Kiongozi wa juu wa Iran Khamenei amuambia Trump hawatishiki, asubiri tarehe 10 February watamuonesha

mcomunisti halisi

Senior Member
Jan 17, 2017
103
328
kiongozi wa juu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei ameyapuuzia tahadhari alizotoa Trump kwa Iran ya kuacha kujaribisha makombora,Khamenei amesema rais wa US amedhihirisha wazi uso kamili wa marekani ya ufisadi.

''Tunamshukuru Trump kwa kuturahisishia maisha kwa kutuonyesha uso kamili wa Marekani''-Khamenei aliuambia mkutano wa makamanda Tehran

''wakati wa kampeni zake za uchaguzi na baada ya uchaguzi ,amethibitisha yale ambayo tulikuwa tunayasema kwa zaidi ya miaka 30 kuhusu siasa,uchumi,tabia na ufisadi wa kijamii uliopo katika uongozi wa US

''Hakuna adui atakayeweza kudhoofisha taifa la Iran''-alisema Khamenei

''Trump amesema tuwe waoga kwake yeye?Hapana! Watu wa Iran watajibu maneno yake siku ya tarehe 10 na wataonyesha msimamo wao dhidi ya vitisho ya aina hizo-''Khamenei

NB:Tarehe 10 february ni siku ya kuadhimisha mapinduzi ya Iran ya mwaka 1979, hivyo tetesi zinasema watajaribisha na kurusha makombora yao mapya na silaha zingine mapya walizotengeneza.

Rais wa USA hivi karibuni alisema Iran wanachezea moto kwa tukio la Iran kufanya majaribio ya Balistic missiles licha ya white house kusema Iran hawakuvunja moja kwa moja makubaliano ya Baraza la usalama la umoja wa mataifa lakini kurusha makombora yenye uwezo wa kubeba vichwa vya nyuklia unavunja hamasa ya amani,
 
Hii mikwara mpaka lini si wafanye hata pambano la kirafiki lakini sijui iran kikinuka ataweza kuhimili hii kolabo matata UK FRANCE GERMANY ISRAEL US CANADA POLAND ETC
 
Kumbe hadi kwa kolabo?, kwanini asiende pekeake?, usupa power hadi kwa kolabo?.
 
Mbona iran majigambo ni mengi sana unatafuta nini iran au unataka uwahi zile bikira 72
 
kiongozi wa juu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei ameyapuuzia tahadhari alizotoa Trump kwa Iran ya kuacha kujaribisha makombora,Khamenei amesema rais wa US amedhihirisha wazi uso kamili wa marekani ya ufisadi.

''Tunamshukuru Trump kwa kuturahisishia maisha kwa kutuonyesha uso kamili wa Marekani''-Khamenei aliuambia mkutano wa makamanda Tehran

''wakati wa kampeni zake za uchaguzi na baada ya uchaguzi ,amethibitisha yale ambayo tulikuwa tunayasema kwa zaidi ya miaka 30 kuhusu siasa,uchumi,tabia na ufisadi wa kijamii uliopo katika uongozi wa US

''Hakuna adui atakayeweza kudhoofisha taifa la Iran''-alisema Khamenei

''Trump amesema tuwe waoga kwake yeye?Hapana! Watu wa Iran watajibu maneno yake siku ya tarehe 10 na wataonyesha msimamo wao dhidi ya vitisho ya aina hizo-''Khamenei

NB:Tarehe 10 february ni siku ya kuadhimisha mapinduzi ya Iran ya mwaka 1979, hivyo tetesi zinasema watajaribisha na kurusha makombora yao mapya na silaha zingine mapya walizotengeneza.

Rais wa USA hivi karibuni alisema Iran wanachezea moto kwa tukio la Iran kufanya majaribio ya Balistic missiles licha ya white house kusema Iran hawakuvunja moja kwa moja makubaliano ya Baraza la usalama la umoja wa mataifa lakini kurusha makombora yenye uwezo wa kubeba vichwa vya nyuklia unavunja hamasa ya amani,
Kwani Khamenei ni kiongozi wa juu Iran? Ayatollah ni kiongozi wa kiroho
 
Shughuli ipo hapa; Urusi ni rafiki wa karibu ma Iran, USA ya sasa inataka ushirika wa karibu na Urusi; USA kuipiga Iran maanake ni kuzuia maslahi ya Urusi so it means uadui kati ya Urusi na USA but again Urusi na USA wote ni wazungu while Iran ni Mshia/Muajemi, Je Mzungu (Urusi) yupo tayari kumsaliti mzungu mwenzie (USA) kwasababu ya Mshia/Muajemi? Time will tell, sisi nchi masikini ngoja tusubiri though mafuta yatapanda bei tena hata huku kwetu. Mungu pishilia mbali kwa hili ingawa tena USA asipomshikisha adabu Mwirani (sijui kosa lake lakini) atadhaniwa kaogopa mkwara wa Ayatolla.
 
Back
Top Bottom