Farolito
JF-Expert Member
- Sep 10, 2018
- 11,634
- 26,370
Kiongozi mkuu wa kanisa la Pentecostal Power Ministry Nabii Eliya Mahela amesema hakubaliani na kile alichokifanya waziri Lugola cha Kumdhalilisha mchungaji wake pamoja na kumlazimisha kufungua kanisa kukanyaga madhabahu ya Mungu na watu wenye imani tofauti na kuifanya kama ukumbi wa wanahabari kwani kufanya hivyo ni makosa makubwa
Aidha amesema kulikuwa hakuna haja ya kumkamata mchungaji wake kwa namna aliyofanya badala yake angempa wito kufika ofisini kwake au ofisi ya usajili wa vyama vya kijamii.
Pia anashangaa kwanini viongozi wa Makanisa kama KKKT au RC na baadhi ya Masheikh wa Misikiti mikubwa hupewa
wito kufika ofisini panapokuwa na tatizo na sio kuwadhalilisha kama alivyofanya kanisani kwake,kwake anajua akifanya hivyo kwa makanisa hayo hawezi mziki wake.
Aidha amesema Wizara ya mambo ya ndani ndio inayoongoza kwa matatizo tangu kupata uhuru ambapo mawaziri hukaa kwa wastani wa miaka 2 na kuondolewa ambapo tangu Uhuru Wizara hio imekuwa na takribani Mawaziri 60 tofauti na Wizara zingine.
Mwisho ameahidi akirudi atafanya Press conference kuongelea suala hili mara atakaporudi kutoka Ughaibuni.
Zaidi sikiliza audio