Kiongozi wa NCCR adai Mbowe alinunua bia baada ya kusikia msiba! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kiongozi wa NCCR adai Mbowe alinunua bia baada ya kusikia msiba!

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Gembe, Aug 18, 2008.

?

Je kuna kosa kwa Mbowe kupiga kileo wakati chacha alipofariki

Poll closed Sep 1, 2008.
 1. Mbowe alikuwa rafiki mkubwa wa Chacha

  20.0%
 2. Mbowe alikuwa sawa kufanya hivi

  80.0%
Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #1
  Aug 18, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Heshima Mbele,

  Habari ambazo zilipamba mageti ya Nyumbani siku ya Jumapili yaliandika Habari kwamba Mhe. Mbowe aliwanunulia Baadhi ya watu raundi ya kinywaji alipokuwa Afrika Kusini na alionekana mchangamfu sana,na alionekana kutoshtushwa na habari za kifo cha Marehemu wangwe.

  Nimeona ni vyema tujadili hili,Je ni kosa la Mbowe na linaweza kuwa na Madhara gani hasa kwa chama chake?Inasemekana kuna mmoja wa kiongozi wa kambi ya upinzani alishmwandikia IGP kuhsu hili na kuomba uchunguzi ufanyike.
   
  Last edited by a moderator: Aug 18, 2008
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  Aug 18, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160

  Mzee Gembe,

  Heshima yako mkuu, mzee tupe source za habari hii ama unaendeleza conspiracy theories, wewe unafikiri hii inasidia nini? ama wataka mjengea Mh Mbowe chuki kwa jamii? watanzania kunapokuwa na msiba tofauti zetu huwa tunaziweka kando sasa mkuu hapa sikuelewi....ama kweli JF kuna vioja wakati mwingine. MoD iwekeni hii mahali pake kulee kwenye vioja/jokes

  Ushi
   
 3. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #3
  Aug 18, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Ukitafuta magazeti ya jana utaipata hiyo,Nimeambiwa ni magazeti ya Mtanzania,Habari leo na majira.ngoja nicheki then nitaweka hapa.

  Ushirombo,hakuna kioja sababu hata Mhe. Mbowe amekubaliana na hilo na kusema yeye alinunua raundi moja tu,aftera ll hii inasaidia na wala siyo kwa kujenga chuki na Mhe. Mbowe ila malipo ni hapa duniani
   
 4. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #4
  Aug 18, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo utaka kusema Ndugu Mbowe alifurahia kifo cha Wangwe?
   
 5. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #5
  Aug 18, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Kazi ipo magazeti hayo nimeyasoma yapo online, wakati mwingine waandishi wetu nao ni kituko kama baadhi wa wanaJF
   
 6. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #6
  Aug 18, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mimi kama Mtanzania huru kwenye nchi huru nahisi huu ni upandikaji wa chuki wenye maslahi binafsi kwa watu wachache wenye yao mambo!
   
 7. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #7
  Aug 18, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  wewe una maoni gani? je ni sahihi kutoa round za kinywaji na kufurahia kifo hicho au sio sahihi?
   
 8. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #8
  Aug 18, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mzee nimekusoma na kukuelewa, nadhani ni ufisadi wa fikra kwa manufaa ya wachache kabisa....sidhani kama Mtukufu Gembe na wenzake watalikwepa hili....na sijui wanafanya hili kwa manufaa ya nani...
   
 9. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #9
  Aug 18, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  kivipi mkuu?....kama alifanya hivyo kuna upandkizaji upi?
   
 10. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #10
  Aug 18, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Hivi unafikiri ni nani alianza kupandikiza chuki,watu huwa tunasahau mapema na hii inaonesha jinsi malipo ni hapa duniani,utakumbuka wakati Mbowe alipokuwa akimpinga chacha Wangwe..aliona sawa?

  kitu ambacho kimenishtua ni kwamba hili jambo limesemwa na Kiongozi wa Upinzani.sasa sijui katumwa na CCM au?
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  Aug 18, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  hivi majuzi tulikuwa kwenye msiba wa ndugu yetu mwingine hapa US, na wabongo walipokutana pamoja na kuwepo msibani walileta vinywaji vya bia kwa wingi tu; sikujua walikuwa wanafurahia kifo cha huyo ndugu yetu. Tena nimeona hili mara nyingi tu. Sijui nchi nyingine kama wabongo wanaleta vinywaji msibani tena hata kabla ya marehemu hajazikwa.

  Kama ndiyo hivyo (kusherehekea kifo cha mtu) basi ni kweli Mbowe amekosea na siyo yeye tu bali watanzania wengi wanaoleta ulabu misibani.
   
