Kiongozi wa NCCR adai Mbowe alinunua bia baada ya kusikia msiba!

Je kuna kosa kwa Mbowe kupiga kileo wakati chacha alipofariki

  • Total voters
    20
  • Poll closed .
Status
Not open for further replies.
Na unaposikia kiongozi wa juu wa upinzania kahamia CCM (mifano ipo) unashtuka vile vile?
Haijawahi kutokea kiongozi wa juu wa CCM akahamia Upinzani,labda awe ametumwa kujua wapinzani wanafanya nini.

As far as i know sijawahi kusikia katibu mwenezi wa CCM kahamia Upinzani?au wwew ulishasikia mwenyekiti wa CCM kahamia CHADEMA?sana sana utasikia yuko ndani ya kambi ya upinzani ndani ya CCM.

Swali bado lipo,Je hii ni chuki dhidi ya mbowe kutoka kwa wapinzani wenzake(hasa TLP ,CUF na NCCR?)na kwanini wanafanya hivi sasa hivi?
 
Alah! kumbe inasemekana na wala haijathibitishwa......

Nyani ngabu,

Mbowe mwenyewe alikiri kuwanunulia kiywaji.

Kevo,
Unataka tunyamaze kwa sababu linawahusu wao?

where we dare talk openly!
 
Tatizo siyo kunywa katika Msiba,yeye alikunywa na kuwanunulia watu baada ya kusikia habari za msiba.sijasema kama ni kosa ila niimeuliza swali tu..nina mpango wa kuandika makala kuhusu hili sababu limeonesha picha mbaya sana hasa kwa wapinzani wao kwa wao na limetolewa na kiongozi wa NCCR.there is something wrong somewhere...

Huyo mtu wa NCCR alikuwepo kwenye kikao hicho cha "Bia"? au na yeye aliambiwa. Binafsi sasa hivi madai kati ya NCCR, Chadema na TLP yanahusiana zaidi na Jimbo la Tarime kuliko kitu kingine chochote. Inawezekana kuwa ni kweli alinunua bia baada ya kusikia habari za msiba, lakini watu wanajuaje kuwa kununua bia hiyo kunahusiana na habari za msiba isipokuwa wanafanya inference ambayo haina msingi. Kwa maoni yako, reaction ya kwanza ya Mbowe ilitakiwa iwe vipi ili ikubalike kuwa ilikuwa ni reaction proper?

Jambo lingine ni kwamba Mheshimiwa alikataa kupewa mchango wa rambi rambi ambazo zilichangwa na wale wote waliokuwapo SA,akasema atawalipia akifika Dar kwa pesa zake na wao walikataa jambo hilo.

Gembe, una contacts za Mbowe, utafanya vizuri kumuuliza yeye mwenyewe ili akupatie maelezo ya hayo madai. Ni makosa makubwa kuamini maneno ya mtu wa pembeni kama hutapata nafasi ya kumuuliza mhusika. Ni yale yale ya Dr. Masau na madai ya Kuhani. Take time to grill him halafu uje utaumbie yeye anatoa maelezo gani?

Tayari IGP keshaandikiwa Barua alifanyie uchunguzi
Uchunguzi kwamba bia ilinunuliwa baada ya kupata habari za msiba, au uchunguzi kuwa inawezekana alikuwa anafurahia msiba wa Wangwe au uchunguzi wa kutaka kujua kwanini alionekana kana kwamba anafurahia msiba?

conncecting to the dot..unakumbuka James Mbatia alisema nini wakati akiongea na waandishi wa Habari?

Hata sikumbuki lakini najua NCCR wanalitaka Tarime kwa udi na uvumba; Nadhani Chadema wakubali kutosimamisha mgombea ili NCCR wasimamishe mgombea wao.
 
Nyani ngabu,

Mbowe mwenyewe alikiri kuwanunulia kiywaji.

Kevo,
Unataka tunyamaze kwa sababu linawahusu wao?

where we dare talk openly!

Wao akina nani?Speak out!
Kila mtu ana uwezo le kusema analotaka ila pale tunapopitiliza na kuongeza chumvi tunahatarisha na kuyagoroga maji then tunasema laiti tungejua?
 
Nyani ngabu,

Mbowe mwenyewe alikiri kuwanunulia kiywaji.

Kevo,
Unataka tunyamaze kwa sababu linawahusu wao?

where we dare talk openly!
Kwa kuwa yeye ndio alikuwa kama "mfiwa" ilifaa akarimiwe badala yake akakataa akazungusha round mwenyewe.....uliona wapi mwenye kilio anazungusha round na kugonga cheers wakati wa msiba?
 
