Kiongozi wa Mbio za Mwenge anapotoa Amri

kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,739
4,732
Hii imekaaje wandudu, Nimeshuhudia kupitia Taarifa TBC 1 kiongozi wa Mbio za mwenge akitoa amri kwa Mhandisi huko singida kurekebisha mara moja ujenzi uliofanyika ambao umefanyika kwa kiwango cha chini la sivyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

My Take
Hivi nchi hii hakuna mpaka ya kiuongozi na kila mtu anaruhusiwa kutoa amri? tumeshuhudia NAPE akitoa amri ambazo kwa mtazamo wangu ni kazi za mawaziri husika.
 
Hata wewe ukiona muandisi kabolonga mwambie kama kweli una penda maendeleo ya nchi yako
-mfate mwambie kiustarabu -
Ikishindikana nenda kwa wahusika wape taarifa au mpigie simu moja moja jembe Magufuli

Jamani hii nchi haitajengwa na serikali bila ushirikiano wetu.Vinginevyo tuwe na makasumba yetu
 
Hii imekaaje wandudu, Nimeshuhudia kupitia Taarifa TBC 1 kiongozi wa Mbio za mwenge akitoa amri kwa Mhandisi huko singida kurekebisha mara moja ujenzi uliofanyika ambao umefanyika kwa kiwango cha chini la sivyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.
Asiporekebisha atamfanya nini?
 
Ni mkuu wa wilaya mtarajiwa kama akina jordan rugimbana ndo tuzo atakayopewa
 
Chanzo cha yote ni siri za EPA na Richmond + Meremeta. Kila mtu anajua chanjo so hakuna wa kumnyooshea mwenzie kidole wote level moja.

Usishangae hata shigela siku hizi anatoa maagizo.
 
anaipenda nchi yake sasa hapo kuna kosa gani? Kwani akinyamaza anayetumia hizo bara bara ni nani kama sio wewe?
 
hii imekaaje wandudu, nimeshuhudia kupitia taarifa tbc 1 kiongozi wa mbio za mwenge akitoa amri kwa mhandisi huko singida kurekebisha mara moja ujenzi uliofanyika ambao umefanyika kwa kiwango cha chini la sivyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

My take
hivi nchi hii hakuna mpaka ya kiuongozi na kila mtu anaruhusiwa kutoa amri? Tumeshuhudia nape akitoa amri ambazo kwa mtazamo wangu ni kazi za mawaziri husika.

we kibogo?!!!!!! We nae kazi kuongezea maneno tu. Ni kweli kiongozi wa mwenge ameongea juu ya jengo hilo lililokuwa na ufa ndani ambazo nyufa ni za plasters ( sio ukuta wote ) tena ziko kwa ndani. Ila alimshauri mhandisi awe karibu na wajenzi. Lakini alipotoka kwenye public hakugomba maana lilishaeleweka. Usipende kuweka maneno hasi kwa kila linenwalo
 
Halafu yule ni kepteni. Hivi ni kepteni wa jeshi au wa boti? Maana mambo ya mwenge ni kisiasa na wajeshi hawaruhusiwi kujihusisha na mambo ya siasa.
 
we kibogo?!!!!!! We nae kazi kuongezea maneno tu. Ni kweli kiongozi wa mwenge ameongea juu ya jengo hilo lililokuwa na ufa ndani ambazo nyufa ni za plasters ( sio ukuta wote ) tena ziko kwa ndani. Ila alimshauri mhandisi awe karibu na wajenzi. Lakini alipotoka kwenye public hakugomba maana lilishaeleweka. Usipende kuweka maneno hasi kwa kila linenwalo

Nilichokiandika ndo nilichokisikia sijachakachua habari
 
Hii imekaaje wandudu, Nimeshuhudia kupitia Taarifa TBC 1 kiongozi wa Mbio za mwenge akitoa amri kwa Mhandisi huko singida kurekebisha mara moja ujenzi uliofanyika ambao umefanyika kwa kiwango cha chini la sivyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

My Take
Hivi nchi hii hakuna mpaka ya kiuongozi na kila mtu anaruhusiwa kutoa amri? tumeshuhudia NAPE akitoa amri ambazo kwa mtazamo wangu ni kazi za mawaziri husika.

kila kiongozi anachokifanya au atakachokifanya ni lazima kiendane na sheria, kanuni na taratibu za nchi, kiongozi yeyote
akitoa amri yeyote ya ajabu muulize anatumia mamlaka gani ya kisheria,kanuni au utaratibu za nchi kusema hayo anayoyasema. mawaziri ktk semina zao za uongozi wanaambiwa lazima wazingatie vigezo hivyo nilivyovitaja.
 
anaipenda nchi yake sasa hapo kuna kosa gani? Kwani akinyamaza anayetumia hizo bara bara ni nani kama sio wewe?

Wote tunaipenda Tanzania,tatizo ninaloliona ni hizo amri alizotoa ni sahihi? na zisipotekelezwa anauwezo wa kumchukulia mtu hatua? au anajifuraisha na kuwafuraisha walio mteua kuwa kiongozi wa mbio za mwenge wa CCM.
 
Hii imekaaje wandudu, Nimeshuhudia kupitia Taarifa TBC 1 kiongozi wa Mbio za mwenge akitoa amri kwa Mhandisi huko singida kurekebisha mara moja ujenzi uliofanyika ambao umefanyika kwa kiwango cha chini la sivyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

My Take
Hivi nchi hii hakuna mpaka ya kiuongozi na kila mtu anaruhusiwa kutoa amri? tumeshuhudia NAPE akitoa amri ambazo kwa mtazamo wangu ni kazi za mawaziri husika.

confused leadership at its worst stage...the country heading to complete failed state
 
Back
Top Bottom