 12. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #12
  Aug 18, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Siwezi kutoa maoni hapo maana sikuwepo na siamini kama mh alitoa round.
   
 13. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #13
  Aug 18, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Kwa mtazamo wangu mimi kinachosherehekewa si kifo bali ni hayo maisha aliyoishi marehemu....but I could be wrong...dunno...
   
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  Aug 18, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280


  Mzee kumpinga mtu siyo hoja, mimi nilimpinga Wangwe tena hadharani na wala sijutii hilo kwa sababu kumpinga kwangu kulitokana na kutofautiana kwa hoja na siyo chuki. Na nilimheshimu na wakati wa mahojiano yetu kuna vitu ambavyo nilimuambia na yeye aliniambia na ninavifanyia kazi. Na nilimuambia kuhusu kitu hicho namuunga mkono. Kutofautiana na wanasiasa ni sehemu ya siasa. Kwa hiyo kumpinga mwanasiasa haina maana ni chuki. Unless unataka kusema tofauti zao ni za kibinafsi zaidi kitu ambacho kinaweza kuwa hoja.

  Kama ni ukweli alinunua unywaji halihitaji kutumwa au kutotumwa ni kustate facts. Tatizo linakuja tunapoweka tafsiri zetu kwenye kitendo hicho. Kudai kuwa mtu hakuonekana kushtushwa sijui mtu anaona vipi, alihitaji kupiga mayowe na kujigalagaza chini (si angeitwa mnafiki). Angejifanya anahuzunika na kusikitika sana (bado angeonekana mnafiki); sijui reaction gani angekuwa nayo ambayo isingeleta maneno mengine. Kuna vitu ambavyo binafsi nimeguswa navyo na nimemuangikia Mbowe mwenyewe na uongozi wa Chadema na wanajua tunatofautiana katika hilo.

  Siyo kila tofauti hata iwe kali namna gani ina maana ni ugomvi.
   
 15. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #15
  Aug 18, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Tatizo siyo kunywa katika Msiba,yeye alikunywa na kuwanunulia watu baada ya kusikia habari za msiba.sijasema kama ni kosa ila niimeuliza swali tu..nina mpango wa kuandika makala kuhusu hili sababu limeonesha picha mbaya sana hasa kwa wapinzani wao kwa wao na limetolewa na kiongozi wa NCCR.there is something wrong somewhere...

  Jambo lingine ni kwamba Mheshimiwa alikataa kupewa mchango wa rambi rambi ambazo zilichangwa na wale wote waliokuwapo SA,akasema atawalipia akifika Dar kwa pesa zake na wao walikataa jambo hilo.

  Tayari IGP keshaandikiwa Barua alifanyie uchunguzi

  conncecting to the dot..unakumbuka James Mbatia alisema nini wakati akiongea na waandishi wa Habari?


   
 16. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #16
  Aug 18, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Ni kweli misiba mingi vinywaji vinaletwa.....lakini hii ya Ndugu Mbowe inasemekana alikuwa kama anashangilia hivi...cheers nyingi kwa kifupi tofauti na mfano uliotolea hapo juu....
   
 17. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #17
  Aug 18, 2008
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,718
  Likes Received: 1,211
  Trophy Points: 280
  Na unaposikia kiongozi wa juu wa upinzania kahamia CCM (mifano ipo) unashtuka vile vile?
   
 18. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #18
  Aug 18, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Mzee Mwanakijiji,

  una uhakika Mhe . Mbowe alimpenda sana Marehemu chacha?kama ni hivyo asingeweza kushiriki katika vikao vya kumsimamisha Wangwe.Mie naweza kusema kuna mambo mawili ambayo yanaharibu vyama vya upinzani na watu wameshindwa kujifunza ,ukianzia kipindi cha Mrema wakati yuko NCCR then akahamia TLP.

  1.Ruzuku
  2.Madaraka(yanachangiwa na ukabila,kujuana)

  vyama vimekuwa vinaacha katiba zao katika kujiendesha na kutegemea mawazo ya watu binafsi.Kimsingi mpaka sasa umoja wa upinzani umeshavunjika sababu kila mtu anajiona yuko bora kuliko mwenzake
   
 19. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #19
  Aug 18, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hata kama alitoa ili nini?Do we have to bring this topic up when everything had settled?Ama ndio hao Watarime waanze upya hasira zao zidi ya Wachagga?hata kama limesemwa na kiongozi wa Upinzania kwani wangesema CCM lisingeleta huge impacts kwenye society?
   
 20. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #20
  Aug 18, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Alah! kumbe inasemekana na wala haijathibitishwa......
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...