Kiongozi Wa Juu Wajiuzulu Kwa Ufisadi Pia? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kiongozi Wa Juu Wajiuzulu Kwa Ufisadi Pia?

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Haika, Apr 21, 2008.

 1. H

  Haika JF-Expert Member

  #1
  Apr 21, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Naomba kuuliza swali:
  Je viongozi wa juu kama rais, Rais wa Zbar wakitajwa kwenye kashfa wana JF mnaweza kuwashadidia hadi wajiuzulu?
  Mfano kama ripoti ya Richmond ambayo haikusomwa, imevuja mtaani na inamtaja Rais kuwa anahusika moja kwa moja na sakata hilo, je kuna mechanism itakayoweza kuuliza maswali? au tutapata kigugumizi?
  Je akiondoka (mfano) itakuwaje? nani atashika nchi?
  Kwa kweli nimewaza sana hadi naogopa, manake tusijeanza kugombea madaraka hadi tukawa kama Somalia, hatutawaliki, manake kama mnavyojua katiba yetu inaviraka ambavyo vinatafsirika kwa kila dizaini, kutegemea unazungumzia nini, na unalenga nini.
   
 2. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #2
  Apr 21, 2008
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  God forbid my sistah!! That we should end up like Somalia and the likes
  Lakini kama ikibidi nae atastaafu. It is said kuwa JK ndiye anayewahimiza hawa jamaa wastaafu....something is cooking, labda na yeye yuko on the way out... hii ni regime ya kujiuzulu, kama ya Baba wa taifa ilivyokuwa ya kung'atuka. TZ setting the trend, kama kawa
   
 3. Kubwajinga

  Kubwajinga JF-Expert Member

  #3
  Apr 21, 2008
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,190
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Haika,
  Kama una data wewe lete tu, watashambuliwa mpaka waondoke. Lolote linaloingia hapa haliachiwi mpaka liive na kutumbuka.

  Katiba inajitosheleza kwa nani atashika madaraka badala yao kwa hiyo hilo wala lisikupe shida. Somalia shida yao sio ufisadi, shida yao kubwa ni ukabila hasa ule wa kundi moja kujiona ni bora kuliko lingine na kutaka kutawala wenzao.
   
 4. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #4
  Apr 21, 2008
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Haika, kwa upande wa Rais kweli ni kigugumizi, kwani tumemuona Mkapa watu walisema lakini wapi, tatizo ni kwamba katiba yetu inaonesha kuwa Rais anakuwa na madaraka makubwa, ujue yeye ndiye anayewateua mawaziri, wakurugenzi wakuu wa mikoa hata wilaya
   
 5. M

  Myujumi Juma Member

  #5
  Apr 25, 2008
  Joined: Oct 31, 2007
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hili halina tatizo hapa JF. Leta data za kutosha za kujenga hoja.

  Hapa naomba waoijua katiba na sheria za nchi vizuri watoe mwongozo. Nafikiri hili ndio swali la msingi sana iwapo Raisi anatakiwa achukuliwe hatua.

  Hali ya Somalia sidhani kama inaweza kutokea katika nchi yetu labda yaktokea mapinduzi ya kijeshi, hivyo usiwe na hofu!

  Nafikiri mjadala uende kwenye swali la msingi, "je kuna mechanism itakayoweza kuuliza maswali?"
   
 6. Single D

  Single D JF-Expert Member

  #6
  Apr 25, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 459
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35

  Haika hata kama Rais ataachia ngazi,wapo wa TZ wengi wenye uwezo wa kuongoza na tukafika salama tuendako.
  Soma katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 37:5

  (5) Endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais
  kufariki dunia, kujiuzulu, kupoteza sifa za uchaguzi au kutomudu
  kazi zake kutokana na maradhi ya mwili au kushindwa
  kutekeleza kazi na shughuli za Rais, basi Makamu wa Rais
  ataapishwa na atakuwa Rais kwa muda uliobaki katika kipindi
  cha miaka mitano na kwa masharti yaliyoelezwa katika ibara ya
  40, kisha baada ya kushauriana na chama cha siasa anachotoka
  Rais atapendekeza jina la mtu atakae kuwa Makamu wa Rais na
  uteuzi huo utathibitishwa na Bunge kwa kura zisizopungua
  asilimia hamsini ya Wabunge wote.
   
Loading...