Nyani ngabu,

Mbowe mwenyewe alikiri kuwanunulia kiywaji.

Kevo,
Unataka tunyamaze kwa sababu linawahusu wao?

where we dare talk openly!

Alikiri wapi? Una nukuu? Una video au audio ya kukiri kwake?

My sneaky suspicion tells me somebody is distorting something here.....
 
MKUU MKAMAP ,CHACHA amefariki nafikiri huu sio wakati mzuri kuongelea mijadala ya marehemu
Kuhusu hayo magazeti ,kwa sasa magazeti yote ya Tanzania habari zao haziaminiki hasa hao NEW HABARI wana beef na MBOWE nimejaribu kufuatilia Mtanzania na RAI tangu CHACHA kafariki heading kwenye frontpage lazima iilenge CHADEMA/MBOWE
 
Gembe umeoza unanuka ufisadi kama hao mafisadi wenzako waliokutuma kutuchanganya hapa JF ili tusiwabade mafisadi. wewe ni mufilisi... ni sawa na yule ibilisi aliyewashawishi Adam na Eva kula tunda. Kwani kununulia pombe watu ni kosa? wewe mbona unanunuliwa na mafisadi. Kama unayaandika haya ili udhoofishe vita ya kuwakomboa Watanzania masikini wanaonyanyasika kwa matokeo ya ufisadi na ulaanike! Damu ya watanzania wanaokufa kwa ajili ya huo ufisadi unaotetea na iwe juu yako na kizazi chako. Ikulilie popote uendako. Utangetange kama yule ibilisi aliyelaaniwa!!!
 
.....HAYA MAGAZETI YAMEAMUA KUKUZA HIZI HABARI KWA FAIDA WANAYOIJUA...NDIO MAANA UKIANGALIA HII HABARI IMETOKA KWA SIKU MOJA...NA KWA MAUDHUI YALEYALE ...TENA UKURASA WA MBELE..KWENYE MAGAZETI MAWILI YA MZALENDO NA MTANZANIA.....mwandishi NI "mwandishi wetu"

sasa hata kama ni kweli walikunywa pombe....mantiki ya hii habari kutoandikwa siku zote ije itolewe leo wiki tatu tangu azikwe...inaelekea ni aina ya CHARACTER ASSASINATION STRATEGY ...iliyoandaliwa kwa ajili ya CHADEMA...

..KWANZA LABDA WATU HAWAJUI BAADHI YA UTAMADUNI WA MAKABILA ....KWA MCHAGGA YEYOTE AKISIKIA MSIBA ANAJUA KUNA POMBE ..TENA NYINGI KULINGANA NA UZITO WA MTU...MCHAGGA AKIPATA TAARIFA NZITO AU MSIBA AU HATA FURAHA ..JAMBO LA KWANZA NI POMBE....SASA KAMA POMBE ALINUNUA POMBE ...NAFIKIRI NI UTAMADUNI TU......ANGEKUWA MNGONI ...ANGEKUNYWA NA KUIMBA ...SIJUI WANGESEMAJE...MAANA MNGONI AMEENDA MBALI ZAIDI YA MCHAGGA ..YEYE AKISIKIA MSIBA AU SHEREHE ..MAANA YAKE NI KUNYWA NA KUIMBA...

....NI MUHIMU KUTOTAFSIRI BAADHI YA MILA NA MAZOEA YA MAKABILA YETU VIBAYA..

..KWA MTANZANIA YEYOTE AMBAYE AMESHAWAHI KUSAFIRISHA MSIBA WA MCHAGGA TOKA DAR...MKIFIKA PALE KOROGWE [MOMBO]..MISIBA YOTE HUSUBIRIANA PALE....BASI HUTAAMINI KUWA WATU WAMEFIWA ....KUANZIA MFIWA HADI ...JAMAA WOTE WANAKUWA WANAKUNYWA POMBE KWA KUNUNULIANA..NA NYAMA ...HADI MUDA WA KUONDOKA..MISIBA HUKAA MOMBO HADI MASAAA MATATU....WAKITOKA PALE GARI ZIMA NI WALEVI....HAKUNA KULIA TENA HADI WANAFIKA ALFAJIRI....NADHANI MWANDISHI WA HABARI HIYO ....AKIONA HIYO HALI ATASEMA ..WACHAGGA HUWA WANASHEHEREKIA VIFO....LAKINI NI TABIA ZAO TU...MTU KUHUZUNIKA SIO LAZIMA UPIGE MAKELELE NA KUJIGALAGAZA NA KUSUSA KULA...KWANI HATA WACHAWI NA WANAFIKI NDIO WANAAOONGOZA KWA KULIA MISIBANI!!!!
 
