Kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni

Hapo kinachoonyesha kuwa hajalirudisha ni nini? Hiyo picha ilipigwa kabla ya kulirudisha au baada? Common sense is not so common!
 
Nimeshawahi kusema mara chache na sitochoka kusema tena - Ushabiki tumeuweka mbele kiasi tunatumia nguvu kupinga hoja badala ya kutumia hoja zenye nguvu katika kutetea utawala, uongozi, dhamana na uwajibikaji; na kupinga ufisadi, ubadhirifu na kutowajibika.
Tumekuwa tukilinganisha mabaya yetu badala ya mema yetu, kiasi tumefika pahala kila linapokuja suala zito linalomgusa kiongozi yoyote wa chama tunaishia kurudia yale yale:
- wetu hawajibiki kidogo tu, wenu hawajabiki sana,
- wetu ni fisadi kidogo tu, wenu ni fisadi sana,
- wetu anatukana kidogo tu, wenu anatukana sana n.k.

Hoja ya magari ya gharama ilianza na mtoto wa mkulima aliposema atalirudisha, amelirudisha? Kutorudisha gari Pinda hakumhalalishii Mbowe kuling'ang'ania. Vivyo hivyo kwa hoja ya posho. Wengi wamepinga, wangapi wamezikataa? Wengine kutokataa posho, hakuwalalalishii wengine kuzipokea.

Hata hivyo, ikiwa mmoja tu atakataa posho au gari, huyu atakuwa anawapa kauli na hoja wananchi wanaoliliwa vyao. Awe Pinda awe Mbowe, kukubali gari la mamia ya mamilioni ya gari wakati wananchi wananchi wanapelekewa vibajaji vya kuuzia Ice cream kama magari ya kubebea wagonjwa huo ni usaliti kwa wananchi.

Kwenye siasa, heshima ya kiongozi yeyote ni kutumiza ahadi zake, awe wa chama tawala au cha upinzani. Mimi nisingemuoana Mbowe mbaya kwa sababu ni mpinzani wala nisingemuona Pinda ni mwema kwa sababu ni mtawala au kinyume cha yake - WOTE WANWASALITI WANANCHI KWA KAULI ZAO.
Kudos!!!
 
Tusijibu kishabiki tu kwa sababu tuna mapenzi na Chama husika. Jaribu kupima alichokizungumza na anachokitekeleza sasa. Ni vitu ambavyo haviwiani. Ni bora angekaa kimya aendelee tu kujifaidia V8 lake.
We rejao mkuki kwa nguruwe eeehhh!!!! Wewe mbona umeleta kishabiki???? Yakuume hayo ya viongozi wako wa ccm kwanza ndo tuone kama una uchungu na nchi. Na shida ni mfumo wenu ndo mbovu....
 
Na Zitto alivyokataa posho na mpaka sasa hapokei, kwanini hakuambiwa kuwa anavunja sheria?
Hapo bado naquestion umakini wa CDM mnaouzungumzia kila siku
Kamuulize kama hachukui za mashirika ya umma... Na saivi yuko marekani mwezi sasa muulize kama halipwi
 
Kigogo,
Naona akili yako imekataa kabisa kukubali kama Mbowe hajarudisha gari ya kiongozi wa kambi ya upinzani bungneni.

Wapinzani wanatekeleza sera za CCM, kwani hujui kuwa punde Mh Mbowe atatumia RAV 4 kama ilivyotangazwa hivi karibuni lakini panapo udhaifu lazima waseme.
 
Mkuu wangu Rejao mpenda amani, wanachosema Chadema kwenye majukwaa sio wanachokitekeleza.

Suala la gari ya kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni pamoja na posho ilikuwa ni mpango wa kuwavuta watu.

Chadema nzima ni mbunge moja tu ambaye kweli kakataa kuchukuwa posho ni Zitto Kabwe tu. Tindu Lissu, yeye anasema hataki posho lakini wanamuwekea kwenye account yake.

Chadema simamieni mnachokisema sio kuwadanganya wananchi.

Kunya anye kuku akinya bata......., mbona ahadi za mkuu wa kaya Kuleta meli ziwa Tanganyika na Nyasa hauziongelei? Acheni unafiki wa mchana kweupe.
 
Mkuu wangu Rejao mpenda amani, wanachosema Chadema kwenye majukwaa sio wanachokitekeleza.

Suala la gari ya kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni pamoja na posho ilikuwa ni mpango wa
PHP:
kuwavuta watu.

Chadema nzima ni mbunge moja tu ambaye kweli kakataa kuchukuwa posho ni Zitto Kabwe tu. Tindu Lissu, yeye anasema hataki posho lakini wanamuwekea kwenye account yake.

Chadema simamieni mnachokisema sio kuwadanganya wananchi.

Zile ahadi lukuki za JK majukwaani wakati wa kampeni mbona hazijatekelezwa? zilikuwa za kuwavutia wanyama wa porini?
 
Chamuhimu hapa siyo FIXED cost ambayo tayari imeshakuwa sunk cost ya kulinunulia hili gari. issue ipo kwenye maintainance, angekuwa amelikataa kama alivyosema, serikali ingekuwa imesave kiasi kikubwa sana cha fedha. Kuendelea kulitumia ni kuuongezea mzigo serikali.

ni kweli ni mzigo kwetu maana ni kodi zetu lakini kwa nini iwe mzigo kwa mbowe tu kutumia vx...hujaona kwa jk kuna ya aina ngapi .........benzi, bmw. nissani,vx yaani anaamua tu atumie nini au ndege huko kwako safii .

