au la? Je wakati anapokea taarifa hiyo Mbowe alikuwa kwenye sehemu ya kinywaji (Pub/Bar) au la?
Maswali hayo hapo juu yakijibiwa kwa usahihi tunaweza kujadili.
Kuna mtu aliyehudhuria msiba wa Rodney Mutie Mengi? watakubaliana na mimi, suala la msiba na pombe ni kitu cha kawaida sana, na kama mfiwa ana uwezo ndie mwenye kugharamia hivyo vyote, kwa hiyo hili si jipya si hoja ya kujadiliwa, kuhusu Mbowe kununulia watu pombe!