Gembe, una contacts za Mbowe, utafanya vizuri kumuuliza yeye mwenyewe ili akupatie maelezo ya hayo madai. Ni makosa makubwa kuamini maneno ya mtu wa pembeni kama hutapata nafasi ya kumuuliza mhusika. Ni yale yale ya Dr. Masau na madai ya Kuhani. Take time to grill him halafu uje utaumbie yeye anatoa maelezo gani?

Mzee Mwanakijiji,

Nitamuuliza sana kuhsu hili na muda si mrefu tutajua,Je ni vibaya kuamini yale unayosoma katika magazeti?kama Lula wa Ndali mwananzela akiandika kwamba Rais wetu hana uwezo kwa kuamua mambo na anategemea sana mawazo ya kina RA na wanamtandao,na kwa kuwa kuwa lulakaandika kwasababu anamfahamu rais, je nimpinge kwa yale aliyoniambia?au hatuamini kile wanachosema wengine?Mie nadhani tuwe tunakubali yale yaliyokubaliwa na wenyewe..Mbowe mwenyewe alikubali kwamba alinunua Pombe,Mkuki mchungu..!

Hata sikumbuki lakini najua NCCR wanalitaka Tarime kwa udi na uvumba; Nadhani Chadema wakubali kutosimamisha mgombea ili NCCR wasimamishe mgombea wao.

Ni kweli NCCR wanalitaka jimbo kama ulivyosema,ila si hawa walikuwa katika muungano wa pamoja na CHADEMA?au ulishakwisha..naomba kupata hadidu rejea za muungano wao
 
Kwa sababu kwangu mimi ningependa kusikia maneno aliyoyasema wakati anakunywa kwa mfano "Cheers he is dead" au "Phew, tunamshukuru Mungu kwa kifo cha Wangwe" halafu akagongesha gilasi. Alisema neno lolote kuashiria alikuwa anafurahia kifo cha Wangwe hadi akanunua ulabu?
 
.....HAYA MAGAZETI YAMEAMUA KUKUZA HIZI HABARI KWA FAIDA WANAYOIJUA...NDIO MAANA UKIANGALIA HII HABARI IMETOKA KWA SIKU MOJA...NA KWA MAUDHUI YALEYALE ...TENA UKURASA WA MBELE..KWENYE MAGAZETI MAWILI YA MZALENDO NA MTANZANIA.....mwandishi NI "mwandishi wetu"

sasa hata kama ni kweli walikunywa pombe....mantiki ya hii habari kutoandikwa siku zote ije itolewe leo wiki tatu tangu azikwe...inaelekea ni aina ya CHARACTER ASSASINATION STRATEGY ...iliyoandaliwa kwa ajili ya CHADEMA...

..KWANZA LABDA WATU HAWAJUI BAADHI YA UTAMADUNI WA MAKABILA ....KWA MCHAGGA YEYOTE AKISIKIA MSIBA ANAJUA KUNA POMBE ..TENA NYINGI KULINGANA NA UZITO WA MTU...MCHAGGA AKIPATA TAARIFA NZITO AU MSIBA AU HATA FURAHA ..JAMBO LA KWANZA NI POMBE....SASA KAMA POMBE ALINUNUA POMBE ...NAFIKIRI NI UTAMADUNI TU......ANGEKUWA MNGONI ...ANGEKUNYWA NA KUIMBA ...SIJUI WANGESEMAJE...MAANA MNGONI AMEENDA MBALI ZAIDI YA MCHAGGA ..YEYE AKISIKIA MSIBA AU SHEREHE ..MAANA YAKE NI KUNYWA NA KUIMBA...

....NI MUHIMU KUTOTAFSIRI BAADHI YA MILA NA MAZOEA YA MAKABILA YETU VIBAYA..

..KWA MTANZANIA YEYOTE AMBAYE AMESHAWAHI KUSAFIRISHA MSIBA WA MCHAGGA TOKA DAR...MKIFIKA PALE KOROGWE [MOMBO]..MISIBA YOTE HUSUBIRIANA PALE....BASI HUTAAMINI KUWA WATU WAMEFIWA ....KUANZIA MFIWA HADI ...JAMAA WOTE WANAKUWA WANAKUNYWA POMBE KWA KUNUNULIANA..NA NYAMA ...HADI MUDA WA KUONDOKA..MISIBA HUKAA MOMBO HADI MASAAA MATATU....WAKITOKA PALE GARI ZIMA NI WALEVI....HAKUNA KULIA TENA HADI WANAFIKA ALFAJIRI....NADHANI MWANDISHI WA HABARI HIYO ....AKIONA HIYO HALI ATASEMA ..WACHAGGA HUWA WANASHEHEREKIA VIFO....LAKINI NI TABIA ZAO TU...MTU KUHUZUNIKA SIO LAZIMA UPIGE MAKELELE NA KUJIGALAGAZA NA KUSUSA KULA...KWANI HATA WACHAWI NA WANAFIKI NDIO WANAAOONGOZA KWA KULIA MISIBANI!!!!

