Kiongozi wa kisiasa unapolazimisha upendwe ni sehemu ya udikteta

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,445
Kiongozi wa kisiasa unapolazimisha upendwe ni sehemu ya udikteta. Kama mtu hakupendi mpe na nauli kabisa aondoke zake. Ama sivyo unaiua thamani yako wewe binafsi, ya chama na yule aliyekuumba. Na hata raha ya kutawala kwako itakosekana. Ukipendwa utaheshimiwa.

Usipoteze thamani ya muda na thamani yako kwa kujaribu kuhonga au kukenua meno ili upendwe na watu. Upendo huja wenyewe. Asiye na upendo kwako, achana naye au mpe nafasi akapende mahala pengine. Fanya kitu ambacho kitamfanya akuelewe na siyo kulazimisha.

Mwili ni kama taifa lenye kila aina ya madini ya thamani. Ukijichukulia poa unakaribisha wawekezaji wa hovyo. Ambao watakuchukulia kirahisi kwa kukuchimba wakuache kama handaki lenye popo. Kiongozi wa kisiasa huhitaji nguvu kubwa ili upendwe. Timiza ahadi zako upendwe mpaka ukereke.

Tatizo la madikteta duniani tangu na tangu ni kutaka kila mtu ampende. Huo ni wehu, anataka atazamwe vizuri, aongelewe kwa mema, ajadiliwe kwa kusifiwa na kila mtu. Mzee baba 'utadata' au itakuwa 'shotikati' ya kuukaribisha wendawazimu walioupata kina Bokassa nyakati zile.
Ukitaka raia akutukuze tenda kile ulichoahidi kumtendea. Nje ya hapo utatumia njia za wazi na gizani kunyamazisha watu. Na dawa ya raia ni ukweli, na ukweli uwe kwa pande zote mbili. Timiza ahadi yako kwao na wao watimize kwa kuungana nawe kwa kila ufanyalo. Mwisho huwa ni furaha tu.

Kuna vitu Mungu hapendi. Kama mja wake kukosa furaha ya maisha. Ni mpumbavu tu anayefuga maumivu ya hisia moyoni mwake. Kulazimisha, kubembeleza au kuhonga ili upendwe. Ni kosa linalostahili kuwa dhambi ya pekee.



Credit: Dk Levy

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Neno zuri ni kushurutisha kupendwa. Kibaya zaidi unakuta unashurutisha kupendwa huku ukiongoza chama cha kizazi kilichopita.
Ndio wapendavyo washurutisha kupendwa. Angalia furaha iliyo usoni inasema mengi
IMG_20200606_230906.jpg
 
Mimi ni mwana CCM damu sema toka magufuli awe Rais niliingiwa sijui na Roho gani ya kumchukia na CCM yake. Siku unavyoongezeka namchukia tu.

Baada ya Magu kuondoka CCM..hiki chama kitakuwa ma wakati mgumu sana endapo atakayepokea kijiti akijichanganya kuwa kama JK.
 
" Usitumie nguvu nyingi kusema nimefanya 1,2,3... acha endapo umefanya sahihi acha yaliyofanyika yajieleze yenyewe.,."Prof.P.L.U Lumumba
Naomba kuambatanisha
 
Back
Top Bottom