 
Chamuhimu hapa siyo FIXED cost ambayo tayari imeshakuwa sunk cost ya kulinunulia hili gari. issue ipo kwenye maintainance, angekuwa amelikataa kama alivyosema, serikali ingekuwa imesave kiasi kikubwa sana cha fedha. Kuendelea kulitumia ni kuuongezea mzigo serikali.
Angalia usivyojua mambo, aliyekwambia wakati halitumii lilikua limepark tu ni nani???? Magamba wako wakubwa wenye sisiem walikua wakilitumia
 
Lakini sioni wa kumnyooshea mwezake kidole kwa haya yote. Hao wanaojidai wanaweza kuibadili Tanzania na mfumo uliopo, ndio hao hao ambao hawawezi kusimamia wanayoyasema.
Asante kwa kuamua kuanika uongo wa baba mwanaasha na serikali yako hadharani, usicheze na wamwabuduo mungu kwa haki na kweli wewe!!!! Tulianza na mungu na tutamaliza na mungu
 
View attachment 54426
Kwa taarifa tulizonazo na wanachi wengi wanavyofahamu, tayari hili gari V8 limekwisharudishwa na Mh. Freeman Mbowe. Lakini cha kushangaza bado huyu mkuu analitumia.

Nashindwa kuwaelewa hawa CDM, kelele zote wanazopiga ni kutuhadaa tu wananchi? Kama kwa hili dogo huyu Mh. kashindwa kulitekeleza, je hayo anayoyahubiri kila siku majukwaani ataweza kuyatekeleza?

Hii inanifanya nikose imani na wapinzani, yapo mengi tu wanayoyazungumza mbayo ukijaribu kuyaangalia utekelezaji wake ni kitu kisichowezekana. Cha muhimu hawa viongozi wetu wasiwe ni watu wa kutudanganya ili kujipatia umaarufu. Kama ukiamua kufanya kitu, fanya kweli!!

Tujadili mambo ya msingi kama ugumu wa maisha, we unatuletea habari gani hii!!!!!!! gamba.
 
kama mbowe bado analitumia hilo gari tunayo haki ya kuhoji unless ameshalitolea ufafanuzi ambao mimi siujui,until then nitaona mbowe is preaching what he is not practising.
 
Mkuu ritz, Hicho ndicho kinachosababisha watu wengi wanaojua kuchambua mambo wakose imani na wapinzani.
Kama waliamua kukakataa kitu, wangebaki na msimamo wao huo huo.
BTW, CHADEMA ni kama gari bovu lisilo na uelekeo maalumu. hawana common goal, kila mtu anajiamulia anvyojua. Leo kiongozi wa BAVICHA atasema hivi, kesho makamu wake atasema hivi, Slaa naye atakuja na lake, Mbowe naye...

...Kinachosemwa ni ukweli hii picha ni ya juzi tu wakati mbowe anaenda clouds,sasa namshangaa anayesema eti picha ni ya lini,watu wengine wanashabikia vyama bila kukiri na hii ndo itaua hivi vyama pamaoja na chadema kujipatia wanachama wengi lakini watapoteza kula kwa huu udanganyifu,tatizo lao hawataki kuambiwa ukweli,mtu akisema ukweli wanamfukuza uanachama hii sio siasa kukweli, kwa sisi tunaojua kuchambua na kufuatilia hawatatupata na dola hatutawakabidhi kamwe
 
Mkuu
REJEO nimewahi kusoma mahali humu ndani kuwa hilo gari ni lake kama Mp na si KUB sijui na chochote hapo kwani nae anamkopo wa VX!
 
View attachment 54426
kwa taarifa tulizonazo na wanachi wengi wanavyofahamu, tayari hili gari v8 limekwisharudishwa na mh. Freeman mbowe. Lakini cha kushangaza bado huyu mkuu analitumia.

Nashindwa kuwaelewa hawa cdm, kelele zote wanazopiga ni kutuhadaa tu wananchi? Kama kwa hili dogo huyu mh. Kashindwa kulitekeleza, je hayo anayoyahubiri kila siku majukwaani ataweza kuyatekeleza?

Hii inanifanya nikose imani na wapinzani, yapo mengi tu wanayoyazungumza mbayo ukijaribu kuyaangalia utekelezaji wake ni kitu kisichowezekana. Cha muhimu hawa viongozi wetu wasiwe ni watu wa kutudanganya ili kujipatia umaarufu. Kama ukiamua kufanya kitu, fanya kweli!!

tusimlaumu sana mbowe. Alipokataa hili gari tu serikali ilisema anavunja sheria na taratibu za serikali. Kwa mujibu wa serikali kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni anastahili zake anazotakiwa kupewa na serikali, hizi ni pamoja na gari, nyumba, ofisi, ulinzi n.k. Kwa sababu hiyo kiongozi huyu hana haki ya kuchagua ni stahili inafaa kwani stahili hizo zipo kwa mujibu wa sheria na taratibu za kuendesha serikali. Kwenda kinyume na hapo ni kuvunja hizo sheria na taratibu. Kitu ambacho ni kosa.
 
Kwani hilo gari ni nani kathibitisha kuwa ni la serikali ambalo alilikataa?
Tuseme kwa kuwa ni VX basi ndio tunahalalisha kuwa ni la serikali lile ambalo alilikataa?Anaweza kuwa anatumia gari jingine tu na heshima yake kama kiongozi wa kambi ya upinzani ikiendelea kwa maana namba za hilo gari kubandikwa kama tuonavyo katika picha.
 
Back
Top Bottom