Kiongozi wa juu wa Iran awakosoa Rais Biden, Trump asema wameharibu sifa ya Marekani

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
1644392573781.png

Picha: Ayatollah Ali Khamenei

Kiongozi wa juu kabisa mwenye usemi wa mwisho nchini Iran, Ayatollah Ali Khamenei, amewatuhumu Rais wa sasa wa Marekani, Joe Biden, na mtangulizi wake, Donald Trump, kwa kuiharibu sifa ya Marekani.

Ukosoaji huo wa moja kwa moja ni hatua ya nadra kufanywa na kiongozi huyo wa Iran dhidi ya viongozi wa Marekani.

Shirika rasmi la habari la serikali nchini Iran, IRNA, limeripoti kwamba Khamenei amesema katika kipindi hiki Marekani inakabiliwa na changamoto kwa namna ambayo haijawahi kushuhudia na kwamba viongozi wake wawili ambao ni Rais wa sasa na mtangulizi wake wameshikana mikono kuiharibu sura ya Marekani.

Hata hivyo, kiongozi huyo wa juu wa Iran hakutowa ufafanuzi zaidi wa alichokisema.

Iran na Marekani zimerudi tena kwenye meza ya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja Mjini Vienna hii leo, lengo likiwa ni kufufuliwa Mkataba wa Nyuklia wa mwaka 2015 ambao Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump, aliukataa mwaka 2018.
 
Hata hivyo kama marekani imeanza kukondakonda hivi.
 
Back
Top Bottom