Nakubaliana na wewe kabisa tena huwa wanaweka mishale ya majivu kuonyeshea ni wapi penye pombe!Basi hata wale wanaolia kwa kupiga vigelegele tuanze kusema nao huwa wanashangilia!
Hapa sishabikii ni njia gani tunatumia kuhuzunika kwenye misiba hapa ni why now when everything has just settled?
Siyo yaleyale ya kupitisha vibahasha vinono kwa editors ili wamchafulie mtu jina?
Something is fishy and it is very fishy and shady indeed!
 
Gembe umeoza unanuka ufisadi kama hao mafisadi wenzako waliokutuma kutuchanganya hapa JF ili tusiwabade mafisadi. wewe ni mufilisi... ni sawa na yule ibilisi aliyewashawishi Adam na Eva kula tunda. Kwani kununulia pombe watu ni kosa? wewe mbona unanunuliwa na mafisadi. Kama unayaandika haya ili udhoofishe vita ya kuwakomboa Watanzania masikini wanaonyanyasika kwa matokeo ya ufisadi na ulaanike! Damu ya watanzania wanaokufa kwa ajili ya huo ufisadi unaotetea na iwe juu yako na kizazi chako. Ikulilie popote uendako. Utangetange kama yule ibilisi aliyelaaniwa!!!
Huu sio ujengaji wa hoja....natumaini umeonywa......
 
Mzee Mwanakijiji,

Nitamuuliza sana kuhsu hili na muda si mrefu tutajua,Je ni vibaya kuamini yale unayosoma katika magazeti?kama Lula wa Ndali mwananzela akiandika kwamba Rais wetu hana uwezo kwa kuamua mambo na anategemea sana mawazo ya kina RA na wanamtandao,na kwa kuwa kuwa lulakaandika kwasababu anamfahamu rais, je nimpinge kwa yale aliyoniambia?au hatuamini kile wanachosema wengine?Mie nadhani tuwe tunakubali yale yaliyokubaliwa na wenyewe..Mbowe mwenyewe alikubali kwamba alinunua Pombe,Mkuki mchungu..!

Gembe, kama mtu kanunua pombe that is a fact akatae itasaidia nini? Swali ambalo ungeliweka vizuri ni kama alikubali kwa kununua pombe alikuwa anafurahia kifo cha Wangwe, alikubali hilo?

Ni kweli NCCR wanalitaka jimbo kama ulivyosema,ila si hawa walikuwa katika muungano wa pamoja na CHADEMA?au ulishakwisha..naomba kupata hadidu rejea za muungano wao

Hakukuwa na muungano kama unavyojua kwa sababu Katiba hairuhusu vyama kuungana, ulikuwa ni ushirikiano tu. Nadhani unaweza kuwauliza kati yao makubaliano yao ya ushirikiano yalikuwa na kina cha namna gani.
 
Kwa sababu kwangu mimi ningependa kusikia maneno aliyoyasema wakati anakunywa kwa mfano "Cheers he is dead" au "Phew, tunamshukuru Mungu kwa kifo cha Wangwe" halafu akagongesha gilasi. Alisema neno lolote kuashiria alikuwa anafurahia kifo cha Wangwe hadi akanunua ulabu?

Spoken like a true "law and order" citizen.Thank you for pointing that out.
 
Gembe umeoza unanuka ufisadi kama hao mafisadi wenzako waliokutuma kutuchanganya hapa JF ili tusiwabade mafisadi. wewe ni mufilisi... ni sawa na yule ibilisi aliyewashawishi Adam na Eva kula tunda. Kwani kununulia pombe watu ni kosa? wewe mbona unanunuliwa na mafisadi. Kama unayaandika haya ili udhoofishe vita ya kuwakomboa Watanzania masikini wanaonyanyasika kwa matokeo ya ufisadi na ulaanike! Damu ya watanzania wanaokufa kwa ajili ya huo ufisadi unaotetea na iwe juu yako na kizazi chako. Ikulilie popote uendako. Utangetange kama yule ibilisi aliyelaaniwa!!!

