Kiongozi wa mhimili wa makahama awe kwenye kamati kuu ya chadema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kiongozi wa mhimili wa makahama awe kwenye kamati kuu ya chadema

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kamakabuzi, Aug 27, 2009.

 1. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #1
  Aug 27, 2009
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,497
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Kwa kuwa katiba ya nchi hii inatambua kuwepo kwa mihimili mitatu ya dola, yaani serikali, Bunge , na Mahakama, na kwa kuwa mihimili hii mitatu inapaswa kufanya kazi bila kuingiliana ila kuchungana, na kwa kuwa kiongozi wa mhimili wa serikali ni Rais, na kiongozi wa mhimili wa Bunge ni Spika, ambao wote ni viongozi wa CCM ngazi ya juu (ina maana tayari mihimili hii miwili imeshaingiliana), naleta hoja kuwa ili mhimili wa tatu (mahakama) usivutwe kuingiliana na hii miwili basi kiongozi wake ajiunge na Chama cha upinzani na epewe nafasi ya kuwa kiongozi katika ngazi za juu.
  This will ensure checks and balances of the system.

  Vinginevyo, kwa kuwa kiongozi wa mhimili wa serikali lazima awe kwenye chama cha siasa huyo aendelee kuwa kiongozi katika chama, ila kwa kuwa kiongozi wa mhimili wa Bunge si lazima awe mwanachama wa chama chochote cha siasa, sawa na ilivyo kwa kiongozi wa mhimili wa Mahakama, naleta hoja kuwa mtu yeyote akisha chaguliwa kuwa spika basi ajivue uanachama wa chama cha siasa na nyadhifa zote za kisiasa ili aweze kuongoza vizuri bunge ambalo ni la wananchi wote; vivyo hivyo kiongozi wa mhimili wa mahakama asiwe mwanachama wa chama chochotecha siasa.

  Nawasilisha
   
  Last edited: Aug 28, 2009
 2. C

  Chuma JF-Expert Member

  #2
  Aug 28, 2009
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  sasa awe Chadema au...Chama chochote cha siasa...nimeelewa tu kiujumla lkn flow ya habari hakuna..!!!
   
 3. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #3
  Aug 28, 2009
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Habari yenyewe ilikuwa inaleta maana kidogo lakini heading ni ina tatizo kidogo. Kwani lazima awe CHADEMA tu? Kuna vyama vingine vya upinzani vilevile
   
 4. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #4
  Aug 28, 2009
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,497
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  unataka flow ya aina gani? Hii flow imewekwa katika mfumo wa "logical statements" Ni vizuri ukaonyesha wapi flow haipo ili tusahihishe.
  Ila kwa kuwa umeelewa kiujumla, basi tunaomba maoni yako ya kiujumla, yaani wewe unaonaje suala la viongozi wa mihimili miwili kuwa viongozi wa CCM na huyu wa mhimili wa tatu awe chama cha upinzani? Au unaonaje viongozi wa Bunge, na Mahakama wasiwe viongozi wa vyama vya siasa? This is the main issue presented for discussion!
   
 5. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #5
  Aug 28, 2009
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,497
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Nafurahi kuwa habari inaleta maana japo unasema kidogo. Heading imewekwa maksudi kutaja Chadema kwani kwa wengi kinaonekana kuwa ndicho chama mbadala wa CCM, ila katika ufafanuzi ndani ya habari yenyewe nimeeleza kuwa awe chama chochote cha upinzani.
  La msingi tujadili the main issue ambayo ni mgongano wa maslahi (conflict of interest) pale kiongozi wa mhimili wa Bunge anapokuwa kiongozi wa Chama cha sisasa na hivyo kulazimika kuilinda serikali ya chama chake badala ya maslahi ya wananchi wote wakiwakilishwa na wabunge?. Je kiongozi wa mhimili wa tatu akiwa wa chama cha upinzani itasaidia kuleta checks and balances za mihimili hii mitatu kama inavyotakiwa ndani ya katiba? Au viongozi wa mihimili miwili (bunge na mahakama) wasiwe viongozi wa kisiasa?
   
Loading...