Laana inatolewa na Mwenyezi Mungu na kamwe binadamu hana uwezo wa kutoa laana hiyo.Unataka kila jambo linalomhusu Mwenyekiti lisiandikwe?kama ni kweli?hii habari imeandika na magazeti ya New Habari corp ila aliyeleta habari ni kiongozi wa NCCR na yeye ndiyo aliyasema haya.

Sina Mpango wa kudhohofisha vita dhidi ya ukombozi wa watanzania,na nashangaa sana kunipa uwezo ambao sina na sijafikia huko na kama nimefikia huko naomba mungu anisaidie sana nisifike kujipa uwezo wa kimungu

Jana Mkapa keshasema,tuache kupiga domo,kama unaweza kujikomboa kwa kujituma fanya hivyo tu,Nchi hii imekuwapo bila Mafisadi miaka ya Nyuma ila hatujaona maendeleo yote makubwa,angalia kuna kijiji kimoja huko lindi hakina shule toka 1974.Tatizo ni kwamba watanzania hatutaki kufanya kazi na tunapenda mambo yaje kirahisi.

Mie siyo ibilisi na kamwe nitasimama kutetea yale yaliyo sahihi na ya muhimu kwa watanzania wote.Wapinzani walishakosea sana muda mrefu san na niliwaonya sana.nilisema Ole mara sita na sasa hawahitaji msaada zaidi ya kuconfess na tuanze upya kupigania haki.

Kwa sasa mie nimejitolea kuwafunda wapinzani
 
Last edited:
Mzee Mwanakijiji,

kama Lula wa Ndali mwananzela akiandika kwamba Rais wetu hana uwezo kwa kuamua mambo na anategemea sana mawazo ya kina RA na wanamtandao,na kwa kuwa kuwa lulakaandika kwasababu anamfahamu rais, je nimpinge kwa yale aliyoniambia?

Gembe, Lula akiandika kuwa Rais Kikwete alipokuwa Iringa alionekana kupewa bahasha kubwa na wananchi wa kijiji kimoja. Katika bahasha hisho inadaiwa kulikuwa na rushwa ya shilingi milioni tano ili awasaidia kupata upendeleo wa aina fulani.

a. Kupokea bahashha itakuwa ni fact
b. Kudai bahasha ni rushwa itakuwa ni speculation ambayo iwe na msingi.

Unachosema ni kuwa :

a. Mbowe alinunua Pombe baada ya habari za msiba (hiyo ni fact)
b. Kama ni furaha ya msiba hilo ni debatable.

Unaoneaje?
 
Mkuu Mwanakijiji,

Uhalisia wa habari ya lula hapo juu ni madai,hivyo yanahitaji uchunguzi tu na madai yanaweza kuwa ya uongo.

Kuhusu Mbowe,Yeye mwenyewe alikiri kuwanunulia Raundi moja.Suala ambalo nakubaliana na wewe ambalo pia ni debatable ni kuwa "Mkuu alifanya vile kama ni furaha au la?"
 
Mkuu Mwanakijiji,

Uhalisia wa habari ya lula hapo juu ni madai,hivyo yanahitaji uchunguzi tu na madai yanaweza kuwa ya uongo.

Kwenye mfano wa Lula ni kuwa anaripoti fact kuwa Rais alipewa bahasha. Siyo madai kuwa alipewa bahasha. Anapoongeza tafsiri kuwa bahasha hiyo ilikuwa ni rushwa bapo ndipo madai yanapokuja. Na Rais angeulizwa kama aliipokea bahasha asingeweza kukataa.

Kuhusu Mbowe,Yeye mwenyewe alikiri kuwanunulia Raundi moja.
Lakini bado hujasema kama alivyokiri kuwa aliwanunulia raundi moja alifanya hivyo kwa sababu ya kufurahia kifo cha Wangwe. Je hivyo ndivyo alivyokiri?

Kama jibu ni hapana, basi hoja ya yeye kununua raudi moja ya bia siyo hoja tena kwa sababu mtu anaripoti kitu ambacho ni factual.

Suala ambalo nakubaliana na wewe ambalo pia ni debatable ni kuwa "Mkuu alifanya vile kama ni furaha au la?"

Nadhani katika thread hii ulitaka kuonesha kuna uhusiano kati ya kifo cha Wangwe na kununuliwa kwa Bia na Mbowe. Ulitaka watu wahusishe taarifa za kununuliwa bia na Mbowe kupokea habari za msiba, na kuhusishwa huko kungekuwa kwa aina ya Mbowe kufurrahia kifo cha Wangwe. Siyo?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom